Serikali yatoa muda mpaka saa 12 jioni kwa mawaziri wasiopeleka tamko la mali watakuwa wamejiondoa

Hii nchi ni corrupt yaani maigizo kila siku, hivi kuorodhesha ndio kuonyesha kuwa kuna maadili mbona wakitoka madarakani hawaulizwi mali zao? Maskini yule mama jaji jana analalama kuwa sheria haijawapa nguvu ya kuhakiki hizo mali zinazoorodheshwa yaani hapo ni kazi bure tu
 
Huu ni usanii tu.Watanzania tunadanganywa mchana kweupe.
Kwani kero za watanzania ni hizo form?
Ajabu hata JP naye hajajaza za kwake wala kutangazia umma kwamba ameingia pale mjengoni akiwa anamiliki nini.Utawala wa mtu mmoja.....hakuna katiba hakuna sheria usanii mtupu!
 
mazingaombwe haya,tutafiki 2020 kwamatukio ukija kuuliza utendaji na mafanikio utaambiwa,tulifukuza flani,tulikamata hiki,ila ukigeuka upande wapili inflation kama kawaida inazidi kukwea alafu maisha still duni
Hadi sasa majipu yaliyokwisha tumbuliwa ni mengi,lakini hakuna mrejesho wa maana.....
Na kila siku yanazidi kutumbuliwa mapya.
Time will tell.
 
Hawa wangetakiwa kufukuzwa siyo kupewa muda kwani walikuwa hawajui kuhusu hizo kujaza hizo fomu?
 
Hii nchi ni corrupt yaani maigizo kila siku, hivi kuorodhesha ndio kuonyesha kuwa kuna maadili mbona wakitoka madarakani hawaulizwi mali zao? Maskini yule mama jaji jana analalama kuwa sheria haijawapa nguvu ya kuhakiki hizo mali zinazoorodheshwa yaani hapo ni kazi bure tu

Sheria inawataka wahakiki mali lakini wamekosa fedha na rasilimali watu. Hicho ndicho alichosema mama jaji.
 
Hapo hakuna atakae achishwa kazi, hichi kibarua kingepewa wananchi maana wangetoa taarifa mpaka zile mali zilizolimbikizwe kwa majina ya watu wengine.
 
Mahiga amesharudisha, naibu waziri amesema atarudisha leo, Kitwanga amesema alishatudisha na anashangaa jina lake kutajwa hivyo katoka nduki kwenda kufuatilia kulikoni huko secretariet, wengine bado kimya kutokana na ITV habari saa tisa alasiri.
 
Ifikapo saa 12 ipigwe roll-call ili tujulishwe parade nani ametekeleza na nani hajatekeleza. Itakuwa safiiii kama enzi za MSTARINI asimamapo Kiranja Mkuu
 
Hii sasa dharau adi mtangazwe ndo mnarudisha me naomba mmoja ajifanye kama vile ajasikia ili tuone action itakayochukuliwa na serikali
 
Baada ya watumishi wa umma kuainisha mali zao..naomba na kila chama cha siasa kiainishe matumizi yao katika uchaguzi mkuu uliopita 2015
 
Wanaeleza waksti wanaingia madarakani mbona wakitoka hawasemi wamenufaikaje ma cheo alichopewa na mali alizovuna. Utoto huo
 
Sheria husika irekebishwe ili mtumishi yeyote wa umma ajaze fomu hizi. Wapo "makarani" ambao wanawezs kuwa na mali au madeni yasiyoendana na vipato vyao. Pia nashauri Sekretariat iongezewe nguvukazi ili waweze kuhakiki mali na madeni ya watumishi wa umma kila mwaka hata kwa sampuli(sample of the total population) nzuri inayokubalika kama afanyavyo CAG.
 
Serikali ifuatilie hizo Mali kwa umakini na isiishie hapo iende kwa public servants hasa pale UDSM kuna mtu kila siku anakwepa hii kwa kwenda China sasahivi kibali kinatoka kwa Mkulu hii lazima itamhusu kipindi hiki
 
Back
Top Bottom