Serious: Nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serious: Nifanyeje?

Discussion in 'JF Doctor' started by Invisible, Feb 26, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  I see, ni mara ya kwanza naleta tatizo langu kwenu wakuu.

  Nina matatizo ambayo nahitaji ushauri wa haraka au wa kina ikiwezekana,.

  Najisikia uchovu wa hali ya juu... Najisikia kucha kila aina ya kazi... Natamani kupumzika japo siku tatu tu niweze kurejea katika hali yangu ya kawaida.

  Ugumu:

  Nahitaji kuzima simu, kuwa mbali na pc kuwa mbali na familia yangu kabisa na kukaa alone kwa muda huo.

  Si rahisi kuwambia familia kuwa nawaacha kwa muda huo, nahisi watajisikia vibaya.

  Si rahisi kukaa mbali na JF, nikifanya hivyo nafsi inakuwa inanisuta all the times.

  Si rahisi kuwaacha kwenye mataa makampuni manne ambao wameniajiri na kazi zao kulala siku moja kwao wanaona kama ndo mwisho wa makampuni yao (ilhali kuna wataalam wengi lakini wananikomalia).

  Sina hamu na pesa zao hata kama wanasema wanavunja mkataba nami kwani mwili hauwezi kuvumilia hali niliyo nayo kwa sasa... Yani niko tayari kuacha na kupumzika liwalo na liwe.

  Mbaya zaidi:

  Nikiwa naendesha gari natamani kutokanyaga hata mafuta wala breki kwani nahisi vinanichosha mwili tu, nikiwa mbele kwenye foleni ya magari najikuta nimekuwa mwingi wa mawazo hata taa zikiruhusu nisipopigiwa kelele na wenzangu kushtukia inakuwa tatizo.

  Je, wakuu nifanye nini???
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu Invisible. Kwanza nakupa pole sana kwa hali hili. Inaonekana kabisa you are too much overloaded!!! You need to offload!!! Kabla sijasema mengi, nakuomba sana kabla ya kwenda kupumzika kmwone kwanza Physician wako na akufanyie vipimo fore most blood sugar level and presha ndipo aendelee na diagnosisi nyingine as per his/her suggestion. For sure atakushauri upumzike, upate usingizi wa kutosha bila bughuda. Ila katika kutekeleza hilo ni vema familia yako wafahamu hali yako na utapumzika wapi. Kuwa away from mawasiliano is ok but not with family members contact.

  Also nikuulize ratiba yako ya kula ikoje??? Usikute unatumia nguvu nyingi sana na replacement ni ndogo. Nashauri nenda kwa Physician sasa usisubiri majibu hapa kwa sasa hivi. Please, we need you most here at our sacred Jamvi.
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Pole sana Invisible!
  Kama binadamu unahitaji muda kupumzika baada ya shughuli zako za kila siku. Naamini mwili wako unachoka sana kwanza unafanya kazi nne bado hujaingia JF tena siyo kama member tu wa kawaida ila una majukumu makubwa na hii forum nionavyo.
  Jitahidi upate muda wa kupumzika,unaweza ukachukua holiday kwa muda kutoka kazini.
  Kitaalamu sijui ni tatizo gani ila naamini unafanya sana kazi either mentally or physically hivyo tafuta muda upumzike.
  Unaweza hata kuanguka siku nyingine! Na hizo kazi nne hata kama ni masaa 3 kila moja kwa siku ila ni stressful kutokana na demand zake tofauti hata kama profession ni moja. Majukumu yamezidi na hupati muda wa kupumzisha mwili wako!
  Pia zingatia ratiba nzuri ya chakula.
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pole mkuu kwa haya.
  Haya ni matatizo yawapatayo watu wafanyao kazi sana bila kupumzika.
  Nafikiri unahitaji ku-recharge battery yako. Wenzetu huwa wanakuwa na somesort of holiday na huwa wanaenda kupumzika kweli. Sisi kwa sababu ya ukwasi wetu tunakomalia kazi tunasahau hata haki za msingi za familia yetu. Mkuu kapumzike, iage na familia yako, waeleze tu mazila yanayokupata,,,, naamini watakuelewa tu.
  take some days off na utaona utendaji wako utakuwa mara dufu kuliko sasa.
  All the best.
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Very simple nenda muhimbili au hospitali yenye hadhi, cheki jamaa waombe wakulaze hapo kwa siku tatu, then kila kitu fresh! We used to call this medical rescue!!
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Nina Daktari wawili na wote walishaniambia PUMZIKA, ikabidi niwambie ukweli kuhusiana na majukumu niliyo nayo na uiumu wa kila jukumu. Wakanishauri (karibia kwa mawazo sawa) kuwa niwaambie waajiri wangu wanipe likizo... Ni mmoja alokubali kunipa likizo ya wiki mbili lakini wengine walilalamika sana huku wakitaja ongezeko la dau katika kazi zao kitu ambacho binafsi kwangu hakikuwa mtego tena! Ni mwezi Septemba mwaka jana hiyo.

