SGR kwenda Rwanda kuna Busara?

SGR kwenda Rwanda kuna Busara?

Wanajukwaa,

Nimepitia takwimu kutoka the National Bureau of Statistics (NBS) na Tanzania Ports Authority (TPA) kuhusu mizigo / shehena yanayopitia bandari za Tanzania kwenda au kutoka nchi za jirani.

Kwa mwaka 2017/18, jumla ya tani 5.6 million zilipitia Tanzania (bandari ya Dar es Salaam pekee) kwenda au kutoka nchi za jirani, ikilinganishwa na tani 4.8 million mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la asilimia 17.1 na ni habari njema kabisa kwa TPA na nchi yetu kwa ujumla.

Ukiangalia mchanganuo wa shehena zinazoenda au kutoka nchi za jirani, asilima 61.1% ni za Zambia (36.6%) na J.D. Kongo (24.4%). Hii ni zaidi ya tani 3.4 million ambazo kwa asilimia kubwa zinawafikia jirani zetu kupitia barabara zetu hapa Tanzania. Ukipitia takwimu za 2017/18, TAZARA imefanikiwa kusafirisha mizigo ya tani 187,558 tu (3.4% ya 5.6 million) kwa njia ya reli.

Shehena za Rwanda ni asilimia 16.5% pekee (au tani 922,134) kwa mwaka wa 2017/18. Ukilinganisha na 2016/17, kuna upungufu wa 9.0% - kitu ambacho kinaashiria kuwa mizigo ya Rwanda inawezekana kuwa inapitia Kenya na Uganda.

Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za NBS na TPA wenyewe.

Naomba mwenye taarifa kuhusu ya haya maamuzi ya kupeleka SGR Rwanda atujulishe zaidi.

Nawasilisha.
Vipi umefanya consideration ya maeneo mengine ya territory ya Tanzania ambapo reli hiyo itapita?.. maeneo hayo pia yatafaidika na Huduma hiyo zaidi kuliko huko Rwanda.. nimekuwa nikiona jinsi maeneo ya pembezoni mwa nchi yanavyobezwa Kwa uduni wa maendeleo, Sgr itachochea maendeleo ya maeneo hayo..Kwa mfano ni gharama kubwa Sana kusafiri kutoka Dar mpaka Ngara,karagwe, au muleba na Bukoba, average money spent kusafiri au kusafirisha bidhaa ni kubwa Sana..its cheaper to trade between Dar na China kuliko Dar na Kagera..SASA nadhani hacha hii miundombinu ije iwasaidie watu wa jamii hizi ku utilise bongo zao kufanya maendeleo..Rwanda can be a Terminal ya SGR Lakini katikati watanzania wengi watapata unafuu wa kusafiri/kusafirisha bidhaa zao to/from their zones.. sometimes you have to invest a lot ili uibue opportunities na kuamsha amsha the sleeping giants which is awesome for our blessed country...Tuendelee pamoja.
 
Rwanda imeipita Tanzania kimaendeleo ya propaganda.Raia wenu wakimbizi bado wapo tunawalisha Kama wakimbizi huku kwetu na hata wakitaka kurudishwa kwenu wanaanza kulia kilio Cha kusaga meno.Raia wa Rwanda kibao wamejaa kila Kona Tanzania wanatafuta maisha Sasa Kama Rwanda imeipita Tanzania wanang'ang'ania nn huku? Yaan haka Kawilaya kanaitwa Rwanda sijui kw nin tulikaachiaga maana kangeendelea kua sehem ya mkoa wetu wa Kagera tu
Kwani huko nchini Rwanda hawakai Binadamu / Watu ambao wanahitaji Huduma? Hivi Watanzania nchi ya Rwanda, Wanyarwanda na Rais wa Rwanda wamewakoseeni nini? Hivi Rwanda ndiyo imewafanya muwe Wavivu, Lege Lege, Goi Goi, Dhaifu Dhaifu na Watu mnaochelewa Kutwa kupiga hatua Madhubuti za Kimaendelo huku mkiwekeza mno katika Majungu, Chuki, Wivu na Uswahili wenu badala ya Kujikita kuangalia kwanini kwa muda mfupi tu huu Rwanda chini ya Rais Paul Kagame inawaacheni Kimaendeleo na hata Wananchi ( Raia ) wake wanazidi kuwa na ' Fikra ' pana kuliko wengi wenu ( japo wapo baadhi wenye Akili kubwa kama za Wanyarwanda ) ila ni wa kuwatafuta sana tena kwa Tochi?
 
Moron.
 
Tujenge kote iende mpaka Rusumo Au Ngara na tukirudi tuanzie morogoro mpaka tunduma tujenge bandari kavu kubwa tunduma na mpakani mwa rwanda kuwepo na sehemu mbili ya kupokea mizigo kutoka nje kuja bandarini na kutoa bandarini kwenda nje ili tule mara mbili dollar kwa export na pesa za import.
 
