Serikali zuia mauaji haya yasitokee. Mnyeti hili ni lako!

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Wanajamvi, wazee wetu walituasa kwamba kinga ni bora kuliko tiba!

Kambi ya wavuvi Migongo Kijiji cha Kisaba kata ya Maisome Sengerema mkoani Mwanza hali ya usalama si shwari na damu inaweza kumwagika muda wowote toka Sasa.

Kambi hii inaweza kuongoza mkoani Mwanza kwa uvuvi haramu kwa kutumia nyavu za nailoni maarufu kama"timber" chini ya Uenyekiti wa Masau Maregesi Bwire anayedaiwa kushirikiana na baadhi ya watendaji Serikalini.

Bwire ambaye amedumu katika nafasi hiyo kwa miaka 24 akiwa pia ni mmiliki wa nyavu haramu ameamua kuwatimua vijana wavuvi zaidi ya 62 walioamua kupinga uvuvi haramu baada ya kupata elimu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwamba sasa wavue samaki aina ya sato wanaoruhusiwa kuvuliwa.

Taarifa kutoka Kambi hii ya wavuvi zinadai kwamba Bwire anawahesabu vijana hawa wazalendo kama wasaliti kwa maelekezo "kutoka juu". Vijana hawa wameamua kununua nyavu sahihi ya kuvulia zaidi ya 600 ambayo Bwire na Kambi yake imepania kuzikamata wikiendi hii na kuzipiga kiberiti.

Baada ya malalamiko yao kupuuzwa na Serikali zaidi ya miezi mitatu vijana hawa wameamua kunoa mapanga, visu, nondo, petroli, mikuki tayari kupambana na atakayegusa nyavu zao halali na kuacha haramu za Bwire na maswaiba wake! Vijana hawa wameapa kufa au kupona kupambania nyavu zao.

Aidha, vijana hawa wanamuona Naibu Waziri Mpya mwenye dhamana Alexander Mnyeti kama mtu pekee anayeweza kunusuru damu isimwagike baada ya kukosa MSAADA kwa ngazi zote za Serikali kata, wilaya na Mkoa.

My take: Alexander Mnyeti hili ni zigo lako litatue uokoe jahazi.
 
Eeh Mungu tuepushe na uovu ktk Taifa letu la Tanganyika
 
Kama kweli wamefika hatua hiyo, basi uongozi wa wilaya na mkoa uwajibishwe kabla damu haijamwagika
 
Back
Top Bottom