SGR kwenda Rwanda kuna Busara?

SGR kwenda Rwanda kuna Busara?

Wanajukwaa,

Nimepitia takwimu kutoka the National Bureau of Statistics (NBS) na Tanzania Ports Authority (TPA) kuhusu mizigo / shehena yanayopitia bandari za Tanzania kwenda au kutoka nchi za jirani.

Kwa mwaka 2017/18, jumla ya tani 5.6 million zilipitia Tanzania (bandari ya Dar es Salaam pekee) kwenda au kutoka nchi za jirani, ikilinganishwa na tani 4.8 million mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la asilimia 17.1 na ni habari njema kabisa kwa TPA na nchi yetu kwa ujumla.

Ukiangalia mchanganuo wa shehena zinazoenda au kutoka nchi za jirani, asilima 61.1% ni za Zambia (36.6%) na J.D. Kongo (24.4%). Hii ni zaidi ya tani 3.4 million ambazo kwa asilimia kubwa zinawafikia jirani zetu kupitia barabara zetu hapa Tanzania. Ukipitia takwimu za 2017/18, TAZARA imefanikiwa kusafirisha mizigo ya tani 187,558 tu (3.4% ya 5.6 million) kwa njia ya reli.

Shehena za Rwanda ni asilimia 16.5% pekee (au tani 922,134) kwa mwaka wa 2017/18. Ukilinganisha na 2016/17, kuna upungufu wa 9.0% - kitu ambacho kinaashiria kuwa mizigo ya Rwanda inawezekana kuwa inapitia Kenya na Uganda.

Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za NBS na TPA wenyewe.

Naomba mwenye taarifa kuhusu ya haya maamuzi ya kupeleka SGR Rwanda atujulishe zaidi.

Nawasilisha.
Uko deep. Nimependa analysis yako. It goes without say kuwa SGR kuanza kwa kuipeleka Rwanda ni uzwazwa. Tunaacha kwenye mzigo mkubwa tunakimbilia Rwanda kwa sababu za kiurafiki tu?
Iko wapi Feasibility study iliyopelekea tukaenda Rwanda?
 
Meta Mada utakuwa ki desk officer kijinga kijinga cha serikali au kibaraka cha Zitto Kabwe. Wafanyabiashara wa Tanzania tunataka hiyo reli ya route ya Rwanda. Kuna fursa kibao kwa wafanyabiashara wa Tanzania kubwa mno
Mleta mada amekuja kwa data, nyie mnakuja na sweeping statements. Ridiculous, you are not great thinkers and you don't belong in this forum. Nendeni kwenye udaku na mahusiano
 
Sasa unaipataje DRC Congo bila kupitia Rwanda/Burundi?
Kuna economic zones 2 kubwa za DRC, iko ya Katanga/Lubumbashi province ambayo unapita Kitwe Zambia na hii ndiyo ina mzigo mkubwa. Nyingine ndiyo hiyo ya Goma/ Bukavu ambayo hata kwa kutokea Kigoma kwa Meli unafika.
 
Nadhani maswali yanajibiwa kwa data, na anayeuliza anataka kujua..., hii hulka ya kila anayeuliza kuonekana anapinga ndicho kilichomfaya yule Emperor kutembea uchi na kutoambiwa kwa sababu ya watu kuogopa kuongea ukweli wao..
Watanzania awamu hii wamekuwa wajinga sana. Kila anachojua Jiwe wanadhania kama genious kumbe ana uelewa finyu wa issues hasa za uchumi.
 
Kwani huko nchini Rwanda hawakai Binadamu / Watu ambao wanahitaji Huduma? Hivi Watanzania nchi ya Rwanda, Wanyarwanda na Rais wa Rwanda wamewakoseeni nini? Hivi Rwanda ndiyo imewafanya muwe Wavivu, Lege Lege, Goi Goi, Dhaifu Dhaifu na Watu mnaochelewa Kutwa kupiga hatua Madhubuti za Kimaendelo huku mkiwekeza mno katika Majungu, Chuki, Wivu na Uswahili wenu badala ya Kujikita kuangalia kwanini kwa muda mfupi tu huu Rwanda chini ya Rais Paul Kagame inawaacheni Kimaendeleo na hata Wananchi ( Raia ) wake wanazidi kuwa na ' Fikra ' pana kuliko wengi wenu ( japo wapo baadhi wenye Akili kubwa kama za Wanyarwanda ) ila ni wa kuwatafuta sana tena kwa Tochi?
Ni kupoteza muda kujilinganisha na Rwanda. Wanachotuzidi ni UDIKTETA tu. Vingine hivi mnawa over rate unnecessarily.
 
