Serikali yazitaka NGO's zote nchini kuwasilisha kwa Msajili taarifa za vyanzo vya Mapato

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,724
2,000
Serikali imetoa siku 30 kwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali kuwasilisha kwa msajili wa NGOs taarifa zake za fedha,vyanzo vyake vya fedha pamoja na miradi ilinayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee Na watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma leo, ambapo amesema mashirika ambayo hayatafanya hivyo yatafutiwa usajili.

Dk Ndugulile amesema kumekuwa na tatizo la NGOs kufanya shuguli ambazo sio kipaumbele cha Taifa na wajibu wa kisheria, hivyo baada ya zoezi hilo kukamilika mashirika hayo yatatakiwa kutoa Taarifa zao za fedha pamoja na vyanzo vyake kwa serikali kila mwaka.
 
Attachments

  • File size
    24.2 KB
    Views
    0

Ochumeraa

JF-Expert Member
May 18, 2015
4,215
2,000
Kuna taarifa nimeiona Leo sikumbuki wapi,inasema serikali imefungia NGOs zote kwenye nchi hiyo kwa sababu zimeshindwa kufuata taratibu za nchi hiyo...Sasa nimeona hii taarifa nikaanza husianisha na ile taarifa
 
eliakeem

JF-Expert Member
May 29, 2009
11,555
2,000
kwanza serikali imechelewa kufanya ufuatiliaji huo. hizi NGO ziko kwa ajili ya manufaa ya umma. MAANA wanapata misaada na michango toka kwa wafadhili baada ya kutoa mipango ya jinsi watakavyo wasaidia kundi fulani la JAMII katika kupambana au kutatua changamoto zao. hivyo ni vyema na haki wakawa na uwazi katika mapato na matumizi YAO. isije ikawa wanatumia michango ambayo waliiomba kwa kusaidia watoto yatima, badala yake wakatumia tofauti. ni wakati sasa SERIKALI iwe na miongozo ya namna GANI bora ya kusimamia hilo.
 
Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
4,591
2,000
Hiii ni kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge yaani Tanzania NGO's Act ya mwaka 2002, sheria hii inayataka mashirika haya kudeclear financier wao, kazi wanazofanya na fedha zinatumikaje...Niliifanyia utafiti mwaka 2013/14 nikiwa mwaka wa mwisho chuo kikuu
 
Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
9,335
2,000
Serikali imetoa siku 30 kwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali kuwasilisha kwa msajili wa NGOs taarifa zake za fedha,vyanzo vyake vya fedha pamoja na miradi ilinayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee Na watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma leo, ambapo amesema mashirika ambayo hayatafanya hivyo yatafutiwa usajili.

Dk Ndugulile amesema kumekuwa na tatizo la NGOs kufanya shuguli ambazo sio kipaumbele cha Taifa na wajibu wa kisheria, hivyo baada ya zoezi hilo kukamilika mashirika hayo yatatakiwa kutoa Taarifa zao za fedha pamoja na vyanzo vyake kwa serikali kila mwaka.
I must be frank,sizipendi NGOs.Zipo kwa ajili ya kutekeleza agenda za the New World Order au kwa kujua au kwa kutokujua.This is good move,hongera JPM.
 
Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
9,335
2,000
Hiii ni kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge yaani Tanzania NGO's Act ya mwaka 2002, sheria hii inayataka mashirika haya kudeclear financier wao, kazi wanazofanya na fedha zinatumikaje...Niliifanyia utafiti mwaka 2013/14 nikiwa mwaka wa mwisho chuo kikuu
What did you find out?
 
eliakeem

JF-Expert Member
May 29, 2009
11,555
2,000
Hiii ni kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge yaani Tanzania NGO's Act ya mwaka 2002, sheria hii inayataka mashirika haya kudeclear financier wao, kazi wanazofanya na fedha zinatumikaje...Niliifanyia utafiti mwaka 2013/14 nikiwa mwaka wa mwisho chuo kikuu

you've a lot of inputs regardingthe subject.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,725
2,000
Serikali imetoa siku 30 kwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali kuwasilisha kwa msajili wa NGOs taarifa zake za fedha,vyanzo vyake vya fedha pamoja na miradi ilinayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee Na watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma leo, ambapo amesema mashirika ambayo hayatafanya hivyo yatafutiwa usajili.

Dk Ndugulile amesema kumekuwa na tatizo la NGOs kufanya shuguli ambazo sio kipaumbele cha Taifa na wajibu wa kisheria, hivyo baada ya zoezi hilo kukamilika mashirika hayo yatatakiwa kutoa Taarifa zao za fedha pamoja na vyanzo vyake kwa serikali kila mwaka.
Vipi TWAWEZA nayo ipo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom