Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
In the early eighties nilipokuwa nawatembelea wenzangu waliobahatika kuingia UDSM niliwakuta wakihangaikia maji. Kama sijakosea ni wakati huo wakajengewa vyoo vya shimo ambapo mtu ukitoka unanuka dawa ya choo. Sasa watoto wao wameingia hapo hapo na matatizo waliyoyakuta baba na mama zao bado yapo. Wamekaa miaka zaidi ya miaka 20 bila kutatuliwa matatizo ya msingi na bado mnataka wawe wastahimilivu? Ustahimilivu una mwisho na mwisho wake mara nyingi si mzuri!
P.S. Karibu tena Bin Maryam!
Kwa mujibu wa Ripoti ya Ulinzi na Usalama iliyowasilishwa Bungeni Dodoma, uamuzi huu umetokana pia na yaliyojiri siku ya wanafunzi duniani Novemba 17 mwaka 2007 ambapo wakati ambapo CHADEMA ilifanya Kongamano ambalo wanafunzi walikwenda kwa gharama zao wenyewe maelfu wakati lile la CCM pamoja na kuwalipa fedha walikwenda wachache tu na waliokwenda bado waliisema serikali ya CCM kutokana na ufisadi. Hivyo, ripoti ya Ulinzi na Usalama kuhusu Hali ya Siasa Tanzania iliyowasilishwa kwenye kikao cha NEC Butiama ikaeleza hatua za kuchukua. Itafuteni tu hiyo ripoti mtaelewa nasema nini. Baadaye sekretariati ya CCM ilakaa na kutoa maelekezo yafuatayo:
1. Mikoa yote yenye vyuo vikuu nchini uongozi wa CCM mkoa ihakikishe wanaoshinda nafasi za uongozi wa wanafunzi wawe wanaCCM kwa gharama yoyote ile. Tayari barua za maelekezo zimashatolewa kwa ajili ya chaguzi za SUA na Mzumbe zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
2. Viongozi wenye msimamo mkali na wale wanaolekea kuunga mkono CHADEMA pale UDSM ama wananunuliwa kwa gharama yoyote au wanatishwa na kunyamazishwa. Rais wa wanafunzi Daudi Deo ameshanunuliwa na sasa yuko kwenye payroll. Tabu ilikuwa kwa Mtatiro na kigenge chake cha vijana wengine kama wakiongozwa na kijana mmoja anayeitwa Owawa
3. Wanafunzi wa UDSM wachonganishwe na umma kwa kuhusushwa na kashfa za ngono, bangi na kuonyeshwa kuwa wanasimamia maslahi yao madogo madogo. Kwa ujumla ni mkakati wa kufunika mijadala ya ufisadi pale chuoni.
Kumbuka haya yalifanyika baada ya Zitto kuzuiwa kutoa mhadhara pale na wanafunzi kuandamana. Mara baada ya Kongamano la Nov 17 yalifuata pia maandamano ya TAHLISO kuhusu ufisadi yaliyokwenda mpaka Jangwani.
PM

Nimeandika kimakosa hapo juu. Sio bungeni Dodoma, ripoti hiyo iliwasilishwa kwenye kikao cha NEC Butiama
Mawazo yangu yote yalikuwa Dodoma wakati naandika
PM
Ni kweli tupuNilitembelea hapo mlimani mwaka 2006..na pia niligundua mambo mengi tu!Maprofessa wenyewe kazi yao kunywa pombe kuanzia asubuhi hadi jioni huku wakishinda na mabaamedi na kuwa wabishi tu by nature!..nenda groceries zote kuwanzia maeneo ya mwenge..utawakuta wakati waliotakiwa kulecture wao wanayachapa maji..they dont care coz nobody cares anyways!Mambo ni mbaya kwa sana!Na pia narudia kuwa mabadiliko yanayohitajika ni makubwa sana na sio haya mabishano ya hapa na pale kuona nani atashinda..we've got to be true and tell the truth only..KATIBA NI LAZIMA IBADILISHWE!Mwafrika wa kike, ingawa wengine hapa JF wanakuona kama mwenye msimamo mkali lakini nimekukubali sana, what you say makes sense.
