Habari wana MMU,
Ni mda mrefu sijaja jamvini kuongea nanyi ila leo imenilazimu kwasababu nina tatizo linalonisumbua sana. Mwaka juzi nilianzisha mahusiano na dada mmoja hapa Dar na baada ya muda alinieleza ukweli baada ya kunificha kwa muda kuwa yeye ni mke wa mwanajeshi na ana watoto wawili na mme wake huwa hamridhishi na ndiyo sababu ameamua kuwa na mimi kwa sababu namridhisha na hajawahi enjoy mapenzi kwa kiasi hicho tangia azaliwe.
Mapenzi yetu ya wizi yalikolea na kutokana na mme wake kwenda Sudan kikazi basi tulijiachia sana mpaka kufikia hatua binti akatoroka kwake akahamia kwangu ila bwana yake aliporudi ikabidi arudi kwake na watoto aliwapeleka Mwanza ukweni. Kinachonisumbua ni kuwa tangia mwezi wa kumi na mbili binti amenitegesha ujauzito na alishabeba mimba mara mbili ila kila mme wake akijua anamlazimisha kutoa na kumwambia kuwa hayukotayari kulea.
Nilipoona haya yamejiri nilimwambia binti tuvunje mahusiano nikabadilisha na namba za simu. Alipoona hayo alichukua vitu vyake na kuhamia kwangu nikiwa kazini nikamkuta nje, leo ni siku ya nane yupo kwangu.
Jamani mie nakufa, naomba mnishauri wadau nifanyenini