Serikali yatoa hongo kwa wabunge - tafsiri yangu

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
nec%2B3.jpg


Tafsiri yangu juu ya ongezeko la posho za wabunge kisirisiri wakati wa kikao cha bunge kilichomalizika bila kufuata utaratibu na hata baadhi ya wabunge kutojua nini kinachoendelea, ni mbinu mpya iliyobuniwa kuwarubuni wabunge wa CCM kupitisha mswada wa sheria ya katiba mpya. Hii inatokana na ukweli kwamba jambo hilo limefanyika sambamba na jitihada za serikali na wabunge wa CCM kutumia wingi wao kupitisha mswada huo.

Ishara za nyakati zinaonyesha jinsi serikali inavyotumia mbinu za kuwafumba macho wabunge kwa kuwaongezea mishahara, malupulupu kwa vile ni chombo pekee chenye kuinyooshea serikali vidole inapolegalega au kuvujisha pesa za umma.
 
acha wale tu.........na wanachuo wanakosa mikopo wao wanaongeza posho zao,,,, acha waleeee, kuleni tu sie tulipe kodiiiii......... ila kama mnaona hadi watu wa shinyanga -- wasukuma wamewachoka mjue hali si shwari we waache tuuu, iko siku wabunge hawatarudi majimboni.
 
Mkuu,
Tunashukuru kwa taarifa, kana ka harufu kaukweli kwenye taarifa yako. That being the case, the future of our country is dark.
 
Ila kiukweli bi kiroboto ni kikwazo cha demokrasia. Nakumbuka mwaka juzi ulizuka mjadala mkubwa sana wa matumizi ya fedha ya barabara ya Chalinze - Segera kutokana na kuwa mwaka mwingine wa fedha ambao haukuwa umepitishwa!!!!

Leo hii bunge linapandisha posho kinyemela za wabunge huku kukiwa hakuna kikao cha bunge chochote kilichoridhia upandishwaji huo.
 
Mkuu,
Tunashukuru kwa taarifa, kana ka harufu kaukweli kwenye taarifa yako. That being the case, the future of our country is dark.

Binafsi nimeshtushwa na habari hii ya kupandishiwa kiwango cha posho kwa waheshimiwa wabunge kwa usiri mkubwa wakati huo huo mswada wa sheria ya kutunga katiba mpya ukiwasilishwa bungeni. Kwa vyo vyote kuna dalili za kutumia ongezeko la posho kuwarubuni wabunge wa CCM wapitishe, na mara baada ya kupitishwa wakafanyiwa tafrija huko huko Dodoma na Rais Kikwete kwa kuwapongeza wabunge wa CCM pekee.
 
Back
Top Bottom