Hoja hapa si kuwalaumu wanafunzi eti ni vihiyo na digri za vichupi, etc. Kwani hao wanafunzi ni product ya nani au nini? Ya education system yetu, walimu wabovu since vidudu, kukosekana kwa vitendea kazi, walimu below standard, mitihani inayo-leak kila kukicha, etc! Kwa hiyo kuleta hiyo argument will not fly. Also they are entitled to choose leaders that they want.
Kumtetea Mukandala siwezi kwa sababu ni lazima atumie hekima. Wanafunzi duniani kote wanajulikana kuwa radicals, na dawa si kuwapiga na kuwafunga jela. That's unacceptable! Na kama hii issue ya mama mjamzito ni kweli, the government has to answer.
Naomba niwakumbushe tunapenda kusema "huwezi kushindana na serikali" lakini hii ni kutoka enzi za ujamaa na one party system, hivi sasa katika democratic system, the government is the people. What we giveth, we taketh. Let us prove this to CCM and taketh away their power to govern because clearly they have failed!
samhani nahisi yote mliongea ni sahihi lakini hayana lakini hayazingatii ukweli na wakati. kuwalaumu wanafunzi hawa ambao wanajua nini wanadai huku maisha yanazidi kuwa magumu kwao kusoma kwa tabu huku milioni zaidi ya mia zinalipwa Richmond na nyingine zaidi ya 140 zinalipwa mkapa na wenzake kila siku na mafisadi hapo huru wanatesa tunawaonea. tuwe wakweli tusikurupuke tujadili mambo ya maana sio kupiga porojo eti kwa vile una nafasi ya kutuma ujumbe. ni muhimu tuwe realistic ili ukweli upatikane. kufurahia wanafunzi kupigwa na kupelekwa mahakamani wakati Balali, Mkapa Lowasa na kina Visenti (Chenge) wamefisadi nchi kiasi hiki na bado wanatesa na mashangingi barabaraniwakati hatudai nao wapigwe wala hawapelekwi mahakani ni ujauzito wa mawazo
Hili la uchaguzi nimeshasema tangu jana kwamba hapa utawala umechemsha sana. Enzi zetu mambo ya DARUSO elections yalikuwa ya kwetu na utawala ulikuwa haugusi zaidi ya kumtuma Dean of Students kama observer tu. Ndio nasema wanafunzi sio watoto wadogo, waachwe wafanye mambo yao na wawajibike nayo. Ndio wanajifunza kujitegemea hivyo. Katika hili mbona tupo page moja kabisa.
Tatizo lingine kubwa hapa ni lack of clarity juu ya sababu hasa za mgomo. Sasa wote tuna-struggle kutafuta sababu, lakini ni jukumu la wagomaji: (i) kueleza kwa uwazi kabisa sababu za kugoma (ii) kushawishi jamii kwamba mgomo wao ni muhimu na kwamba wametumia njia zote imeshindikana na imebidi wagome (iii) mgomo wao sio kwa ajili ya maslahi yao leo tu bali pia ni katika kudai mambo ya msingi yatakayosaidia hata kizazi kijacho.
Principle moja tuliokuwa tunatumia sisi ni kwamba tulikuwa hatupo tayari kufanya mgomo (i) bila kueleza sababu vizuri za kugoma na zikaeleweka (ii) tulikuwa tunahakikisha kwamba katika kila mgomo tunakuwa na agenda inayogusa jamii ili tupate sympathy ya kutosha ndio maana utakuta kwamba tuliweza kwenda kupeleka msaada wa unga kwa wale wananchi waliobomolewa nyumba kule Kwamzungwi-Pugu. Na kuna kipindi tuligoma kwa ajili ya pesa za chakula lakini ndani yake tukaweka agenda kwamba tunadai nyongeza ya bajeti katika waizara ya elimu na kila mtu akatuunga mkono. Lengo ilikuwa ni kuonyesha kwamba DARUSO ni chombo cha kuwasemea wasio na sauti (voice of the voiceless)na wala sio chombo cha kutetea mambo ya mkate na bluebend za wanafunzi tu.