Vipi umefanya consideration ya maeneo mengine ya territory ya Tanzania ambapo reli hiyo itapita?.. maeneo hayo pia yatafaidika na Huduma hiyo zaidi kuliko huko Rwanda.. nimekuwa nikiona jinsi maeneo ya pembezoni mwa nchi yanavyobezwa Kwa uduni wa maendeleo, Sgr itachochea maendeleo ya maeneo hayo..Kwa mfano ni gharama kubwa Sana kusafiri kutoka Dar mpaka Ngara,karagwe, au muleba na Bukoba, average money spent kusafiri au kusafirisha bidhaa ni kubwa Sana..its cheaper to trade between Dar na China kuliko Dar na Kagera..SASA nadhani hacha hii miundombinu ije iwasaidie watu wa jamii hizi ku utilise bongo zao kufanya maendeleo..Rwanda can be a Terminal ya SGR Lakini katikati watanzania wengi watapata unafuu wa kusafiri/kusafirisha bidhaa zao to/from their zones.. sometimes you have to invest a lot ili uibue opportunities na kuamsha amsha the sleeping giants which is awesome for our blessed country...Tuendelee pamoja.
Nakubaliana na wewe 100% - ni mawazo mazuri sana. Lakini ukweli ni kwamba SGR siyo bure. Tumekopa hela nyingi sana na ni lazima tulipe madeni na riba juu. Je, si busara kwanza kuwekeza kwenye maeneo yenye kuleta profit na cash nyingi zaidi ili tumalize mkopo kwa haraka zaidi? Mfano, SGR ya Mombasa kwenda Nairobi kwa mwaka wa kwanza (2018) imeweza kuzalisha US$ 86 million (Tshs 197 billion) na hapo bado mizigo mingi sana kutoka bandari ya Mombasa yalipitia barabarani. Soma (SGR raked in Sh10bn revenue in first year). Pia, ile SGR terminal na ICD ya kupakia mizigo kwenye reli pale Mombasa imezidiwa. Hivi kama asilimia 90% tu ya mizigo kutoka bandari ya Mombasa ingepitia SGR hiyo hela isingetoshea benki kuu ya Kenya! Baada ya hapo si unaweza kutandika reli nchi nzima ukaamsha the sleeping giants?
 
Kwani huko nchini Rwanda hawakai Binadamu / Watu ambao wanahitaji Huduma? Hivi Watanzania nchi ya Rwanda, Wanyarwanda na Rais wa Rwanda wamewakoseeni nini? Hivi Rwanda ndiyo imewafanya muwe Wavivu, Lege Lege, Goi Goi, Dhaifu Dhaifu na Watu mnaochelewa Kutwa kupiga hatua Madhubuti za Kimaendelo huku mkiwekeza mno katika Majungu, Chuki, Wivu na Uswahili wenu badala ya Kujikita kuangalia kwanini kwa muda mfupi tu huu Rwanda chini ya Rais Paul Kagame inawaacheni Kimaendeleo na hata Wananchi ( Raia ) wake wanazidi kuwa na ' Fikra ' pana kuliko wengi wenu ( japo wapo baadhi wenye Akili kubwa kama za Wanyarwanda ) ila ni wa kuwatafuta sana tena kwa Tochi?

Duuh, Mkuu we wa huko nini? maana si kwa kwa maneno hayo, yaani utadhani yanaletwa na upepo wa kisulisuli
 
Meta Mada utakuwa ki desk officer kijinga kijinga cha serikali au kibaraka cha Zitto Kabwe. Wafanyabiashara wa Tanzania tunataka hiyo reli ya route ya Rwanda. Kuna fursa kibao kwa wafanyabiashara wa Tanzania kubwa mno

Ndio nini hiki umeandika?

Shame on you!
 
Inaweza ikatoboa mpaka Congo kwahiyo usiangalie udogo wa nchi kijiografia na kutolea maamuzi.
Rwanda ni “Entry Point” ya soko la DRC mashariki na Burundi. Pia na kanda ya Ziwa hasa mikoa ya Kagera na Geita.
 
Nakubaliana na wewe 100% - ni mawazo mazuri sana. Lakini ukweli ni kwamba SGR siyo bure. Tumekopa hela nyingi sana na ni lazima tulipe madeni na riba juu. Je, si busara kwanza kuwekeza kwenye maeneo yenye kuleta profit na cash nyingi zaidi ili tumalize mkopo kwa haraka zaidi? Mfano, SGR ya Mombasa kwenda Nairobi kwa mwaka wa kwanza (2018) imeweza kuzalisha US$ 86 million (Tshs 197 billion) na hapo bado mizigo mingi sana kutoka bandari ya Mombasa yalipitia barabarani. Soma (SGR raked in Sh10bn revenue in first year). Pia, ile SGR terminal na ICD ya kupakia mizigo kwenye reli pale Mombasa imezidiwa. Hivi kama asilimia 90% tu ya mizigo kutoka bandari ya Mombasa ingepitia SGR hiyo hela isingetoshea benki kuu ya Kenya! Baada ya hapo si unaweza kutandika reli nchi nzima ukaamsha the sleeping giants?
Nakuelewa..SGR sio bure pesa imekopwa nyingi tuu na almost miradi mingi iliyotapakaa nchi hii especially ya barabara ni mikopo, SASA hii network inatibu vitu vingi Sana, itapunguza uharibifu wa barabara , itapunguza gharama za usafirishaji lakini kubwa zaidi itarahisisha muingiliano wa watu wa maeneo inapopita( itachochea intertrade)..mi nadhani uwe positive na hii kitu ili as the Country tuweze Kudevelop pamoja hakuna haja maeneo mengine yasubiri Sana bila kuchangia maendeleo ya nchi..we need to pull/push together.
 
Kwa nini tusiboreshe TAZARA kufikia kiwango cha SGR? TAZARA inasafirisha tani 187,558 tu wakati ina "potential" ya mamilioni ya tani. Mwaka 2018, Zambia walizalisha copper kiasi cha tani 861,946 (2017 tani 799,329) - halafu tunajua Zambia hawana viwanda vya kuchakata copper. Copper yote inaenda China na nchi nyingine. Je, matani yote haya yalipitia wapi? Je, si kesho kutwa tu Zambia watafikia tani milion moja, moja na nusu, mbili na kuendelea? Je, hatutaki hiyo biashara ya kusafirisha tu? The 2018 copper production hits 861,946 tonnes - Zambia Chamber of Mines

Hapo sijagusa DR Congo!
Mzigo wa Zambia almost wote unapita Dar
DRC ni nchi kubwa Sana huwezi safirisha shehena yake yote kwa kupitia tunduma pekee, huko unakokupiga vita kwamba SGR isipite ndipo penye mzigo mkubwa wa DRC tunaoukosa

Ukiwa na ng'ombe wako wawili, mmoja anatoa maziwa maximum mwingine minium, ni busara utumie maarifa zaidi kwa yule anatoa kidogo kuliko kuwekeza nguvu zote kwa kile ambacho tayari ni kingi huku ukikosa kingi zaidi kwa upande wa pili.
 
Nchi yetu haijielewi yenyewe inataka shindana ma Kenya kuhusu soko la Rwanda na Uganda na kuacha Masoko makubwa ya Zambia
Huko kushindana ndio kunafanya uonekane huna akili, hivi nchi inaweza shindana na Kenya? Tanzania inapambania bandari zake zihudumie shehena kubwa, inatumia potentials zake vizuri wewe na akili yako ndogo unaona huko ni kushindana
 
La hasha. Hiyo reli itakayoenda nchi nyingine kupitia Rwanda itakuwa siyo yetu tena. Sisi tutakula hizo charges za kusafirisha shehena hadi mpakani, baada ya hapo anakula Kagame. We might as well as transport 3.4 million tonnes on SGR directly rather than share it with Rwanda by bringing the SGR their way!
Mzee kinachoangaliwa ni shehena ipite kwenye bandari zetu, hilo suala la fees kwenye railway linakuja kama preamble tu, na kwenye business yoyote huwezi kupata yote mwenyewe, business ni win win situation, Rwanda atapata lakini sisi tutapata zaidi kuanzia kwenye SGR mpaka kwenye bandari
 
Sina chochote dhidi ya nchi ya Rwanda. Naangalia data na kufanya mchanganuo. Moja, Rwanda is already in business with Uganda and Kenya. Pili, shehena za Rwanda ni tani laki 9 tu. Hatuwezi kulinganisha na laki 9 za Rwanda na tani milion 3.4 kwenda DRC na Zambia! Ni ukichaa!

Fikiria uamuzi wa kuongeza Terminal III ya Julius Nyerere International Airport. Terminal II ilikuwa imezidiwa kikomo chake cha wasafiri milioni 1.5 kwa kusafirisha zaidi ya watu million 2.4 - ilikuwa inatuumiza sana! Ni uamuzi wa busara kabisa ambao uko supported na data! Terminal III mpya ina uwezo wa kuhudumia wasafiri million 6 - kwa hiyo tutakuwa nayo kwa miaka mingi tu. It is a good investment with a solid business case.
Sasa kama ulikuwa na majibu yako kwa mini umeuliza swali?
 
Back
Top Bottom