Sina chochote dhidi ya nchi ya Rwanda. Naangalia data na kufanya mchanganuo. Moja, Rwanda is already in business with Uganda and Kenya. Pili, shehena za Rwanda ni tani laki 9 tu. Hatuwezi kulinganisha na laki 9 za Rwanda na tani milion 3.4 kwenda DRC na Zambia! Ni ukichaa!

Fikiria uamuzi wa kuongeza Terminal III ya Julius Nyerere International Airport. Terminal II ilikuwa imezidiwa kikomo chake cha wasafiri milioni 1.5 kwa kusafirisha zaidi ya watu million 2.4 - ilikuwa inatuumiza sana! Ni uamuzi wa busara kabisa ambao uko supported na data! Terminal III mpya ina uwezo wa kuhudumia wasafiri million 6 - kwa hiyo tutakuwa nayo kwa miaka mingi tu. It is a good investment with a solid business case.
Hakuna takataka ya kujibu hoja zako mtoa mada. Uko deep sana, wengi humu ni praise and worship team ya awamu ya 5. Nimekukubali sana Mkuu, uko real na very factual
 
Vipi umefanya consideration ya maeneo mengine ya territory ya Tanzania ambapo reli hiyo itapita?.. maeneo hayo pia yatafaidika na Huduma hiyo zaidi kuliko huko Rwanda.. nimekuwa nikiona jinsi maeneo ya pembezoni mwa nchi yanavyobezwa Kwa uduni wa maendeleo, Sgr itachochea maendeleo ya maeneo hayo..Kwa mfano ni gharama kubwa Sana kusafiri kutoka Dar mpaka Ngara,karagwe, au muleba na Bukoba, average money spent kusafiri au kusafirisha bidhaa ni kubwa Sana..its cheaper to trade between Dar na China kuliko Dar na Kagera..SASA nadhani hacha hii miundombinu ije iwasaidie watu wa jamii hizi ku utilise bongo zao kufanya maendeleo..Rwanda can be a Terminal ya SGR Lakini katikati watanzania wengi watapata unafuu wa kusafiri/kusafirisha bidhaa zao to/from their zones.. sometimes you have to invest a lot ili uibue opportunities na kuamsha amsha the sleeping giants which is awesome for our blessed country...Tuendelee pamoja.
Biashara ya Reli ni mizigo wala siyo abiria. Abiria ni huduma tu. Huwezi kupata Return on Investment kwa kubeba abiria. Je hapo ulipopataja pana any substancial economic activities kama viwanda? Sana sana naona njiani kuna pamba tu!!
 
Nakuelewa..SGR sio bure pesa imekopwa nyingi tuu na almost miradi mingi iliyotapakaa nchi hii especially ya barabara ni mikopo, SASA hii network inatibu vitu vingi Sana, itapunguza uharibifu wa barabara , itapunguza gharama za usafirishaji lakini kubwa zaidi itarahisisha muingiliano wa watu wa maeneo inapopita( itachochea intertrade)..mi nadhani uwe positive na hii kitu ili as the Country tuweze Kudevelop pamoja hakuna haja maeneo mengine yasubiri Sana bila kuchangia maendeleo ya nchi..we need to pull/push together.
Una point ila mleta mada anaongelea priority!! Kipi kianze na kipi kifuate
 
Mleta mada ni matokeo ya elimu duni iliyokuzawadia cheti tu bila uwezo mkubwa wa kufikiri.

SGR kuelekea Rwanda?!usiangalie inapoishia tu,umeshindwa kufikiri huku njiani inakopita ni watu wangapi wanahitaji huduma ya reli hii?

Unajua population ya kanda ya ziwa , kanda ya kati na magharibi ni zaidi ya asilimia sabini ya population ya nchi nzima?