Tatizo la wanafunzi wetu leo sababu za migomo (i) hazieleweki kwa hiyo kila mtu anabaki kubuni (ii) hazigusi jamii na hivyo inakuwa rahisi kwa serikali kushinda maana wanaishia kuzomewa na wananchi walio wengi.
Nakuhakikishia serikali haiwezi kufunga chuo kwa sababu ya mgomo ikijua wanafunzi wana sympathy ya wananchi katika mgomo wao. Kila mara serikali kabla haijafunga chuo huwa inasoma kwanza maoni ya wananchi; wakiona wananchi wengi hawaungi mkono mgomo wanafunga, wakigundua wanafunzi wana sympathy ya wananchi hawafungi. Hili ni jambo ambalo viongozi wa wanafunzi ni muhimu wakilijua. Always make sure your agenda is relevant to the people's problems, otherwise mtabaki peke yenu na wananchi wa Manzese watawazomea!
In the early eighties nilipokuwa nawatembelea wenzangu waliobahatika kuingia UDSM niliwakuta wakihangaikia maji. Kama sijakosea ni wakati huo wakajengewa vyoo vya shimo ambapo mtu ukitoka unanuka dawa ya choo. Sasa watoto wao wameingia hapo hapo na matatizo waliyoyakuta baba na mama zao bado yapo. Wamekaa miaka zaidi ya miaka 20 bila kutatuliwa matatizo ya msingi na bado mnataka wawe wastahimilivu? Ustahimilivu una mwisho na mwisho wake mara nyingi si mzuri!
P.S. Karibu tena Bin Maryam!
Kitila,
[/SIZE]
- Wale wote walioleta vurugu wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
- Kutolewe elimu kwa wanafunzi, e.g. seminars, letters, n.k., kuwaelimisha nini faida na hasara za migomo, with concrete examples of those affected in the past. Waelimishwe juu ya haki ya kila mtu kugoma au kutogoma without intimidation.
- Kunapokuwepo dalili za migomo, ni muhimu kwa uongozi wa chuo kuimarisha ulinzi kwa kuongeza polisi wa doria kwenye maeneo yote ili anayetaka kugoma awe salama na yule asiyetaka naye pia usalama wake uhakikishwe. Hii itazuia tabia ya kuleta FFU baadaye wakati furugu zinapoanza au munkari wa wanafunzi unapokuwa umepanda.
Im shocked!Natumaini Maghembe ataelezea hizi habari zinazovuma hapa kuwa polisi wameua mama mjamzito mwanafunzi wa UD aliyekuwa anaendelea na maisha yake hapo shuleni!
Kitila,
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa mgomo wa wanafunzi haueleweki kabisaa.
Mambo mengine ni ya kitoto kiasi cha kujiuliza nini kimekisibu UDSM? Migomo sasa imekuwa na mfumo wa kisekondari, maana inashangaza kuwa, eti wanafunzi wamegoma na kufikia kuvunja sheria kwa vile tu hakuna maji au kwa vile a 'Ugandan' student amekataliwa kuwa kiongozi wao, how stupid is this.
Are these reasons worth sucrificing their entire future? What would have happened if they had elected a different candidate? What if they had continued to register their water shortage grievances with the VC, Minister etc? Hawa wanafunzi inaonekana kabisa walikuwa na nia ya kugoma na walichokuwa wanatafuta tu ni sababu tu ya kugomea tu. This insanity has to stop. Other universities, Tumaini, Nyegezi etc., will soon outshine UDSM because of these never ending foolishness.
