Sh 11.6 trilioni zapotea kifisadi TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sh 11.6 trilioni zapotea kifisadi TANZANIA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Apr 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Send to a friend Tuesday, 20 April 2010 07:42 0diggsdigg

  [​IMG]Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo

  Na Mwandishi Wetu

  TANZANIA imeshapoteza Sh11.6 trilioni, ikiwa ni wastani wa Sh289.3 bilioni kila mwaka kutokana na ufisadi, ukwepaji kodi na mzunguko wa fedha haramu, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi moja ya Marekani.Fedha hizo ni mara mbili ya fedha zilizoibwa kutoka kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika kipindi cha mwaka 2005/06.
  Taarifa hiyo ya taasisi ya Global Financial Integrity yenye kichwa cha habari kisemacho

  "Illicity Financial Flows from Africa: Hidden Resources for Development (Mtiririko Haramu wa Kifedha Kutoka Afrika:Rasilimali za Maendeleo Zilizojificha)", imesema katika utafiti huo kuwa fedha hizo zimekuwa zikipotea kwa miongo minne na hivyo kufanya fedha zote zilizopotea katika kipindi hicho cha miaka 40 kufikia Sh11.6 trilioni, au kwa maneno mengine Sh11,000 bilioni.

  Kwa mujibu wa utafiti huo ulioripotiwa na gazeti la The East African toleo namba 807 la Aprili 19 hadi 25 mwaka huu, utafiti huo ulifanywa na timu ya uangalizi wa fedha ya Marekani katika maeneo ya mzunguko wa fedha haramu, ukwepaji wa kodi, ufisadi serikalini na shughuili nyingine haramu.

  Utafiti umeonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kupoteza fedha katika maeneo hayo kwa nchi za Afrika Mashariki, ikifuatiwa na Kenya iliyopoteza dola 7.3 bilioni za Kimarekani(sawa na Sh9.5 trilioni za Kitanzania) na Uganda iliyopoteza dola 6.4bilioni za Kimare

  kani ambazo ni sawa na Sh 8.32 trilioni.Mahesabu yaliyofanywa kulingana na matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kuwa nchi hizo tatu za Afrika Mashariki, zimepoteza dola za Marekani 22.6 bilioni, sawa na Sh29.4 trilioni katika kipindi hicho.

  Utafiti huo umeeleza kuwa madhara ya kupotea fedha hizo, yanawaumiza wananchi wengi katika nchi hizo ambazo zote ni masikini.

  Ripoti imeonyesha pia kuwa Tanzania inashika nafasi ya 13 kati ya nchi 15 zinazoongoza kwa matumizi haramu ya fedha baada ya Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Cameroon, Ivory Coast, Ethiopia, Gabon, Ghana, Madagascar, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini na Sudan. Zambia na Zimbabwe zinashika nafasi ya 14 na 15.

  Hata hivyo Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo aliliambia gazeti hilo la The East African kuwa serikali imeanzisha kitengo cha intelijensia ya fedha kuongoza mapambano dhidi ya mzunguko wa fedha haramu nchini.

  "Tatizo hili lipo, katika ngazi ya taifa na ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), tumeliona hili tatizo kwa muda mrefu na tumeamua kuungana kupambana nalo," alisema Mkulo.

  Msemaji wa Global Financial Integrity ameeleza kuwa kiasi cha fedha kilichopotezwa na nchi hizo tatu kinaweza kuwa zaidi ya mara mbili ya Sh29.4 trilioni kama njia nyingine haramu zingetajwa kwenye ripoti hiyo.

  Utafiti huo unaonyesha kuwa rushwa na wizi unaohusisha wafanyakazi wa serikali unachangia asilimia tatu ya matumizi haramu ya fedha zinazovuka mipaka.

  Ripoti hiyo imebainisha kuwa nchi za Afrika pekee hupoteza dola 854 bilioni za Kimarekani kwa matumizi haramu, huku nchi tano zinazoongoza zikiwa ni Nigeria (dola 89.5 bilioni), Misri (dola 70.5 bilioni), Algeria (dola 25.7 bilioni), Morocco (dola 25 bilioni) na Afrika Kusini (dola 24.9 bilioni).
  http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/803-sh-116-trilioni-zapotea-kifisadi.html

   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Hii sra ya huyu jamaa inaonesha kutokuwa na uwajibikaji. Tangu amemreplace yule mama mambo ni yaleyale tu. Na Kinara wao yuko USA kakwama!
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hesabu hii ya huakika? mbona inatisha na kuumiza kichwa sana.


  sina mengi ya kusema zaidi ya kuwajibika kwangu kupitia kura yangu na kumuachia Mungu.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Viongozi wetu kamwe hawawezi kusema ukweli, ya Mkulo kusema eti wameanzisha kitengo cha intelejensia wapi Mkulo hao unaowasema waliamua kula haramu kwenye EPA ije leo kufanya kazi, wameokoka lini hadi kuwa na uadilifu wa kuweza kutenda yale mazuri yanayotizamiwa na WTZ. Mie binafsi natilia shaka uwezo na upeo wao juu ya masuala ya hela haramu. Usipoteze muda kuanzisha sijui intelejensia shughulika kwanza na watumishi kwenye wizara yako kwanza hao wa kimataifa huwawezi jenga kwanza uwezo wa kudhibit mambo ya ndani
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Kikwete alisema hajui ni kwa nini Tanzania ni maskini alipoulizwa swali hilo Europe. Leo amepewa jibu kwamba ni UFISADI, UKWEPAJI KODI na MZUNGUKO WA FEDHA HARAMU. hatutaki huko kujikanyaka kama alivyoanza mkulo kwamba serikali ilishajua ni fedha haramu. Mbona hataji ufisadi na ukwepaji wa Kodi? Kikwete afanyie kazi sababu hizo kama kweli anania ya kustawisha tanzania ambalo ndo jukumu lake kuu kikatiba kama rais.hatutaki serikali ina MIKAKATI kama alivyoanza kusema mkulo.Tunataka kusikia serikali IMEFANYA Hiki.
   
 6. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hiyo kwenye red nimeipenda zaidi. Tunahitaji hilo kwa watu wote duniani ili dunia iwe mahali salama pa kuishi, watu wakiishi na kutenda haki kama MUNGU atakavyo.
   
 7. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Duh, hii sasa ni songombingo! 11 trillion zimeishia mikononi mwa wajanja! Ndio maana mahekalu yanajengwa kila siku, huku wadanganyika wanaendelea kufa na njaa. Hii hali inasikitisha kwa kweli.
   
Loading...