Najua unataka kutuonesha kuwa maamuzi haya hayakuwa sahihi ila naona ni fikra za chuki tu zimekusukuma kuandika hayo
Wewe ni mburura tu. Soma mada za wenzio upite, huna uwezo wa kuchangia hii mada.
 
Biashara ya Reli ni mizigo wala siyo abiria. Abiria ni huduma tu. Huwezi kupata Return on Investment kwa kubeba abiria. Je hapo ulipopataja pana any substancial economic activities kama viwanda? Sana sana naona njiani kuna pamba tu!!
Last time I checked Sir Richard Branson amefanya mageuzi makubwa ktk usafiri wa treni za Kasi za abiria na alifanikiwa ku- treble namba ya abiria kutoka 15-40m ndani ya muda mchache..hii SGR wanasema itakuwa inatumia masaa machache kutoka Dar mpaka mikoa ya kanda ya ziwa..SASA nadhani itawawia rahisi abiria kusafiri ata for weekend trip kwenda kuangalia au kufatilia Mambo Yao(ninaamini ule mzoroto wa maendeleo sehemu hizi utaisha)..watu wengi wangependa kuinvest maeneo haya but travel costs na time inawaput off..SGR will cure that.
Please note: mazao mengi mikoa hii yamekufa kutokana na gharama za kuyasafirisha ili yawe exported na maeneo haya yako very fertile Sana mazao yatalimwa Kwa wingi na mzigo utapatikana tuu..na mikakati ipo inatekelezwa on the ground..and mind you wale wafugaji waliojaa mjini kwenye market ya mifugo Yao hutawaona tena..mifugo Bora itakua inafika Dar within hours bila stress ya kukaa njiani muda murefu...ngoja ijengwe.. utafurahia Sana ndugu.
 
Meta Mada utakuwa ki desk officer kijinga kijinga cha serikali au kibaraka cha Zitto Kabwe. Wafanyabiashara wa Tanzania tunataka hiyo reli ya route ya Rwanda. Kuna fursa kibao kwa wafanyabiashara wa Tanzania kubwa mno
Nikichukua mchango wako huuna kuulinganisha na ule aliotoa mleta mada, sina shaka yoyote ya kujua 'mjinga' ni nani.

Acheni mambo ya mihemko ya kisiasa na ushabiki kuyachanganya na maswala mhimu yanayolihusu taifa letu.

Mleta mada kaeleza vizuri kabisa; kaweka na takwimu, wewe unakuja hapa na kuropoka tu kama unatoka chooni.

Sikuuona mchango wako kule kwa mpuuzi mwenzio Paskali. Hayo ndio mnayoyajua, mengine yote hamna taarifa nayo.
 
Nadhani maswali yanajibiwa kwa data, na anayeuliza anataka kujua..., hii hulka ya kila anayeuliza kuonekana anapinga ndicho kilichomfaya yule Emperor kutembea uchi na kutoambiwa kwa sababu ya watu kuogopa kuongea ukweli wao..
Kuna vitu vingine ni common sense..... Reli ya Kati ni yetu tuna maamuzi nayo .... Reli ya Tazara ni ya nchi mbili ukilazimishia kuweka sgr je zambia wata backup plan!!??
 
Shida yetu kama taifa miaka yote ni priorities.

Unakimbilia fursa mpya ilhali uliyonayo tayari hukidhi mahitaji yake! Hiyo siyo biashara ni ubabaishaji tu.

Ndiyo maana mnafunga biashara kila siku.

Hata kwa kutumia common sense tu,Rwamba kuna biashara gani kwa kuliganisha na Zambia?
Nimekuelewa kuwa unasumbuliwa na ubishi bye
 
