Duh vijana wanakimbia sana. Haya ndio magari wana deliver kwa wateja wa Tz?Mimi huko wanaanita kobe ndio natembea 180km/h mguu naweka hapo vijana wanaenda 220 na kuendelea wengine wanamaliza sahani ila wanatoa macho kama fundi saa wakifika Tunduma macho kama wamemwagiwa mchanga..
Amin Amin brotherHii inaweza kutokea ila tusiombee.
Nataka kujua kama mbongo anaweza kuhatarisha Maisha yake na Mali zake kisa Fame ?Does it matter? If it's blacks or brown?
Foleni na kadhia nyingi tu barabrani ambazo zinafanya hayo madhindano kutokuwa na uharisia labda kama wana mambo yao mengineUnaweza kukutana na foleni ya malori 5km
Daa, Nchi hii imebadilika sana, tuendako ni pazuri zaidi. Nchi ina vijana wenye ujasiri sanaWamatumbi. Mkuu Gen Z huwajui? Wana vurugu na magari yao huko barabarani balaa. Halafu wanapost kwemye pages zao za Instagram bila woga wala aibu.
Wanajaribu kuonesha kuwa pamoja na changamoto za barabara unaweza kufika Dodoma kabla ya treni. Sio mashindano ya mwendo kwasabbau inajulikana train ni 160kph na BMW inaweza kwenda hadi 240kph.Foleni na kadhia nyingi tu barabrani ambazo zinafanya hayo madhindano kutokuwa na uharisia labda kama wana mambo yao mengine
Wanakimbia balaa wanaweza kutoka alfajir ya leo Johannesburg na wakafika keshokutwa usiku Tunduma kama Kazungula waliwahi kutengeneza documents maana pale ndio wanalaza watu wana mtandao upo chini sana..Duh vijana wanakimbia sana. Haya ndio magari wana deliver kwa wateja wa Tz?
Hahaha. Hapana mkuu. Akili kisoda hao. Labda ingekua straight line, ndio wangesema wajaribu ila ukiangalia matuta, foleni, trafiki, barabara mbovu, kona, hainamke sense.. ata ukijitahidi sana ukatumia 8 hours wewe umeendesha vibaya sana na risk ni kubwa sana..Mad Max haupo kwenye kamati ya hii ligi?
Uko sahihi kabisa broTop gear walitumia gari sikumbuki ni ipi ila ni high end kushindana na Euro star train. Wote walianzia sehemu moja. Ingine walishindanisha Buggati na zile ndege ndogo. Sikumbuki nani alishinda.
Ninayokumbuka ni Buggati vs Typhoon fighter jet. Race ya 1mile kwenda na kurudi. Ndege inaruka juu 1m na inarudi chini 1mile kuvuka mstari. Buggati ilichapwa na ile ndege kama utani.
Gari itayotumika ni BMW X3 ,N55 six inline engine, turbocharged yenye eight speed transmissionNaona hoja yako ina mantiki. Kama wanatangulia masaa mawili, basi ushindani unabadilika kabisa.
Kwa mfano:
Ordinary SGR: huondoka saa 12:00 asubuhi na kufika takribani baada ya saa 4 (karibu saa 10:00 AM).
BMW: linaondoka saa 4:00 asubuhi.
Hii ina maana gari lina dirisha la saa 6 (kuanzia saa 4:00 hadi saa 10:00) kufika Dodoma kabla ya treni. Kwa umbali wa takribani km 450, wastani unaohitajika ni karibu 75 km/h, ambao unaweza kupatikana kwa kuendesha kwa utulivu, ukizingatia vituo, msongamano, na sheria za barabarani.
Ndiyo maana watu wengi wanaweza kusema kwamba:
Kama lengo ni "kufika kabla ya treni", kuondoka masaa mawili mapema kunafanya changamoto iwe rahisi zaidi.
Kama lengo ni "kuonyesha gari lina kasi kuliko treni", basi kulinganisha kungekuwa na maana zaidi kama vyote vingeondoka kwa wakati mmoja. Hapo ndipo ungehitajika kudumisha wastani wa zaidi ya 110 km/h, jambo ambalo si rahisi na linaweza kuwalazimisha madereva kuendesha kwa kasi zisizo salama katika baadhi ya sehemu za barabara.
Kuhusu BMW X3 F25, toleo hilo linaweza kuwa na injini tofauti kulingana na mwaka na soko:
N20 – petroli 2.0 turbo.
N47 – dizeli 2.0 turbo.
N55 – petroli 3.0 turbo (hutumika kwenye matoleo yenye nguvu zaidi kama X3 xDrive35i).
Hata hivyo, aina ya injini siyo jambo kuu kwenye changamoto ya aina hii. Kinachoamua zaidi ni usalama, sheria za barabarani, hali ya barabara, na muda wa kusimama njiani.
Kwa mtazamo wangu, kama ni maudhui ya burudani na wanazingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani, hakuna tatizo. Lakini kama ushindani unawahamasisha watu kuendesha kwa kasi kupita kiasi ili "kuishinda treni", hilo si jambo la busara. Treni ina faida ya kutokukutana na foleni, makutano, au magari mengine, wakati dereva wa gari lazima azingatie sheria na hali halisi ya barabara.