Serikalil: Hakuna mgonjwa wa Ebola nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
Serikali ya Tanzania imesema kuwa hakuna mgonjwa wa Ebola aliyeripotiwa nchini huku ikiwashauri wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Jana Uganda ilitangaza mlipuko huo baada ya watu sita kufariki huku mgonjwa mmoja vipimo vya maabara kuthibitisha kuwa anaugua ugonjwa huo katika Wilaya ya Mubende iliyopo katikati ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Septemba 21, 2022 na Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel imesema kuwa “Wizara inapenda kuwajulisha kwamba hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini,

Aidha ninawashauri wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi na sabuni, kuepuka kugusa mwili au majimaji ya mwili wa mhisiwa au mgonjwa wa Ebola, na kuepuka safari zisizo za lazima kutembelea maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huu” imesema taarifa hiyo.

Amewaagiza waganga waganga wakuu wa mikoa na halmashauri nchini kuimarisha utoaji wa elimu, ufuatiliaji wa ugonjwa, uchunguzi wa kitaalam na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba.

“Nimewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kuimarisha utoaji wa elimu, ufuatiliaji wa ugonjwa, uchunguzi wa kitaalam na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba na kinga muhimu katika maeneo yao. Vilevile, nimewaelekeza kuimarisha uchunguzi wa wageni wanaoingia nchini kupitia mipaka yetu ikiwemo matumizi ya vipima joto (thermal scanners)”.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom