TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,514
- 11,277
Waziri Membe ameeleza kuwa nchi wahisani zilikuwa na Mpango wa kuanza kutoa msaada moja kwa moja kwenye sekta ambazo Serikali itakuwa inazainisha ikiwa na maana hawatakuwa wanapeleka fungu Serikalini. Kwa maelezo ya Membe ni kuwa Nchi wahisani zilitaka Serikali iwaambie iwapo watahitaji kuboresha sekta ya elimu basi wahisani watakuja na wataalamu wao kisha kutuboreshea Sekta ya elimu kama ni kujenga Shule au kununua vitabu.
Au kama tukihitaji maji basi wanakuja na wataalamu wao wanatuchimbia visima bila kutoa fedha Serikalini. Kwa maelezo ya Membe, ni kuwa Serikali ya Tanzania imeukataa Mpango huo na inataka wahisani watupatie hizo fedha kisha tutaamua wenyewe tunachohitaji kuzifanyia.
My take: Ni kwamba Serikali yetu imeonekana kuwa inababaisha kwenye matumizi ya fedha za misaada na nchi wahisani zinataka kuwakwepa. Kitendo cha Serikali kungangania hizo fedha kinatoa taswira kuwa Serikalini hakuna wabunifu wa vyanzo vya mapato na hivyo wasipopata hizo fedha Serikali haitaweza kusimama.
Siku wahisani wakisitisha hiyo misaada ina maana Serikali itajiuzulu?