Serikali yazitaka NGO's zote nchini kuwasilisha kwa Msajili taarifa za vyanzo vya Mapato

Huu uwazi/ transparency kwa umma ni kwa NGOs tuu? Serikali nayo iwe transparent na ianze kwa Kurudisha bunge live and then zitungwe sheria kulazimisha maafisa kutoa taarifa kwa umma/ waandishi.
Washughulikie ile kamati ya urosso, mbona waliotajwa wanapeta mpaka leo
 
waangewaachi jamani,wanasaidia serikali na jamii….
What if the cons outweigh the pros, unatetea sana hayo mashirika, umeajiriwa na mojawapo nini.
Serikali haiwafungii, chillax. Inawataka waelezee shughuli zao specifically, na vyanzo vyao vya pesa, mbona issue ni ndogo tu. Na ni sheria ya JMT.
Sasa unataka wawaachie tu, doesnt make sense.
 
Serikali imetoa siku 30 kwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali kuwasilisha kwa msajili wa NGOs taarifa zake za fedha,vyanzo vyake vya fedha pamoja na miradi ilinayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee Na watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma leo, ambapo amesema mashirika ambayo hayatafanya hivyo yatafutiwa usajili.

Dk Ndugulile amesema kumekuwa na tatizo la NGOs kufanya shuguli ambazo sio kipaumbele cha Taifa na wajibu wa kisheria, hivyo baada ya zoezi hilo kukamilika mashirika hayo yatatakiwa kutoa Taarifa zao za fedha pamoja na vyanzo vyake kwa serikali kila mwaka.
NGO=No Government Oders?
 
I must be frank,sizipendi NGOs.Zipo kwa ajili ya kutekeleza agenda za the New World Order au kwa kujua au kwa kutokujua.This is good move,hongera JPM.
Yani kwa akili zako unafikiri Magufuli wako ana uwezo wa kuipinga new world order
Jitafakali sana
 
Kuna vitu viwili hapo 1.kutoa Huduma za kiafya kwa Makundi maalum
2.kuhamasisha kuwepo kwa Makundi maalum yaani kuwepo kwa ushoga .
Naomba kujua Tanzania kunataasisi inayo hamasisha kuwepo kwa ushoga?(kama IPO haitufai) au kuna NGOs zinazotoa Huduma za kiafya ?
Tanzania hakuna taasisi kama hiyo!
 
Yani kwa akili zako unafikiri Magufuli wako ana uwezo wa kuipinga new world order
Jitafakali sana
Ipo vita ya chini kwa chini against the NWO inayoendelea kwa sasa ikiongozwa na Rais Putin wa Urusi akisaidiwa na Trump!You won't believe it, but it's real.Kama uko makini na ni mchunguzi mzuri nadhani utakuwa umeshaona alliances fulani kati ya Trump na Putin ambazo ni suspicious.Hata wao wenyewe sasa hivi wana wasiwasi,kwa kuwa kama kwa mfano serikali ya Marekani,European Union na Germany wakiamua na wakasaidiwa na Urusi ni kuwakamata tu kama Quelea Qulea,mbona wanajulikana?Mkuu a coup is possible,ngoja tusubiri.
 
Nani kakudanganya NGOs hazifanyi biashara? NGOs zina mapato kutoka kwa Donors sio lazima yatoke kwenye biashara.
Siku hizi NGOs ni profit making organization but not sharing.
Siyo NGOs zote zenye component ya biashara na hata kama zikiwepo so kwa ajili ya profits. Hebu weka mfano wa NGO moja inavyofanya biashara na kupata faida inayokuza biashara!
 
kwanza serikali imechelewa kufanya ufuatiliaji huo. hizi NGO ziko kwa ajili ya manufaa ya umma. MAANA wanapata misaada na michango toka kwa wafadhili baada ya kutoa mipango ya jinsi watakavyo wasaidia kundi fulani la JAMII katika kupambana au kutatua changamoto zao. hivyo ni vyema na haki wakawa na uwazi katika mapato na matumizi YAO. isije ikawa wanatumia michango ambayo waliiomba kwa kusaidia watoto yatima, badala yake wakatumia tofauti. ni wakati sasa SERIKALI iwe na miongozo ya namna GANI bora ya kusimamia hilo.
Zipo pia NGOs nyingi ambazo ni extention ya sera ovu za nchi za magharibi.Hizi ziwe identified na zifutwe kabisa.Tusipo kuwa makini tutakula mabua
 
Nani kakudanganya NGOs hazifanyi biashara? NGOs zina mapato kutoka kwa Donors sio lazima yatoke kwenye biashara.
Siku hizi NGOs ni profit making organization but not sharing.
Hapo ni sawa na kusema tufanye ukaguzi kwenye misaada anayopewa yatima au mhitaji yeyote
 
Serikali imetoa siku 30 kwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali kuwasilisha kwa msajili wa NGOs taarifa zake za fedha,vyanzo vyake vya fedha pamoja na miradi ilinayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee Na watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma leo, ambapo amesema mashirika ambayo hayatafanya hivyo yatafutiwa usajili.

Dk Ndugulile amesema kumekuwa na tatizo la NGOs kufanya shuguli ambazo sio kipaumbele cha Taifa na wajibu wa kisheria, hivyo baada ya zoezi hilo kukamilika mashirika hayo yatatakiwa kutoa Taarifa zao za fedha pamoja na vyanzo vyake kwa serikali kila mwaka.
Safi sana... ni wezi kweli2!
 
Back
Top Bottom