SGR kwenda Rwanda kuna Busara?

SGR kwenda Rwanda kuna Busara?

Sina chochote dhidi ya nchi ya Rwanda. Naangalia data na kufanya mchanganuo. Moja, Rwanda is already in business with Uganda and Kenya. Pili, shehena za Rwanda ni tani laki 9 tu. Hatuwezi kulinganisha na laki 9 za Rwanda na tani milion 3.4 kwenda DRC na Zambia! Ni ukichaa!

Fikiria uamuzi wa kuongeza Terminal III ya Julius Nyerere International Airport. Terminal II ilikuwa imezidiwa kikomo chake cha wasafiri milioni 1.5 kwa kusafirisha zaidi ya watu million 2.4 - ilikuwa inatuumiza sana! Ni uamuzi wa busara kabisa ambao uko supported na data! Terminal III mpya ina uwezo wa kuhudumia wasafiri million 6 - kwa hiyo tutakuwa nayo kwa miaka mingi tu. It is a good investment with a solid business case.
Hivi unajua kuwa mpaka sasa Rwanda inapitia Uganda kwenda Mombasa simply kwa sababu kuna kipande upande wa Tanzania hakuna lami? Hivi SGR ikifika kigali Mizigo yote toka Rwanda itapitia Dar ambapo ni karibu na gharama ni nafuu sana. Uamuzi wa kupeleka SGR kwenda Rwanda ni wa kibiashara zaidi
 
Mjadala ni mzuri.

Nipo upande wa mtoa mada.
Kwa vile wewe naye si wafanyabiashara! Kawaida ya Mfanyabiashara ni kutafuta fursa mpya baadala ya kuridhika na alizonazo. Ndo maana Dalali ukiwa Mteja wake atakuletea Mchanga ukiwa wa mwisho maana kwake hiyo ni ready money na anahangaika na Mteja mpya
 
Kinachoangaliwa hapa ni namna ya kuliteka soko la kusafirisha mizigo ya central Africa ambako tuna washindani wengi ikiwemo hasidi wetu mkubwa Kenya.

Obvious mizigo inayoenda Zambia ni soko letu lisilokuwa na ushindani mkubwa. So ili tuweze kupata na soko la Central Africa ni lazima tuwe na kitu Cha ziada na si kingine Bali kuwa na reli Bora kabisa. Ndiyo maana watendaji wakuu wakaona ni vizuri kujenga SGR kuelekea huko.

Pia ni njia nzuri ya kuwasaidia watz kusafirisha mizigo yao kwenda sehemu mbalimbali ikiwemo Moro, Dom, singida, Shy, mwanza, bukoba na Kagera.

Binafsi naunga mkono SGR kupita njia hiyo.
 
TAZARA ni SGR sema iwe electrified
Kwa nini tusiboreshe TAZARA kufikia kiwango cha SGR? TAZARA inasafirisha tani 187,558 tu wakati ina "potential" ya mamilioni ya tani. Mwaka 2018, Zambia walizalisha copper kiasi cha tani 861,946 (2017 tani 799,329) - halafu tunajua Zambia hawana viwanda vya kuchakata copper. Copper yote inaenda China na nchi nyingine. Je, matani yote haya yalipitia wapi? Je, si kesho kutwa tu Zambia watafikia tani milion moja, moja na nusu, mbili na kuendelea? Je, hatutaki hiyo biashara ya kusafirisha tu? The 2018 copper production hits 861,946 tonnes - Zambia Chamber of Mines

Hapo sijagusa DR Congo!
 
Pia kumbuka kuna njia ya Reli kati ya Angola na Congo ilizinduliwa mwezi wa 4 kama sikosei. Ilikuwepo kipindi cha nyuma ikafungwa.

