Serikali yetu sijui inachelewa wapi kuongeza kodi ya magari yanayovuka mipaka kwenda Kenya

Mbolabilika

JF-Expert Member
Jul 30, 2019
2,125
2,859
Najiuliza maswali mengi kwani serikali ya TANZANIA haitozi Kodi kwa magari ya mizigo yanayoenda Kenya? Au kama wanatoza kwanini wasijaribu kuangalia upya hizo tozo ili waongeze kodi ya 25% kwa magari ya mizigo yanayoenda Kenya ambayo ni nafaka, matunda na viungo na kuongeza japo 10% kwa yanayoingia? Kwasababu lazima serikali ifaidike na mazao yanayouzwa nje. Au munaonaje wazalendo wenzangu?
 
natakiwa uelewe kuwa mazao uanapouzwa nje ni faida kwa mkulima amabye kimsingi serikali haimsaidii kwa chochote.
 
Inatakiwa uelewe kuwa mazao uanapouzwa nje ni faida kwa mkulima amabye kimsingi serikali haimsaidii kwa chochote.
Kwakua Kenya jeuri na wananjaa watanunua tu ila Kwa pesa mingi lengo kuwapandishia bei mahitaji muhimu ili akili iwakae sawa
 
Wao c wanakopi Sera za Trmp za uhasama basi inabidi hawa kuwapeleka hivyo hivyo kitrump trump
 
Kwakua Kenya jeuri na wananjaa watanunua tu ila Kwa pesa mingi lengo kuwapandishia bei mahitaji muhimu ili akili iwakae sawa

We ongea ujinga tu,Kenya tulizingua kuwauzia mahindi alichokifanya Kenyatta kaagiza mahindi kutoka Mexico ni miezi 3 sasa yanashusha mahindi tu huko bandarini.

Njoo uwaangalie wakulima wetu waliokua wanategemea kuuza mahindi Kenya uone wana hali gani sasa hivi.
 
Umejaribu kufikiri kuwa kwa kufanya hivyo athari zake zaweza kuwa zipi labda?
Athari zake mfumuko wa bei tu upande wa pili sababu haina jinsi lazima watahitaji tu na hawawezi kuchukua kwengine gharama zitakua kubwa zaidi na hakuna uhakika wa kupata hivyo vitu Kwa wakati
 
We ongea ujinga tu,Kenya tulizingua kuwauzia mahindi alichokifanya Kenyatta kaagiza mahindi kutoka Mexico ni miezi 3 sasawanashusha yanashusha mahindi tu huko bandarini.

Njoo uwaangalie wakulima wetu waliokua wanategemea kuuza mahindi Kenya uone wana hali gani sasa hivi.
Mahindi bei inagoma kupanda,sababu hayana out let
 
Athari zake mfumuko wa bei tu upande wa pili sababu haina jinsi lazima watahitaji tu na hawawezi kuchukua kwengine gharama zitakua kubwa zaidi na hakuna uhakika wa kupata hivyo vitu Kwa wakati

Ni zaidi ya unavyowaza !

Kodi haipaswi kutozwa kwa kumkomoa mlaji wa mwisho au vyovyote vile!

Utozwaji wa kodi unakanuni zake!

Tafuta kujua!
 
Najiuliza maswali mengi kwani serikali ya TANZANIA haitozi Kodi kwa magari ya mizigo yanayoenda Kenya? Au kama wanatoza kwanini wasijaribu kuangalia upya hizo tozo ili waongeze kodi ya 25% kwa magari ya mizigo yanayoenda Kenya ambayo ni nafaka, matunda na viungo na kuongeza japo 10% kwa yanayoingia? Kwasababu lazima serikali ifaidike na mazao yanayouzwa nje. Au munaonaje wazalendo wenzangu?
Kuna mkataba wa comesa
 
Pandisheni kodi mtakavyo, hela tunazo jeuri tunayo il mwisho wa siku mkumbuke lazima mpimwe corona kabla kuvuka mpaka.
Mkuu , Kuna rafiki zangu wamepita kuja kwenu , hivi majuzi, karibu boarder post zenu zote , kwenye Vipimo vya Corona Kuna rushwa ya kufa mtu.
Wewe uko huku ukisisitiza Watanzania wapimwe kuingia Kenya , Kwenye site ni pesa ndio inadetermine mtu aingie Kenya au abaki Tanzania.

Siafiki hata hivyo Kodi kupandishwa maana kutaumiza sana mkulima wa Tanzania.
 
Hapo ndio upumbavu wa tamaa za hela, yaani mtu anaamua kuwaponza raia wenzake kisa kapewa mihela......
 
Back
Top Bottom