Sethi: Tegeta Escrow namwachia Mungu

Sethi: Tegeta Escrow namwachia Mungu

Hili jamaa ni jizi na tapeli la kimataifa.. Nashangaa Magamba wamemkumbatia utafikiri Mungu wao.. Nyerere alishawahi kusema "Umasikini wa mwisho kabisa ni umaskini wa fikra..Anaweza akaja tapeli na kichupa tu na wewe una almasi/diamond,, akakwambia hiyo ya kwako sio almasi, almasi ni hii.. Ulivyomjinga unakabidhi dhahabu kwake yeye anakupa kichupa unatoka pale unashangalia kama zuzu!!" Huu mfano wa Nyerere ni typical kabisa na MaCCM ya leo kuanzia mwenyekiti wao mpaka wasakatonge wake..

Soma hapa kama unabisha singasinga sio tapale
[TABLE="width: 623"]
[TR]
[TD="width: 375, align: left"]
Hello
[/TD]
[TD="align: left"]book peter | home[/TD]
[TD="width: 38"]
za.png
[/TD]
[TD="width: 49"]Login[/TD]
[TD="width: 38"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[h=1]
complaint.png
Harbinder Singh Sethi Complaint[/h]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="class: blue-shade, width: 25%, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]
cp-wbg.png
SUPPLIER[/TD]
[TD="class: border, width: 27%, align: left"][h=2]Harbinder Singh Sethi[/h][/TD]
[TD="class: blue-shade, width: 24%, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]INDUSTRY[/TD]
[TD="class: border, width: 24%, align: left"]Consultant[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]BRANCH / AREA[/TD]
[TD="class: border, align: left"]Sandton, Johannesburg[/TD]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]COUNTRY[/TD]
[TD="class: border, align: left"]South Africa[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]TIME / DATE[/TD]
[TD="class: border, align: left"]07:00 Wed 15 Jan[/TD]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]PERSON RESPONSIBLE[/TD]
[TD="class: border, align: left"]Harbinder Sethi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]CUSTOMER[/TD]
[TD="class: border, align: left"]brian51[/TD]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]View all reports by user[/TD]
[TD="class: border, align: left"]
compliment.png
0
complaint.png
1
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]PROBLEM[/TD]
[TD="class: border, align: left"][h=3]Breach of Contract[/h][/TD]
[TD="class: yellow-shade2 yellow-border, bgcolor: #FDFEED, colspan: 2"][TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD]
email.png
email report
social-box-twt.png
post report
facebook-icon.png
facebook-comment.png

0[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
feedback.png
view customer feedback rating & analysis[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]INCIDENT[/TD]
[TD="class: border, align: left"]Wed 15 Jan[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: blue-shade, bgcolor: #EDF5FC, align: right"]HEADLINE[/TD]
[TD="class: border, colspan: 3, align: left"][h=2]********** Transactions and Businesses[/h][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: purple-shade border justify, bgcolor: #FEF7FF, colspan: 4"]This note is to inform all the citizens to be very careful with this gentlemen by the name Harbinder Singh Sethi/Mr. Sethi. He comes across to anyone as a big businessman and a person with big contacts in Africa but the fact is he is no more having that huge business and contacts which he flaunts. You would be wasting your time running behind him. I have been told that he has LIQUIDATED his companies and all his assets have been taken over by the leading banks of South Africa. There are many cases registered against him and everyone should do a Google search on this man before dealing with him.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Wezi na wanasiasa ni wazuri sana katika kumtaja Mungu, huyu siyo wa kwanza kusema hivi hata Idd Simba, Omary Nundu, Msabaha na wale jamaa wa City Water walipoondolewa ilikuwa hivi hivi
 
Serikali imewekwa MFUKONI na Harbinder Sing Sethi.
Hawamfanyi lolote na wakicheza anawashitaki
 
Mungu hashughuliki na ufisadi, Mungu ni mtakatifu mno hawezi shiriki ufisadi na seth. Labda aseme anawaachia miungu wake wachafu.

Mungu wa Seth (ng'ombe) kwetu ni kitoweo kizuri sn, akimuachia huyo mungu wake sisi tunamtafuna.
 
Faizafoxy njoo umtetee fisadi huyu. Maana wewe pekeako ndio ulie aki na nguvu za kuutetea ufisadi wakati walioiba wenyewe wanasema wanamwachia mungu. Je na huyo mungu anaye mwongelea ni mungu wako pia?
 
Kumbe Sethi ni Mtanzania??? Nilikuwa sijui hili....


Ofcourse Mtanzania, haujaona Mamilioni yaliyoenda kwa watendaji wa RITA? CEO Saiboko na mtendaji wake? Kuwa Mtanzania sio lazima uzaliwe Bongo, sometime kuna shortcut, gharama ni wewe tu kupanda dau.

