Serikali yaugomea mpango mpya wa nchi Wahisani

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,502
11,247
Waziri Membe ameeleza kuwa nchi wahisani zilikuwa na Mpango wa kuanza kutoa msaada moja kwa moja kwenye sekta ambazo Serikali itakuwa inazainisha ikiwa na maana hawatakuwa wanapeleka fungu Serikalini. Kwa maelezo ya Membe ni kuwa Nchi wahisani zilitaka Serikali iwaambie iwapo watahitaji kuboresha sekta ya elimu basi wahisani watakuja na wataalamu wao kisha kutuboreshea Sekta ya elimu kama ni kujenga Shule au kununua vitabu.

Au kama tukihitaji maji basi wanakuja na wataalamu wao wanatuchimbia visima bila kutoa fedha Serikalini. Kwa maelezo ya Membe, ni kuwa Serikali ya Tanzania imeukataa Mpango huo na inataka wahisani watupatie hizo fedha kisha tutaamua wenyewe tunachohitaji kuzifanyia.

My take: Ni kwamba Serikali yetu imeonekana kuwa inababaisha kwenye matumizi ya fedha za misaada na nchi wahisani zinataka kuwakwepa. Kitendo cha Serikali kung’ang’ania hizo fedha kinatoa taswira kuwa Serikalini hakuna wabunifu wa vyanzo vya mapato na hivyo wasipopata hizo fedha Serikali haitaweza kusimama.

Siku wahisani wakisitisha hiyo misaada ina maana Serikali itajiuzulu?
 
Wao wanataka V8 kwa kila mtu na hawawezi kuletewa kama hela hawashiki wao,
 
sasa mnataka sisi wengine huku maofisini tule nini? kama wazungu wakifanya hivyo mbona mirija ya safari na magari mapya itakuwa imeziba? hembu tuacheni tutajua sisi wenyewe namna ya kupanga matumizi..alaaa
 
Tunaishi kwa kutegemea wahisani wakati tuna kila rasilimali za kutuwezesha kuishi bila kumtegemea yeyote,tutabaki kuwa taifa la kuombaomba kila siku huku mipango mingi ya maendeleo ikibaki bila kutekelezwa ipasavyo.
Ipo siku misaada itakata na hatutakuwa na pa kukimbilia na hapo ndio watu watajua maaana ya kauli ya MAPINDUZI....!!!!
 
Wanajua namna ambavyo wanachakachua miradi mbali mbali kwa hyo dili litaharibika kwao.
 
naungana na serikali kwa msimamo huo. Kwani kukubali hilo hakukuwa na haja ya serikali kuendelea kuwepo, hiyo ingekuwa ni hatua ya kwanza tu baadaye hata mipango ya maendeleo ingepangwa na wao wenyewe wahisani. na hicho si kitu kingine bali ni ukoloni halisi.
 
Viongozi wanaiba pesa huku wanaenda kuficha kwenye mabenki ya wanaotusaidia, alafu wanaomba tena wanasema miradi haikukamilika, ili wapewe waibe wakafiche tena!

Wahisani wanatuonea huruma watanzania, ndio maana wanaona njia ya kumkomboa mtanzania ni hiyo wanayotaka kuitumia.
.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wanajua namna ambavyo wanachakachua miradi mbali mbali kwa hyo dili litaharibika kwao.
 
Waziri Membe ameeleza kuwa nchi wahisani zilikuwa na Mpango wa kuanza kutoa msaada moja kwa moja kwenye sekta ambazo Serikali itakuwa inazainisha ikiwa na maana hawatakuwa wanapeleka fungu Serikalini. Kwa maelezo ya Membe ni kuwa Nchi wahisani zilitaka Serikali iwaambie iwapo watahitaji kuboresha sekta ya elimu basi wahisani watakuja na wataalamu wao kisha kutuboreshea Sekta ya elimu kama ni kujenga Shule au kununua vitabu.

Au kama tukihitaji maji basi wanakuja na wataalamu wao wanatuchimbia visima bila kutoa fedha Serikalini. Kwa maelezo ya Membe, ni kuwa Serikali ya Tanzania imeukataa Mpango huo na inataka wahisani watupatie hizo fedha kisha tutaamua wenyewe tunachohitaji kuzifanyia.

My take: Ni kwamba Serikali yetu imeonekana kuwa inababaisha kwenye matumizi ya fedha za misaada na nchi wahisani zinataka kuwakwepa. Kitendo cha Serikali kung'ang'ania hizo fedha kinatoa taswira kuwa Serikalini hakuna wabunifu wa vyanzo vya mapato na hivyo wasipopata hizo fedha Serikali haitaweza kusimama.

Siku wahisani wakisitisha hiyo misaada ina maana Serikali itajiuzulu?

Serikali ikikubali basi itakuwa imekubali ukoloni mkongwe kurudi nchini.
 
