Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Ndege zina services schedule zake kila baada ya miaka kadhaa (ni vitu ambavyo avikwepeki) ndio maana unawasikia wakipiga kelele kufufua hangar la Arusha kupunguza hizo gharama za kupeleka ndege Canada.

Service zipo lakini sio kwa gharama Hizo endapo ndege zingekuwa mpya, lakini ndege za Tanganyika ni ndege feki mitumba ndiyo maana wajanja wameamua kupiga bilion 13 kijanja janja
 
Mliambiwa mandege mnauziwa ya mitumba mkaanza kupiga kelele haya sasa ndge hazina hats miaka miwili tayari zinapelekwa gereji.haya ni matumizi mabaya ya Fedha za umma
 
Acha ushamba ndege mpya huwa haina ujinga huo, ndege mpya huwa na guarantee miaka kadhaa ya service bure, lakini mtukufu malaika toka chato alinunua vindege magalasha haijapita hata miaka miwili vimeanza kuleta njaa kwa wananchi pesa za walipa kodi bilion 13 zinaibiwa kisanii kwa kisingizio cha kupeleka ndege mitumba Canada ni aibu kwa CCM kuendelea kuwadharau watanzania kuwafanya ni mbumbumbu sana hawajitambui
Matusi ni kuchelewa kunywa dawa? Ufisadi unaweza ku prove? wanasiasa wa bongo hamvutii kwa sababu ya kuwa na akili kama washirikina.....
Inama usome hiyo link uone miles ngapi zinafaa kwa maintenace....
https://www.aircraftcostcalculator.com/media/106417/acc_report_q_series.pdf
 
Someni kilichomo ndani msisome heading na kuanza kukosoa au kupongeza, don’t judge the book from its cover neither should you judge the content from its heading, you have to read the whole story and find the facts there in stipulated

The headings aka titles are therefore meaningless?
 
Wakuu Habari zenu, anaejua hii shule ilipo au jina lake tafadhali nijuze
PIC SHULE.jpg
 
Acha uongo,hiyo ni ile ndege ya pekee ambayo atcl walikuwa nayo kabla Serikali haijaanza kununua zingne.usiwe unaongea kitu bila kuchunguza

Sent using Jamii Forums mobile app

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
...soma vizuri sio kila kitu kuunga juhudi..
 
Kukarabati ndege ni jambo la kawaida. Ila hapa ndipo tutapojifunza kuwa biashara ya ndege ni zaidi ya kununua tu ndege lukuki.

Na ndiyo maana mashirika mengi huwa hata ndege zao ni za kukodisha, eg south africa airways. Kazi ya kampuni ya ndege inatakiwa iwe ku-manage routes zenye faida na kuhakikisha ndege zinakuwa angani zikiwa zimejaa abiria kila wakati. Najua wengi hamtaelewa mpaka muone.
Tanzania ni nchi ambayo mungu ameibariki sana maana kila mmoja wetu ni mtaalam wa kila kitu.
Any way hebu tuangalie habari ifuatayo;
The A220 is the first passenger plane to receive ETOPS certification from Transport Canada, allowing A220 operators to fly up to 180 minutes away from the nearest airport.
"The fact that we are talking about the only model in its long-haul segment, as well as abrupt approaches, offers new opportunities for routes to airlines," said Rob Dewar, Head of Engineering and Customer Support, A220. Thus, the ETOPS 180 certification allows A220 operators to start new routes without limitations, routes over water stretches or distant regions, currently unchecked.
Powered by the Pratt & Whitney PW1500G engines and offering between 100 and 150 seats, the Airbus A220 delivers 20% less power than the previous generation of aircraft. Autonomy is up to 5920 km, depending on the version. So far, Airbus received 537 orders for the A220 range (-100 and -300).
 
Hujui kitu, tumeambiwa ndege zimeingiza bilioni 4.5 kama faida (hii nayo ni uongo kwasababu ATCL inaendeshwa kwa hasara kubwa).

Leo zinaenda kukarabatiwa kwa bilioni 14! Huu ni unyani tu, hakuna kingine.

Tunaoibiwa hapa ni wananchi, waliozinunua bila utaratibu wametajirika sana kwa kupiga cha juu. Na hata haya matengenezo wanaweka cha juu.
Ni suala la muda tu hili shirika litakufa kwa aibu kubwa.
Hayo ni maneno yasiyo na ushahidi na ni ukasuku wa hali ya juu na zaidi ya yote Katesya, DUA LA KUKU HALIMPATI MWEWE NA LAANA ISIYO NA HATIA HAIFANYI KUSUDIO LAKE.
 
Acha ushamba ndege mpya huwa haina ujinga huo, ndege mpya huwa na guarantee miaka kadhaa ya service bure, lakini mtukufu malaika toka chato alinunua vindege magalasha haijapita hata miaka miwili vimeanza kuleta njaa kwa wananchi pesa za walipa kodi bilion 13 zinaibiwa kisanii kwa kisingizio cha kupeleka ndege mitumba Canada ni aibu kwa CCM kuendelea kuwadharau watanzania kuwafanya ni mbumbumbu sana hawajitambui
Fuata link hizi bro. ukizisoma vizuri, utagundua kwa mm Zitto alisema vile.
Contact us | Bombardier Business Aircraft

1. Pre owned aircraft foe sale By Bombadier Co.
Browse pre-owned jets | Bombardier Business Aircraft
 
Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

14JAN 2019

Bombardier kukarabatiwa 
Canada kwa bilioni 13.9/-

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).


WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.


“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.


Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.


Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo.
Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.


“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.


Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.




Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.


Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi.
“Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.


Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege.
Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.


Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.


Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.

Vingezo kwa wahudumu wa ndege viwe:1. Fluent in spoken English and French/Spanish is an added advantage. 2. ‘A’ secondary education however a person with a diploma is an added advantage. Bila hivo tutakuwa tunajenga misingi mibovu, dunia ipo kiganjani!
 
Vingezo kwa wahudumu wa ndege viwe:1. Fluent in spoken English and French/Spanish is an added advantage. 2. ‘A’ secondary education however a person with a diploma is an added advantage. Bila hivo tutakuwa tunajenga misingi mibovu, dunia ipo kiganjani!
meaning?
 
Back
Top Bottom