  Nilipimwa na kukutwa nilikuwa sina ugonjwa HATA MMOJA (kipindi hicho niliwahi kuandika hapa juu ya maumivu ya kichwa kwa wenye kumbukumbu). Kupumzika wiki moja kwa kampuni moja kulisaidia kidogo kwani tangu kipindi hicho sijapata matatizo ya kichwa kabisa.

  Dah, huwa nakula mara moja kwa siku... Mchana sili kabisa zaidi ya kupata kikombe cha kahawa.

  Inawezekana basi, huwa naogopa sana vyakula ambavyo havijapikwa na mpishi ninayemfahamu kwa karibu. Am not ready to risk... Hata hotelini nachagua sana na huwa nahakikisha sifahamiki hotelini hapo na nakula chakula kilicho tayari vinginevyo nanunua soda tu na kulala mbele.

  Nashukuru mkuu, lakini hao ndo wamenambia jaribu kufikiria cha kufanya kwani wamenishauri niwe mbali na pc, nizime simu kwa muda na ikiwezekana niwe mbali na familia kwa muda kidogo niweze kurudi kwenye form.

  Na hivi ndivyo ninavyoambiwa na waajiri wangu... Nilitarajia unambie "Pumzika na iache JF kwa muda tukutane baada ya mwezi hivi"

  Hahaha, huu ndo ugumu ninaokumbana nao mkuu Maane.

  Am trying to be frank!
   
 7. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  This must be BIG JOKE. Aombe alazwe? Mwombe radhi Inv.
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pole sana mkuu. Ni ngumu kuamua jinsi ya kuweka kando vitu ambavyo umeviozea sana na hasa pale ambapo wewe ni mtu wa kukabili majumu yako na si kuyakimbia kama baadhi yetu. Hata hivyo mwili hauna mawasiliano na kazi zako. Ukichoka umechoka tu hata kama ungetamani kuendelea na mapambano. Hebu kaa chini ufikirie hao wote wanaokuhitaji na familia wangefanyaje kama leo Mungu angeamua kukupumzisha kwake. Ukishapata jibu, ambalo ni lazima litakushawishi kuwa lazima maisha yataendelea tu hata wakipata taabu, basi utakubaliana na hali hii ili ukapumzike nao wapate taabu kidogo. Jambo la faraja ni kwamba Mwenyezi Mungu bado anakupenda na baada ya siku kidogo utarudi ukiwa mwenye furaha na amani! Unahitaji neema ya Mungu kufanya maamuzi. Sina wasi wasi utaamua kupumzika soon. I will miss you though!!
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Oh,

  Asante mkuu BelindaJacob,

  Nalilia kupumzika... Nahisi ndo suluhisho. Tatizo ni vipi nifanye? Baadae nahisi tatizo jingine labda ni la kisaikolojia na wala si uchovu.

  Laba niseme zaidi:

  Nina watoto 8 mpaka sasa (Nyumbani Tanzania) ambao hawana wazazi (yatima) na wengine wana wazazi lakini uwezo uko chini ninaowasomesha na sidhani kama inawezekana kupita dakika bila kuwawazia, hawa sidhani kama unaweza kunishauri kuwa niwabwage! Sintokusikiliza...