Kwa sasa kuna shehena kubwa sana ya Shaba inapitia bandari ya Angola
 
Hapo ni Angola na wao wanapambana kukamata mizigo ya Kongo. Hivyo kwa nchi kama kongo ina mibadala mingi sana
20191017_075745.jpeg
20191017_195854.jpeg
 
Kwani huko nchini Rwanda hawakai Binadamu / Watu ambao wanahitaji Huduma? Hivi Watanzania nchi ya Rwanda, Wanyarwanda na Rais wa Rwanda wamewakoseeni nini? Hivi Rwanda ndiyo imewafanya muwe Wavivu, Lege Lege, Goi Goi, Dhaifu Dhaifu na Watu mnaochelewa Kutwa kupiga hatua Madhubuti za Kimaendelo huku mkiwekeza mno katika Majungu, Chuki, Wivu na Uswahili wenu badala ya Kujikita kuangalia kwanini kwa muda mfupi tu huu Rwanda chini ya Rais Paul Kagame inawaacheni Kimaendeleo na hata Wananchi ( Raia ) wake wanazidi kuwa na ' Fikra ' pana kuliko wengi wenu ( japo wapo baadhi wenye Akili kubwa kama za Wanyarwanda ) ila ni wa kuwatafuta sana tena kwa Tochi?
Huwezi linganisha kijiji na Mkoa
 
Kuna mahali nimesoma kuwa uko mbeleni wanategemea kuboresha reli hii iliyopo ya kati nayo iwe SGR, sasa kama ni hivyo hakuna haja ya reli hii mpya kwenda tena kigoma wakati iliyopo itaboreshwa soon, hivyo sioni tatizo hii mpya ikatoa huduma kwa mikoa na wilaya zilizo pakana na burudu na Rwanda, nazani wameijaribu kukwepa duplication huko mbeleni.
 
Iko hivi reli ikienda rwanda ina maana tutapakia mizigo ya Rwanda halafu kuanzia kigali kwenda Goma na Bukavu ni karibu ina maana drc ya huko itapakia mizigo kwetu, pia bujumbura siyo mbali sana na kigali na usisahau hata kampala nayo siyo mbali na kigali,

So wako sahihi, kuhusu reli kwenda kigoma itaenda baadaye maana kule kuna mji wa uvira ambao mahitaji yao kupata bujumbura ni karibu sana, mji wa kalemie ni mkubwa lkn huwez hata kidogo kuufananisha na Goma na Bukavu! Kwa Congo mji wa kwanza kwa population ni kinshasa ambao hatuwez kuufikia, wa pili ni lubumbashi ambao tunaufikia kwa kupitia Zambia, maana kalemie to lubumbashi ni kama hakuna netwrok ya barabara cause iliyopo ni mbaya kuliko maelezo, so mji wa tatu na wa nne ni Goma na Bukavu ambayo iko karibu sana na Kigali!
 
Kwa vile wewe naye si wafanyabiashara! Kawaida ya Mfanyabiashara ni kutafuta fursa mpya baadala ya kuridhika na alizonazo. Ndo maana Dalali ukiwa Mteja wake atakuletea Mchanga ukiwa wa mwisho maana kwake hiyo ni ready money na anahangaika na Mteja mpya
Shida yetu kama taifa miaka yote ni priorities.

Unakimbilia fursa mpya ilhali uliyonayo tayari hukidhi mahitaji yake! Hiyo siyo biashara ni ubabaishaji tu.

Ndiyo maana mnafunga biashara kila siku.

Hata kwa kutumia common sense tu,Rwamba kuna biashara gani kwa kuliganisha na Zambia?
 
Iko hivi reli ikienda rwanda ina maana tutapakia mizigo ya Rwanda halafu kuanzia kigali kwenda Goma na Bukavu ni karibu ina maana drc ya huko itapakia mizigo kwetu, pia bujumbura siyo mbali sana na kigali na usisahau hata kampala nayo siyo mbali na kigali,

So wako sahihi, kuhusu reli kwenda kigoma itaenda baadaye maana kule kuna mji wa uvira ambao mahitaji yao kupata bujumbura ni karibu sana, mji wa kalemie ni mkubwa lkn huwez hata kidogo kuufananisha na Goma na Bukavu! Kwa Congo mji wa kwanza kwa population ni kinshasa ambao hatuwez kuufikia, wa pili ni lubumbashi ambao tunaufikia kwa kupitia Zambia, maana kalemie to lubumbashi ni kama hakuna netwrok ya barabara cause iliyopo ni mbaya kuliko maelezo, so mji wa tatu na wa nne ni Goma na Bukavu ambayo iko karibu sana na Kigali!

Shukran sana. Ila natamani ungetoa data ya kutosha ili mada yako inoge zaidi.
 
