chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Katibu mkuu wa wizara ya afya na Mkurugenzi utawala na utumishi wamezungumzia kuhusu suala la madaktari kukatwa mishahara na wanafunzi madaktari kutolipwa fedha za kujikimu,
Ktibu mkuu wa wizara amesema hawajakuwa na mipango ya kupeleka taarifa kwa jamii juu ya mipango iliyonayo serikali au mipango inayofanya ya kuingilia maslahi ya wafanyakazi kwenye sekta ya afya, amesema wanaangalia ni kwa jinsi watawafanya watu kupenda kuchukua kozi za afya na kuwafanya wafanye kazi sehemu mbalimbali nchini na sio mjini tu hasa Dar wakati kwingine kuna uhaba
Wizara ya Utumishi, Hazina pamoja na Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma inaangalia namna ya kufanya ili wote wenye vigezo vya uzoefu na elimu vilivyo sawa wapate mshahara sawa ili hata wanahamishwa masilahi yao yasiathirike kwa kuwa kuna taasisi kama MOI, Jakaya Kikwete, Muhimbili,Ocean Road kuwa na mshahara tofauti na ule unaotoka utumishi
Naye Mkurugenzi wa utawala na utumishi amesema sio hospitali zote za kikanda zitapunguziwa mshahara bali ni Bugando tu ndio watakaorekebishiwa kwa kuwa ndio wana mshahara tofauti na wengine
Kuhusu suala la wanafunzi au interns, hawatafutiwa posho zao wataendelea kupewa fedha