Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jul 19, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Mwambigija, maarufu kama Mzee wa Upako na Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete, wamekamatwa na kusafirishwa hadi wilayani Chunya kisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kutoa maneno ya uchochezi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kusema kuwa walikamatwa juzi katika eneo la Inyara, wakiwa ndani ya basi kuelekea Dodoma.

  Alisema kuwa viongozi hao walisafirishwa hadi Chunya ambako waliunganishwa na wenzao wawili kabla ya kupelekwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

  Kamanda Diwani aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Katibu wa CHADEMA Kata ya Makongorosi, Erick Luvanda na Katibu Mwenezi wa kata hiyo, Dominick Chaula.

  Alisema baada ya kusomewa mashtaka yao mahakamani, watuhumiwa walipewa dhamana na kutakiwa kurudi tena mahakamani hapo Agosti 16, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kwa kesi hiyo.

  Hivi karibuni viongozi hao kwa kushirikiana na viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Chunya walifanya mikutano mbalimbali kwa siku 10 wilayani humo ikiwa ni sehemu ya operesheni iliyopewa jina la ‘CHADEMA Twanga Kotekote' yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kukijenga chama hicho.

  Source:Tanzania Daima
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hii kesi ndiyo itakayo wapatia jina hawa wakuu wa chama na kukiuza/kukitangaza chama kizuri zaidi kesi inafanyikia huko huko Chunya
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kesi iko mahakamani,hakuna kuiongelea hapa!
   
 4. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Duu hawa jamaa kwel cdm kikojuu tumeshazoe kes laa wala hatuogopi tunasonga mbele..
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kumpiga chura teke ni kumwongezea mwendo!!!!!
   
 6. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh, kaazi kweli kweli!
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wanawapaisha, chati yao itapanda kweli.
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hata iweje 2015 tutapeta tu.:flypig:
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Haya ni maandalizi tu, 2015 yataisha, halafu tutawfundisha jinsi ya kutawala bila hila na visasi. Hata wao watafurahi.
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni upepo tu, utapita.
   
 11. h

  hans79 JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Dalili za kuanguka kwa hiyo wanatapatapa lakini hawawezi kuzuia mabadiliko.Imekwisha amuriwe CHADEMA iwe na inakuwa.
   
 12. Kinyamagala

  Kinyamagala Senior Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nguvu ya dola haiwezi kuwanyamazisha wananchi walokata tamaa hata siku moja,UKWELI NA HAKI HUSHINDA DHIDI YA DHULUMA
   
 13. I

  IDIOS Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Mwambigija, maarufu kama Mzee wa Upako na Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete, wamekamatwa na kusafirishwa hadi wilayani Chunya kisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kutoa maneno ya uchochezi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kusema kuwa walikamatwa juzi katika eneo la Inyara, wakiwa ndani ya basi kuelekea Dodoma. Alisema kuwa viongozi hao walisafirishwa hadi Chunya ambako waliunganishwa na wenzao wawili kabla ya kupelekwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayowakabili. Kamanda Diwani aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Katibu wa CHADEMA Kata ya Makongorosi, Erick Luvanda na Katibu Mwenezi wa kata hiyo, Dominick Chaula. Alisema baada ya kusomewa mashtaka yao mahakamani, watuhumiwa walipewa dhamana na kutakiwa kurudi tena mahakamani hapo Agosti 16, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kwa kesi hiyo. Hivi karibuni viongozi hao kwa kushirikiana na viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Chunya walifanya mikutano mbalimbali kwa siku 10 wilayani humo ikiwa ni sehemu ya operesheni iliyopewa jina la ‘CHADEMA Twanga Kotekote’ yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kukijenga chama hicho.
   
 14. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mapito kuelekea tanzania tuitakayo, makamanda lazma tuteseke kwa ajil ya huyu mkolon mweusi.
   
 15. A

  Awo JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hivi hizi kesi huwa zinaishia wapi? Maana siha uhakika kama kuna hata moja imewahi kumalizika tukasikia hukumu yake ilikuwaje!
   
 16. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  siyo Tanzania ni Tanganyika tuitakayo
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mara nyingi huwa wanasamehewa na kuambiwa wasirudie tena.
   
 18. A

  Awo JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Ok. Polisi wangekuwa wanatangaza basi kama wanavyotangaza kuwakamata na kuwafikisha mahakamani. Mara nyingine huwa nadhani kazi ya polisi ni kukamata na kufikisha watu mahakamani, kinachoendelea si juu yao. Sijui wanapimaje mafanikio ya kazi zao.
   
 19. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanadhani kwa kufanya hivyo watapunguza kasi m4c kumbe ndio wanaibusti.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Laiti hawa watu wetu wanaosimamia haki wangekuwa wanawapeleka mahakamani mafisadi na weizi wa fedha za wananchi kwa spidi kama hiyo, nchi yetu ingekuwa pepo.
   
Loading...