Huyu Membe aidha ni kilaza ama yuko usingizini.......mbona Marekani kupitia USAID wanaendesha miradi yao yote bila kuipa serikali hata senti tano? Tatizo serikali ikipewa pesa basi kama hazikuibwa zitatumiwa katika mambo yasiyo husiana na mradi au kuchelewesha mradi
Membe ni tatizo! kama unakumbuka chenji ya rada alivyoikomalia! Uingereza ilitaka kutumia njia kama hii ya kuja kununua vitabu, kujenga vyumba vya madarasa, maabara... n.k lakini kwa usimamizi wao! Membe akakataa tena kwa mbinde mpaka wabunge wakaenda wakiongozwa na Job Ndugai ndio pesa zikatolewa!

Lakini wapi? pesa kidogo zikaenda, zingine ndivyo sivyo, wakalipana mishahara maana kipindi zinatoka serikali ilikuwa choka mbaya.
Alafu tumpe urais huyu....? kama hatujakuwa kama Zimbabwe.
 
Nilitegemea Membe angesimama mara moja na kusema "Hatutaki misaada yenu tena" sasa tunajikita katika kumobilize rasilimali za ndani na kuhakikisha tunajitegemea. Unampa masharti mwenye kukupa msaada?Inawezekana kweli?
 
waziri membe ameeleza kuwa nchi wahisani zilikuwa na mpango wa kuanza kutoa msaada moja kwa moja kwenye sekta ambazo serikali itakuwa inazainisha ikiwa na maana hawatakuwa wanapeleka fungu serikalini. Kwa maelezo ya membe ni kuwa nchi wahisani zilitaka serikali iwaambie iwapo watahitaji kuboresha sekta ya elimu basi wahisani watakuja na wataalamu wao kisha kutuboreshea sekta ya elimu kama ni kujenga shule au kununua vitabu.

Au kama tukihitaji maji basi wanakuja na wataalamu wao wanatuchimbia visima bila kutoa fedha serikalini. Kwa maelezo ya membe, ni kuwa serikali ya tanzania imeukataa mpango huo na inataka wahisani watupatie hizo fedha kisha tutaamua wenyewe tunachohitaji kuzifanyia.

My take: Ni kwamba serikali yetu imeonekana kuwa inababaisha kwenye matumizi ya fedha za misaada na nchi wahisani zinataka kuwakwepa. Kitendo cha serikali kung'ang'ania hizo fedha kinatoa taswira kuwa serikalini hakuna wabunifu wa vyanzo vya mapato na hivyo wasipopata hizo fedha serikali haitaweza kusimama.

Siku wahisani wakisitisha hiyo misaada ina maana serikali itajiuzulu?


serikali lege lege siku zote hutegemea uhisani..
 
Wahisani wamejifunza kutoka Uganda. Fedha zao za misaada zimefisadiwa mchana kweupee!
 
Ningekua ni Mimi waisani ningekomalia mpaka misaada iende direct kwa walengwa kama hawataki napeleka kwa wanaotaka (bravo wahisani wabane majizi)
 
Serikali ikikubali basi itakuwa imekubali ukoloni mkongwe kurudi nchini.

Kama hawayataki hayo wakusanye kodi bila udanganyifu wa kuwaficha wakubwa na biashara zao, wapunguze kutanua na kutumbua peas ya wala kodi. Ni sawa mtu aliyeolewa au kuoa amchagulie mwenzie siku ya kulala uchi!
 
Serikali ikikubali basi itakuwa imekubali ukoloni mkongwe kurudi nchini.

Ukoloni huanzia kwenye fikra. Fikra za serikali hii ni kuomba misaada na kuifuja. Mi nasema ni viwete akilini ila midomo imeunganishwa na choo. Wanapewa misaada wanakula hawafanyii kitu. WAJIKOMBOE NA UTUMWA WA FIKRA. Pesa za wahisani zinachangwa na walipa kodi wao. Walipa kodi wetu wako lakini ndiyo usipime hizo ni allowance za akina Nape kuendesha CCM na kutekeleza mauaji ya kisiasa. HAZINA BARAKA.
 
Kweli serikali yetu inampungufu makubwa kwenye matumizi, na vipaombele vingi havitekelezwi kwasababu ya pesa zinapelekwa maeneo mengine yasiyo ya kipaombele. Lakini pia siafika wao kutekeleza miradi moja kwa moja hasa kwa maana ya usalama wa nchi na ukuzaji wa ajila zetu. mfano wachina ukiruhusu waje watekeleze watakuja na hata mfagizi pia sio tu hawaimini serikali bali hata mfanyakazi mweusi.
 
Mimi naunga mkono wazo la wahisani. Ni ukweli usiofichika kwamba pesa nyingi za wahisani zimekuwa zikiishia mikononi mwa watu binafsi huku miradi mingi ikisimama au kutekelezwa chini ya kiwango. Mfano ni riport za mkaguzi mkuu wa serikali C.I.G, utaona jinsi halmashauri zetu zinavyokwiba pesa na hakuna hatua inachukuliwa.

Wahisani pia wanakatishwa tamaa na jinsi viongozi wa serikali wanavyotanua na mashangingi na kujipa mishahara minono huku wakijua nchi inaendeshwa kwa mtindo wa ombaomba
 
Back
Top Bottom