Last time I checked Sir Richard Branson amefanya mageuzi makubwa ktk usafiri wa treni za Kasi za abiria na alifanikiwa ku- treble namba ya abiria kutoka 15-40m ndani ya muda mchache..hii SGR wanasema itakuwa inatumia masaa machache kutoka Dar mpaka mikoa ya kanda ya ziwa..SASA nadhani itawawia rahisi abiria kusafiri ata for weekend trip kwenda kuangalia au kufatilia Mambo Yao(ninaamini ule mzoroto wa maendeleo sehemu hizi utaisha)..watu wengi wangependa kuinvest maeneo haya but travel costs na time inawaput off..SGR will cure that.
Please note: mazao mengi mikoa hii yamekufa kutokana na gharama za kuyasafirisha ili yawe exported na maeneo haya yako very fertile Sana mazao yatalimwa Kwa wingi na mzigo utapatikana tuu..na mikakati ipo inatekelezwa on the ground..and mind you wale wafugaji waliojaa mjini kwenye market ya mifugo Yao hutawaona tena..mifugo Bora itakua inafika Dar within hours bila stress ya kukaa njiani muda murefu...ngoja ijengwe.. utafurahia Sana ndugu.
Ya nini uende mbali kote huko kwa 'Sir Virgin' na mfano mzuri tunao hapahapa jirani Kenya.

SGR ya kenya imeingiza mara tano zaidi kwa kusafirisha mizigo ikilinganishwa na kiasi kilichopatikana kutokana na kusafirisha abiria.
Kwa hapa Tanzania ukijenga reli ukitegemea pato toka kwa wasafiri pekee bila mizigo hiyo reli itakuwa ni hasara kila mwaka.
 
You've brought neither data nor analysis. Leta takwimu kidogo hapa.
Hizo data alizoleta ni historical data they have nothing to do with the future.Mfano eneo halina duka mkusanya data mjinga atakuletea data mfano za mauzo.za miaka mitatu iliyopita kuwa eneo Hilo halijauza chochote kwa kipindi Cha miaka mitatu Lakini hasemi kuwa halijauza kwa kuwa hamna duka.Takwimu Kama za Mleta mada Ni hopeless hazina reasoning ya uhalisia wa what is underground .Ndio maana any serious bussiness men Kama wachaga,wahindi ,waarabu na wapemba hawatumii takwimu za NBS kufanya Maamuzi yao ya kibiashara wanawaachia hizo takwimu maafisa madesk officer wa serikali na Wana siasa Akina Zitto Kabwe na wapiga filimbi wa hamelini wenzao
 
Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za N
Inaonekana hujui maana ya SGR-ni standard gauge railway!Tazara ni SGR ndio maana mabehewa yake hayawezi kuingia kwenye reli hii ya kati ambayo.ni meter gauge
Kuhusu mizigo ya Rwanda kupita uganda na kenya,ni kwamba tumeshakubaliana nao,SGR itamwaga zigo lao lote bandari kavu ya kahama,halafu wao watachukua kuanzia pale,ambapo ni karibu sana
 
Ulitaka wajenge kuelekea Zambia wakati TAZARA ipo? Huwezi linganisha rail ya TAZARA na Central corridor railway, hii ya Central ni takataka
Pia afahamu kuwa Tazara ni SGR,ndio maana treni za watalii toka south africa zikija tanzania zinatembelea kwenye reli ya tazara,hawashuki na kubadili mabehewa
 
Ni kupoteza muda kujilinganisha na Rwanda. Wanachotuzidi ni UDIKTETA tu. Vingine hivi mnawa over rate unnecessarily.
Rwanda is overrated Sana.
Everything is built around one person. Nothing will work in his absence. That is how NOT to develop a country. Sasa hivi wana ugomvi mkubwa na World Bank kuhusu takwimu zao hewa za uchumi. Things are not adding up.
 
Wewe umeangalia shehena kuelekea Rwanda, Burundi Uganda, DRC ni ndogo umetumia akili yako vizuri kujiuliza kwanini ni ndogo?

Sasa kuna watu wametumia akili zao vizuri kujiuliza kwanini ni ndogo na wakapata jibu kwamba shehena ya kutosha ipo lakini inaenda Kenya sababu a, b, c ndio maana wamekuja na solution ya SGR

Ulitaka wajenge kuelekea Zambia wakati TAZARA ipo? Huwezi linganisha rail ya TAZARA na Central corridor railway, hii ya Central ni takataka
Hapana...Engineer mkuu Magufuli alitupilia mbali feasibility study akaamua kutumia detailed design and construction akaja na jibu. Hakuna kama Engineer John Pombe Magufuli. Sisi wengine ni vilaza wakubwa!
 
Back
Top Bottom