Kitila makes some good points but fails to conclude. Here are my takes;
Wale wote walioleta vurugu wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Kutolewe elimu kwa wanafunzi, e.g. seminars, letters, n.k., kuwaelimisha nini faida na hasara za migomo, with concrete examples of those affected in the past. Waelimishwe juu ya haki ya kila mtu kugoma au kutogoma without intimidation.
Intimidators wa wanafunzi wanaopingana na migomo wachunguzwe na kupewa adhabu kali ikiwemo hata kufunguliwa mashitaka. Ni muhimu kwa wanafunzi kuelewa kuwa intimidation sio demokrasia. Kama wao wanapinga serikali kutumia nguvu kuzima matakwa yao, hawana budi na wao kuacha vitendo vya vitisho kwa wanafunzi na waalimu wao wasiokubaliana nao.
Chuo kisisimamishe masomo wala kubadilisha ratiba yake wakati wanafunzi wanapogoma au kusababisha chuo kufungwa. Hili liwe wazi wakati wanafunzi wanapojiunga ili waelewe consequences za kugoma.
Kunapokuwepo dalili za migomo, ni muhimu kwa uongozi wa chuo kuimarisha ulinzi kwa kuongeza polisi wa doria kwenye maeneo yote ili anayetaka kugoma awe salama na yule asiyetaka naye pia usalama wake uhakikishwe. Hii itazuia tabia ya kuleta FFU baadaye wakati furugu zinapoanza au munkari wa wanafunzi unapokuwa umepanda.
Mwisho ni ushauri wangu kwa wanafunzi waliomo humu mtandaoni ni kuwa, ni vizuri sana kushiriki katika siasa iwe ni CCM au upinzani. Lakini jihadhari sana kutumia imani zako za kisiasa kwenye mambo ambayo yataingiliana na ulichofuata hapo chuoni, kwani unaweza ukakosa vyote.
Halafu nikisema naanza kuambiwa eti nina low self esteem....inseciruty...na mambo mengine lukuki. Hivi inachukua muda gani kutatua haya matatizo ya wanafunzi...karne?
wanashida gani wakati watoto wao wamejaa huku UK na US wanasoma colleges wakitoka huku wanawekwa bank kuu, kwanza nataka kujua watoto wa magembe wanasoma wapi,mwenye taarifa zao azilete hapa
....inaweza kuwa 'shock' kwa upande wako! lakini nipo bega kwa bega na wewe juu ya suala hili!
...again, inabidi watu tuache tabia ya 'ndio hali halisi'!! jamani eeenh kukatika kwa maji sio sahihi (tena hasa tatizo hili linapokuwa sugu), lift kutokufanya kazi sio sahihi, umeme kukatika hovyo hovyo sio sahihi(tena sio chuo tu, bali kila mahali....hizi ni huduma muhimu sana kuwa treated kama ni anasa).
....uongozi wa chuo hautakiwi ku-influence chaguzi za wanafunzi!! hii tabia ipo hata sekondari, walimu wakuu/walimu wa nidhani wanakuwa na mkono ktk chaguzi za wanafunzi(nimeyaona haya pale ilboru)....tabia hii lazima ikome!!
.....narudia tena, ulalamishi huu wa wanafunzi ni halali pasipo kuwa na shaka, na yeyote anaedhania vinginevyo ana matatizo makubwa sana ya uhuru wa kufikiria!!.
Mimi nadhani tatizo lilianzia na Nyerere, msingi mbovu husababisha nyumba mbovu. Nyerere asingekifungua hicho chuo kabisa. Hawa viongozi wa sasa wanatelekeza lile lililoanzishwa na marehemu; hawawajibika hata kidogo kwa matatizo yanayoendelea hapo chuoni. Nyerere na yeye si aliwatimuaga wanafunzi pale, hawa wanafuata nyayo tu hawana utashi wao binafsi.