Si tumekubali kugawa bei kwa kila kitu, sasa shida iko wapi?

SMH
 
Pengine Sethi hana makosa. Hii kesi haitajulikana ukweli wake mpaka JK atakapoachia ngazi na kukamatwa.
 
Huyu ni Mwizi tu na Mungu hawezi kukubali maombi yake ya kuendelea kuihujumu Tanzania na Watanzania... Due Diligence ya Advocate Ngwilimi iliweka wazi kuwa PAP ni Utapeli lakini Muhongo aling'ang'ania....
 
unasitahili hicho ulichopewa sbb watu waliokufa sbb za ya ww kutokulipa kodi ni wengi madawa yalikosa Mungu ameishaanza kukupatia majibu
 
Huwa hamsomi post tunazoweka humu, tuliandika zamani humu kuwa Habinder Singh Sethi ni Mtanzania tena kwao ni Iringa.
Ah Mtanzania? fuatilia goldenberg scandal ya kenya. Kenya Ilifilisiwaje na KANU kufa? Mhusika ni nani tafuta habari usikurupuke!!
 
The breathtaking extent of corruption perpetrated by the family of the former Kenyan leader Daniel Arap Moi is revealed in a secret report which lays bare a web of shell companies, secret trusts and front men used to steal over two billion dollars’ worth of state money. The suppressed U.K auditor's report details how Kenyan state finances were laundered across the world to buy properties and companies in London, New York and South Africa and even a 10,000 hectare ranch in Australia. Ex-President Moi allegedly has two properties in London held under a trust set up by Mukesh Gohil; and in South Africa Moi owns a number of properties in South Africa. His front man in South Africa is Harbinder Singh Sethi, has 74 properties listed under closed corporations all of which are registered in his name.

Source 1: https://wikileaks.org/wiki/The_looting_of_Kenya_under_President_Moi
Reference 1: How Kenyan Tycoon Sealed IPTL Deal In Dar
Reference 2: RI Consulting Services: Harbinder Singh Sethi - Chairman

Endelea kumuachia Mungu wako aliyekutuma kuwa tapeli,Hata huyu mwandishi wa nipashe hajui kuhoji,kinachomtia matatani sio pesa iliyoingia ambayo ni ikulu walimpatia.Tatizo lake aliponunua IPTL alitumia nyaraka feki na tra wamefuta baadhi,Hapo ndipo kosa la kutaifisha mtambo huo.Uliona wapi 7 unit kuuzwa kwa tsh.6,000/- wakati 3unit imeuzwa kwa mabilioni!!!???
 
Pengine Sethi hana makosa. Hii kesi haitajulikana ukweli wake mpaka JK atakapoachia ngazi na kukamatwa.

Hata kama utawatoa kafara Musoma stars lakini ni wewe JK ambaye damu yao itakuwa juu yako,Mbena katangulia salama nawe Rais wangu jipime ili ulinde heshima ya nchi hii,inafikia mpaka unanyimwa msaada ndio unaruhusu hatua zichukuliwe,aibu kubwa kwa JK
 
Huyu mwandishi nae, mbona hajaitaja MKOMBOZI au sbb ni benki ya parokia yake!
 
Huwa hamsomi post tunazoweka humu, tuliandika zamani humu kuwa Habinder Singh Sethi ni Mtanzania tena kwao ni Iringa.

Tena mwanachama hai na mfadhili mkuu wa chama cha map..........FaizaaaaHHH!!!!!!!!!??????
 
IPTL--December3--2014.jpg

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi

Sitakubali kutaifishwa mitambo ya IPTL
Akana kuangamiza Kanu Kenya

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi
Wakati masikio ya Watanzania yakiwa yameelekezwa Ikulu kusikia maamuzi ya Rais Jakaya Kikwete juu ya maazimio manane yaliyotolewa na Bunge kuhusu sakata la uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi, ameibuka na kudai kuwa anamuachia Mungu yote yaliyotokea.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwa simu katika mahojiano maalum na NIPASHE kuhusu mambo yaliyojitokeza katika mkutano wa16 na 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati wabunge walipokuwa wakijadili kashafa ya uchotaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Sethi alisema maamuzi yaliyofikiwa na Bunge kimsingi ni ya kumuonea kwa sababu alifuata taratibu na sheria za nchi wakati wa kutoa fedha hizo, hivyo anamuachia Mwenyezi Mungu ndiye ataamua hatma ya suala hilo.

Sethi ambaye hakutaka kueleza alipo kwa sasa, alisema uamuzi wa Bunge haujamtendea haki kwa sababu kwanza hakupewa nafasi na chombo chochote kutoa maelezo yake na badala yake yamefikiwa maamuzi mazito kama hayo.

Mahojiano kati ya mwandishi wa habari hii na Sethi yalikuwa kama hivi:

Mwandishi: Umesikia maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusu suala la akaunti ya Escrow, je, unasemaje?

Sethi: Suala hili lipo mahakamani naomba msamaha siwezi nikajibu chochote, lakini kimsingi wabunge wamenionea tu, hizo fedha nimechukua kihalali kwa kufuata sheria za nchi sijaenda kumwibia mtu yeyote. Kunionea hivyo ni kitu kibaya sana, mimi namuachia Mungu tu.

Mwandishi: Kama unaona umeonewa na Bunge, je, unakusudia kuchukua hatua zozote za kisheria?

Sethi: Kwa sasa siwezi kuchukua hatua zozote kwa sababu suala hili kwanza bado lipo mahakamani, tunasubiri uamuzi wa mahakama. Mimi naheshimu mahakama ya kila nchi na Tanzania zaidi kwa sababu hii ni nchi yangu.

Mwandishi: Kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Bunge, je, utakuwa tayari kufuta kesi mahakamani inayoendelea kuhusiana na suala hili.

Sethi: Hapana, hatufuti kesi yeyote, tutaendelea mahakamani ili haki iweze kupatikana.

Mwandishi: Zipo taarifa kuwa rekodi yako ni mbaya na ulisababisha hadi serikali ya chama cha KANU nchini Kenya ikaangushwa kwenye uchaguzi.

Sethi: Mimi siyo mtu wa siasa, mimi ni mfanyakazi na ni mfanyabiashara wa kuzalisha umeme siyo siasa, siwezi kuangusha serikali wala chama cha mtu yeyote. Mimi siyo mtu wa siasa kazi yangu ni kuzalisha umeme na Tanzania nimefanya kazi kubwa hiyo kabla ya uwekezaji wangu umeme ulikuwa unazalishwa megawati 10 leo hii zinazalishwa megawati 100.

Pia umeme uliokuwa unazalishwa uliuzwa kwa senti 36 mimi nauza kwa senti 25, wengine wanazalisha kwa senti 50 na wakitaka kufunga kiwanda (mitambo) sawa ili waendelee na umeme wa bei ya juu, Mungu mkubwa tunamuachia yeye ndiye ataamua.

Mwandishi: Moja ya maamuzi ya Bunge ni kwamba watataifisha mitambo. Je, unasemaje?

Sethi: Hilo haliwezekani kabisa na kufanya hivyo tutakuwa tunaipeleka nchi kubaya sana na hakuna atakayeingia Tanzania tena. kwanza sikupewa nafasi hata ya kujieleza.
Miongoni mwa tuhuma alizozitoa Kafulila bungeni ni madai kwamba Seth alichangia kukizamisha chama kilichokuwa tawala nchini Kenya cha Kanu kutokana na kashfa maarufu ya ufisadi nchini humo ya Goldenberg.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wabunge walitoa maazimio manane kuhusu sakata la Escrow likiwamo la kutenguliwa kwa nyadhifa za Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema.

Wengine waliopendekezwa kuvuliwa yadhifa zao ni wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge hilo, William Ngeleja (Sheria, Katiba na Utawala), Andrew Chenge (Bajeti) na Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini).

Pia wamo Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), viongozi wa umma na maofisa wa ngazi za juu serikalini waliohusishwa na vitendo vya kijinai katika sakata hilo linalohusisha kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL).

Kadhalika, Takukuru, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, kutakiwa kufanya uchunguzi dhidi ya wote waliotajwa kuhusika na sakata hilo na watakaobainika kuhusika kwenye vitendo vya jinai hatua za sheria zichukuliwe dhidi yao.

Maazimio mengine ni kumtaka Rais kuunda tume ya uchunguzi ya kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya majaji kuhusishwa kwenye kashfa hiyo.

Majaji waliotakiwa kuchunguzwa ni Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Prof. Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Aidha, Bunge lilitaka mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi kuitaja Stanbic Bank Tanzania Ltd na benki nyingine yoyote itakayogundulika baada ya uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika akaunti ya Escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu.

Pia, serikali iandae na kuwasilisha muswada wa marekebisho ya sheria iliyounda Takukuru kwa lengo la kuanzisha taasisi mahsusi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo.

Serikali imetakiwa kutekeleza azimio la Bunge la kupitia mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya Tanesco na kampuni binafsi za kufua umeme na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapitio ya mikataba hiyo kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti.

CHANZO: NIPASHE
MUNGU yupi apendaye wezi?
 
Back
Top Bottom