Hapo ni Angola na wao wanapambana kukamata mizigo ya Kongo. Hivyo kwa nchi kama kongo ina mibadala mingi sanaView attachment 1236366View attachment 1236367

Ni kweli. Ila masoko ya bidhaa kutoka Kongo yako Mashariki, siyo Magharibi. China and India.

Ukipeleka bidhaa zako Angola kutoka Kongo, inabidi uzunguke tena Afrika Kusini uikamate bahari Hindi mpaka ufike China. It does not make sense. The Dar Port is strategic and preferred. Angalia data kutoka NBS na TPA! Shehena zimeongezeka sana!

Zambia - 20.4%
J.D. Kongo - 20.0%

Ni balaa. Angola will lose money.
 
Shida yetu kama taifa miaka yote ni priorities.

Unakimbilia fursa mpya ilhali uliyonayo tayari hukidhi mahitaji yake! Hiyo siyo biashara ni ubabaishaji tu.

Ndiyo maana mnafunga biashara kila siku.

Hata kwa kutumia common sense tu,Rwamba kuna biashara gani kwa kuliganisha na Zambia?

Mkuu umenena. Rwanda is a tiny country iliyominywa na nchi kadhaa. Hawana natural resources kabisa na wananufaika sana na machafuko ya Kongo. Siku Kongo ikitulia Rwanda inaanguka. Ila namsifu PK kwa kuwekeza kwenye watu wake (human capital) na teknolojia. Anaona mbali.

J.D. Kongo ina zaidi ya watu milioni 85. Ambapo kuna watu wazima takriban milioni 41. Hivi, tukisema waamke asubuhi wote kunywa chai kikombe kimoja tu! Hiyo ni takriban tani 123 ya chai na tani 164 za sukari! Kila sekunde 9 mtu anazaliwa J.D. Kongo. Yani tokea ni weke hii post saa 11 jioni na sasa hivi saa 3 usiku, takriban watoto 129,600 wameshazaliwa Kongo. We need this business. DR Congo Population 2019 (Demographics, Maps, Graphs)
 
Mleta mada ni matokeo ya elimu duni iliyokuzawadia cheti tu bila uwezo mkubwa wa kufikiri.

SGR kuelekea Rwanda?!usiangalie inapoishia tu,umeshindwa kufikiri huku njiani inakopita ni watu wangapi wanahitaji huduma ya reli hii?

Unajua population ya kanda ya ziwa , kanda ya kati na magharibi ni zaidi ya asilimia sabini ya population ya nchi nzima?

Najua unataka kutuonesha kuwa maamuzi haya hayakuwa sahihi ila naona ni fikra za chuki tu zimekusukuma kuandika hayo
 
Wanajukwaa,

Nimepitia takwimu kutoka the National Bureau of Statistics (NBS) na Tanzania Ports Authority (TPA) kuhusu mizigo / shehena yanayopitia bandari za Tanzania kwenda au kutoka nchi za jirani.

Kwa mwaka 2017/18, jumla ya tani 5.6 million zilipitia Tanzania (bandari ya Dar es Salaam pekee) kwenda au kutoka nchi za jirani, ikilinganishwa na tani 4.8 million mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la asilimia 17.1 na ni habari njema kabisa kwa TPA na nchi yetu kwa ujumla.

Ukiangalia mchanganuo wa shehena zinazoenda au kutoka nchi za jirani, asilima 61.1% ni za Zambia (36.6%) na J.D. Kongo (24.4%). Hii ni zaidi ya tani 3.4 million ambazo kwa asilimia kubwa zinawafikia jirani zetu kupitia barabara zetu hapa Tanzania. Ukipitia takwimu za 2017/18, TAZARA imefanikiwa kusafirisha mizigo ya tani 187,558 tu (3.4% ya 5.6 million) kwa njia ya reli.

Shehena za Rwanda ni asilimia 16.5% pekee (au tani 922,134) kwa mwaka wa 2017/18. Ukilinganisha na 2016/17, kuna upungufu wa 9.0% - kitu ambacho kinaashiria kuwa mizigo ya Rwanda inawezekana kuwa inapitia Kenya na Uganda.

Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za NBS na TPA wenyewe.

Naomba mwenye taarifa kuhusu ya haya maamuzi ya kupeleka SGR Rwanda atujulishe zaidi.

Nawasilisha.
ACCC CCCçcfccd
 
Back
Top Bottom