Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Hakuna mtu kuchangia wala nini, hiyo itakuwa njia rahisi ya kuidekeza serikali kuwajibika. Binafsi nasema kama tunataka kuchangia iwe under two conditions:

a. Serikali itamke hadharani kuwa imeshindwa kuwasomesha vijana hawa na kutimiza ahadi yake kwao.

b. Prof. Msolla ajiuzulu na kukubali kushindwa kuisimamia bodi ya mikopo.

MKJJ

I understand mtazamo wako hapo juu cha muhimu hapo juu. That is too political demands kwa bongo yetu. Hao watoto huko waliko wataendeleakusota.
 
MKJJ

I understand mtazamo wako hapo juu cha muhimu hapo juu. That is too political demands kwa bongo yetu. Hao watoto huko waliko wataendeleakusota.

Kwa kweli kuwachangia hawa ndugu zetu ni jambo la Busara.Pia Prof.Msolla hiyo nafasi imenshinda, sijui ni binadamu wa aina gani huyu.Haiwezekani ashindwe kulitafutia ufumbuzi wa haraka hili jambo hadi hawa wanafunzi wateseke namna hii.Kwa kweli uzembe huu si wa kuvumilia hata kidogo ulioambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.Kwa hili MSOLLA NI BORA UJIUZULU
 
Yebo Yebo... naelewa unachosema lakini sitaki tuidekeze serikali.. maana wakijua Watanzania watachangia hawatawajibika. Nakubaliana na wazo la kuchangia, ngoja tutafute contacts kwanza halafu tuelewe nini kinachoendelea. Kesho (Jumatatu) nitajitahidi kuwapata wakubwa wa hiyo Wizara.. na hata Wizara Mkuu kiongozi Shujaa na Mahiri!!
 
Mkjj,

heshima yako mzee, hongera kwa jitihada zako zisizochoka.

kwa kweli huyu mh. MSOLLA anastahili ajiuzulu kwani kazi imemshinda, hata familiya yake inaonyesha hawezi kuiongoza sembuse Wizara.
 
Ndugu zangu inamaana mlikuwa hamjui ya kuwa serikali kuwatelekeza vijana wake kwa kipindi ambacho sio cha uchaguzi ni ajenda ya kudumu?nasema hayo kwa sababu tumewaona wamachinga wakiwa wanachinjiwa baharini,tumewashuhudia wanafunzi wa vyuo vikuu vya hapa nchini wakiwa wanachinjiwa baharini kwani kuwataka watu ambao wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku kulipia 40%ya ada yao wawapo vyuoni ni kutaka kuwaondoa wanafunzi maskini wasiweze kuipata elimu ya juu?

Nipende sasa kuwakumbusha jambo moja ambalo wanaforum mmekuwa mkiliangalia pasipo mkuweka uzito wa kutosha,
Hivi kitendo cha kusema kuwa watoto wa wabunge na maprofesa wasilipiwe na bodi sio cha kutaka kuwafanya wanafunzi kutoka familia maskini kukosa watu wa kuwasemea kwenye vyombo vya maamuzi kama vile bungeni ?
Je?kusema kuwa watoto wa maprofesa wasilipiwe ile hali sera za elimu ya juu huwa zinaandaliwa na hao maprosefa itakuwaje kwani wao wenyewe hata kama wakiaandaa sera mbaya hazitawadhuru wao kwani bodi haiwahusu?

hivi ni kwa nini nisiamini ya kuwa hawa viongozi wetu wanaompango wa kutugawa sisi watanzania kwenye tabaka la matajiri na maskini?kwani pindi migomo itakapoanza watajulikana dhahiri ni kina nani wanaolipiwa na bodi na ni wapi sio watoto wa vigogo?na hili litakuwa rahisi zaidi kuwadhibiti watoto wa maskini na kutoa matamko makali kuwa waliogoma hawapendi kufuata sheria na pia je wale watoto wa vigogo wakidemand kuendelea na masomo itakuwaje ile hali maskini wao wamegoma kwa kukosa mikopo?
 
MKJJ

Shukrani kwa mahojiano ya wanafunzi walioko Ukraine, huyu waziri ni lazima ajiuzulu ni muda gani anahitaji kutatua tatizo hili. Serikali iliwapeleka na kuwaambia kuwa itawalipia sasa yako wapi. HII NI AIBU WAKATI BALOZI ALIKWENDA KUWAONA NA ANAFAHAMU MATATIZO YAO.
 
itafurahisha sana kama vyombo vya habari vya nyumbani vyote kwa ujumla wao vitavalia njuga suala hili... maana leo ni mtoto wa mwenzako next time ni mtoto wako!!
 
Mzeee MMJ,

Vipi ukimtafuta huyo waziri au iandikwe barua safi kwake toka humu, ninakuahidi nitampa mikononi mwake kama ile ya Mahita!
 
Mzee ES....nimemtafuta sina contacts zake.. kama unazo nisaidie bwana... ikishindikana tutatuma barua..
 
Nimezungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Mhe. Nimrod Mkono kuhusu suala hili la wanafunzi kukwama huko Ukraine.... kuna mambo yamenishangaza...!!!
 
Back
Top Bottom