  Hii hali inanitatiza SANA mpaka nafikia hatua ya kusema mbele zenu wakuu, kama kuna ambaye anaweza kunishauri kama kuna cha kunywa ama kula kunifanya nirejee kwenye form basi naomba sana anipe ushauri...

  Hizo kampuni ninazozifanyia kazi ni kuwa nafanya kazi ya aina moja kwa wote isipokuwa kampuni tatu zimeridhia kuniacha nibaki kwa mwajiri wa mwanzo zenyewe zinatuma kazi zake kwa njia tofauti na wakti mwingine kuleta ofisini kwangu physically.
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Hapana Mkuu Invisible. Ukirudi hapo nyuma kwenye post yangu nilimaanisha pumzika ili upate nguvu maana tunakuhitaji hapa jamvini. Si kwamba uwepo, ndo maana nimekuambia ondoka hapa sasa hivi usisibiri ushauri wa hapa maana muda unazidi kusonga mbele. Nakuombea afya njema. Aga hapa for a while, tuta kumiss but we need you healthly!!!

  Halafu kufanyia kazi 4 companies na bado JF is hectic!!! Yaani mkuu wangu ni kuwa fedha haitoshi mpaka uamue kufanyia hizo consultancy makampuni hayo yote??? Chagua hapo mawili then uyaambie yakuongeze mshahara/fees as compensation for the other 2 forgone. Please do that Mkuu wangu.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Wakti naanza kazi na haya makampuni nilikuwa na target ya kujifunza kufanya kazi nyingi at a time. Sijutii uamuzi huu ila nahisi naelemewa kwa wakti huu.

  Nikiwambia waongeze fees huwa si tatizo, wanachotaka niwape invoice haraka. Ndo maana nikasema kwa sasa hata hela sina hamu nayo tena, nimechoka mkuu.

  Nashukuru kwa ufafanuzi wa awali, nimekusoma sana.

  Tatizo ni hivi:

  Nikiomba likizo kwa wengine wote, tutalazimika kuifunga JF kwa siku mbili ili kufanya maintenance KUBWA SANA kisha hata nikiwa kando basi kila kitu kiwe kheri kabisa na nikirejea iwe ni kuangalia posts ambazo ziliwekwa wakti sipo online.

  Itabidi mkiombwa JF kuwa down for maintenance mtukubalie tu
   
 12. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Pole mkuu!

  Intervention ingine je wewe ni mtu wa kusali?

  Tumia mda spritually kumwomba Mola pia uende zaidi church\msikitini

  Hii is so powerful na pia waweza kuonana na mchungaji\padre akakushauri!
   
 13. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu, Ukubwa jalala.
  goodday.
   
 14. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Mkuu Invo,
  Pole sana kwa......naamini itakuwa fatique kama wanavyosema wazungu, you need a good brake but kutokana na uliyosema inabidi umake sure kwanza kila kitu kiko mahali pake kabla hujatoweka na kwenda kujichimbia mahali.
  Waajiri itakuwa rahisi kuwatelekeza kwa siku kadhaa kwa excuse ya 'ugonjwa', tafuta mtu ambaye atakusaidia kwa issue ya watoto for few days.
  Cha muhimu sana acha simu yako nyumbani na tafuta katoto kadogodogo kazuriiiiii kaka na wala usiogope kuingia gharama za kwenda nako mahali kama ngurudoto, kakuchuechue misuli na kukunyoosha viungo. Kama unaye wife am sure atakuamini ukisema una safari muhimu ya kikazi.
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Invisible!
  Nimekuelewa vizuri sana, huwezi kuwabwaga hao watoto maana umedhamiria kwa jinsi ya uwezo wako kuwaendeleza kielimu wawe na msingi bora wa maisha. Pia unapata Baraka.

