ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 45,536
- 52,619
Kwa mujibu wa karibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma anasema Vigogo wa Serikali Wamekwepa kueleza vyanzo vya Mali na utajiri wao.
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema baadhi ya viongozi wamekwepa kutoa ufafanuzi wa vyanzo vya mapato waliyonayo na wameshindwa kutaja thamani ya mali walizonazo kwenye fomu ya tamko la mali.
Pia imesema baadhi ya viongozi wameshindwa kujaza taarifa za wenza wao hasa taarifa za fedha zilizoko benki na kukwepa kujaza vipengele muhimu, huku wengine wakipokea zawadi mbalimbali bila kuzitolea matamko.
Hayo yamo kwenye taarifa ya sekretarieti hiyo iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki na Kamishna wa Sekretarieti hiyo, Sivangilwa Mwangesi, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari juu ya mafanikio ya sekretarieti.
Chanzo: Nipashe
Swali.
Kama watu Wameshindwa kuelezea walivyopata Mali,ni wazi wameibia Wananchi,Kwa nini Sekretarieti haiwapeleki TAKUKURU?