  Inavyoonyesha pia umejaribu kulitatua hili suala kwa namna mbalimbali ila zimeshindikana hata hili ya holiday naona hautaliweza japo ni muhimu kidogo. Maana huwezi chukua likizo au ukichukua bado unafanya kazi kama vile upo kazini.

  Kuhusu kitu cha kunywa ili urudi katika hali yako hapo sifahamu ila itahitaji mtaalamu kiafya akushauri zaidi mana kila mtu anakuwa na experience yake atumiapo kitu fulani.

  Pole kwa hilo tatizo!
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu sijui ni Invisible gani huyu anaongea, 'the real one', 'fake one', au yule mpolempole hivi....au computer imetekwa na 'real robot' tena?

  Nauliza hivi kwa maana kwamba, kuna mmoja wa ma-Invisible wa JF alishawahi kuleta tatizo kwenye hili jukwaa HAPA, tulijaribu kumpatia ushauri wa aina mbalimbali, ila sina uhakika kama alipata nafuu katika tatizo hilo, hivyo kama atakuwa huyo huyo basi hii si mara yake ya kwanza kama alivyoashiria hapo juu.

  Invisible - robot akipata matatizo itakuwa noma sana, maana mambo ya JF bila automation yake afanyayo yanaweza kuwa magumu kwa Invisibles wenzake. Iposiku itabidi tuvumilie tu atoweke ili aweze kubadilisha microchips zake, naona zinaanza kuwa kuu-kuu, upgrade inahitajika.

  Inaniogopesha sana pale anaposema kuwa hata wakati anaendesha gari, kuna nyakati anakuwa anazingirwa na kukata tamaa - anakuwa "mwingi wa mawazo." Hapa mimi inaniogopesha. Mawazo gani hayo na yanasababishwa na nini? Je, Invisible huyu anahitaji ushauri wa kisaikolojia ukiambatana na physical remedy ya aina fulani hivi?! Ngoja nitathmini cha kufanya kuweza kumsaidia mwenzetu, maana inawezekana kabisa hata hivi tunavyofanya hivi sasa ni moja tu ya mambo yanayomwongezea mawazo mengi... yaani kusoma na kusoma ushauri mbalimbali badala ya kuwa amepumzika. Tegemea mawasiliano yangu Invisible (yeyote)!

  SteveD.
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Dah! Pole sana Robot! That should be Body Fatigue Mkuu, Nakushauri Fanya Mazoezi japo ya kukimbia ili Mzunguko wa Damu na Oxygen katika mwili view safi vile vile Jaribu Water Therapy Mkuu kila siku asubuhi kabla hujapiga mswaki gida maji kama glass nne kaka infact this is my way of Life na huwa najisikia fresh almost siku Nzima. Na Muda wa kupumzika nao ni muhimu sana
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kumbe ni Invisible Fake!

  Vitu fake siku hizi vipo vingi!
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Yes my boy........asikuambie mtu sijui unywe asprini sijui umuone dokta mashoka hamna tiba hapo......

  tatizo lako si lako tu mie limenipata mara kadhaa ilifikia kipindi nakata tamaa ya maisha kwa kusongwa na mawazo yanayosababishwa na kuwa busy saana....ubusy wa kazi zinazotumia kichwa sana kufikiri saana.......
  ..............na watu wanajiua sana hasa japan na south korea kwa tatizo lako.....ni tatizo kubwa sana unahitaji tiba......

  .............nahisi kazi unayofanya either ur a programmer au DBA something like dat field hizo ni kazi zo borind sana zinaleta stress sana kwa ufanyaji wake wa kazi wa muda mrefu.....
  ........bora wewe unazima kwenye trafiki laits mie niliwahi kupikia chakula lotion nikijua ni mafuta.....nimekuja kugundua nakula......

  .......TIBA kama alivyosema KKS......kama ni tafuta "kibiyonce" wako jivinjari nae pembeni kidogo ya mji kwa siku 2 tu.....mind u usiache pc...pc is life.....
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Give it a break man. Your body is a machine, which when in need of a break, it tells you so and yours has just done that. It is upon you to decide, to meet your body, your mind or the world needs
   
Loading...