Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Tatizo limetokea suala hapa
Ni ku ainisha suluhu ya tatizo,tatizo letu wantanzia ni kulindana.

Wanajumuia,washika dau wa udsm acheni UNAZI semeni tatizo nini pale udsm.

Migomo ya udsm sio ya jana niza enzi na enzi ,kumbukeni 1990 nini kiliwakuta akina mbatia.

Semeni ,hizi migomo inateteresha uchumi wetu Na maamuzi ya hao viongozi ndio yanaua kabisa uchumi
 
Tatizo limetokea suala hapa
Ni ku ainisha suluhu ya tatizo,tatizo letu wantanzia ni kulindana.

Wanajumuia,washika dau wa udsm acheni UNAZI semeni tatizo nini pale udsm.

Migomo ya udsm sio ya jana niza enzi na enzi ,kumbukeni 1990 nini kiliwakuta akina mbatia.

Semeni ,hizi migomo inateteresha uchumi wetu Na maamuzi ya hao viongozi ndio yanaua kabisa uchumi


tatizo lipi? matatizo yaliyopita kwa taarifa yako most of the yalipatiwa suluhu kwa njia hii hii ya mgomo. Kwa hili la sasa tatizo halijawekwa bayana so suluhu itapatikanaje?
kulindana? inaonyesha wewe ndio uyelijua sana hili ni vyema ungesema tu ukweli unamlinda nani.

Wewe ulikuwepo UDSM hiyo 1990s, acha kukomalia mambo bila kujua kiini. Haya kumbusha kilichowakuta kina Mbatia na uwataje hao wenzie ni kina nani.

kuitana majina sio nia njema, hao unaowaambia waache UNAZI unafikiri wanafurahia kuitwa hivyo? then unawataka waseme, waseme nini ilhali wewe unajua kila kitu na unachokijua wewe ndio sahihi? usiwafanye watu wajinga hapa, kukaa kimya sio kushindwa hoja, sometimes ni kuepuka kupewa jina.
 
tatizo lipi? matatizo yaliyopita kwa taarifa yako most of the yalipatiwa suluhu kwa njia hii hii ya mgomo. Kwa hili la sasa tatizo halijawekwa bayana so suluhu itapatikanaje?
kulindana? inaonyesha wewe ndio uyelijua sana hili ni vyema ungesema tu ukweli unamlinda nani.

Wewe ulikuwepo UDSM hiyo 1990s, acha kukomalia mambo bila kujua kiini. Haya kumbusha kilichowakuta kina Mbatia na uwataje hao wenzie ni kina nani.

kuitana majina sio nia njema, hao unaowaambia waache UNAZI unafikiri wanafurajia kuitwa hivyo? then unawataka waseme, waseme nini ilhali wewe unajua kila kitu na unachokijua wewe ndio sahihi? usiwafanye watu wajinga hapa, kukaa kimya sio kushindwa hoja, sometimes ni kuepuka kupewa jina.

Mambo ya kufichana yamepitwa na wakati mtu kama ni Mnazi nitamuita mnazi mpaka kieleweke.Ni kama walivyo kwa mafisadi kama ni fisadi ni fisadi hakuna tasifida hapa.

Matatizo gani wewe unayosema yamepatiwa ufumbuzi??? MAMA acha kuhadaa watu.
statistics toka mwaka 2000 udsm wameshagoma na kusimamishwa zaidi ya mara NNE na wamegoma mfululuzo zaidi ya miaka 3 kutokea leo na ukirudi nyuma.Sasa wewe unasema yamepatiwa ufumbuzi yepi hayo??

endelea na makala hii kutoka majira

Habari za Tanzania Ijumaa Apr 25, 2008

Imetolewa mara ya mwisho: 25.04.2008 0127 EAT
•
Tatizo Chuo Kikuu ni Mukandala - TAHLISO

Habari Zinazoshabihiana
• Chuo Kikuu sasa wamwangukia Kikwete 03.05.2007 [Soma]
• Uongozi Chuo Kikuu waijibu DARUSO 09.05.2007 [Soma]
• Sitta ateua wajumbe Baraza la Mitihani 17.10.2007 [Soma]

*Wampa siku nne kurejesha wanafunzi waliofukuzwa
* Wengine 62 watimuliwa

Na Gladness Mboma

UMOJA wa Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) umemjia juu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala kwa madai kuwa ndiye kiini cha kupotea amani chuoni hapo.

Wanafunzi hao pia wamemtaka Prof. Mukandala kuhakikisha anawarejesha chuoni wanafunzo wote waliofukuzwa ifikapo Aprili 27 mwaka huu.

Mbali na hilo, TAHLISO imemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe afute kauli yake ya kuwafutia udahili na kuwanyima mikopo wanafunzi wanaotuhumiwa kuhusika na mgomo sambamba na kutaka wasidahiliwe katika chuo chochote nchini.

Wanafunzi hao walidai kauli ya waziri huyo ni ya kibabe, kiburi na ukatili dhidi ya vijana wa nchi hii kwani kwa kiasi kikubwa mgogoro ulioibuka chuoni hapo umechangiwa na uongozi wa chuo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa TAHLISO Bw. Chitage Edwin, alisema kuwa taasisi hiyo inathamini zaidi amani na haki kuliko kile alichoita 'umamluki' wa Prof. Mukandala.

"Uchunguzi wa TAHLISO umebaini kuwa Prof. Mukandala ndio chimbuko la kuvunjika kwa amani mara kwa mara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tunamtaka Mukandala awarejeshe wanafunzi wote ifikapo Aprili 27. TAHLISO inathamini zaidi amani amani na haki kuliko umamluki wa Profesa Mukandala," alisema na kuendelea kuwa;

"Tunalaani kitendo cha utawala wa chuo kuingilia mchakato wa uchaguzi. Kitendo cha uongozi wa chuo kuandika barua kusitisha uchaguzi na kubandika katika kuta na mbao za matangazo pasipokujadiliana na tume ya uchaguzi ni kinyume cha kanuni za uchaguzi chuoni hapo.

Kwa utafiti tuliofanya kulikuwa hakuna hali yoyote ya hatari kwa kipindi hicho, hivyo chuo hakikuwa na sababu yoyote ya kuingilia utaratibu tena bila hata kuvihusisha vyombo mahususi kama Tume ya uchaguzi,"alisisitiza Bw. Edwin

Bw. Edwin pia aliwataka wakuu wa vyuo wenye tabia hiyo, kuwaacha vijana wajifunze utamaduni wa demokrasia kwa kufanya chaguzi huru na haki pasipokushinikizwa na kutishwa.

Pia amewakumbusha wakuu wote wa vyuo kuongoza vyuo vikuu kitaalamu na waepuke umamluki au upiga debe wa propaganda chafu za kisiasa na kwamba ni lazima wakumbuke wakati wote kuwa chuo kikuu si jimbo la uchaguzi.

"Tunautaka utawala kusitisha mara moja hujuma kwa mwanafunzi kutoka Uganda aliyekuwa mgombea wa urais, uwaachie wao ndio wataamua kupitia sanduku la kura kama anawafaa au hawafai

Nchi hii haikujengwa katika misingi ya ubaguzi wa aina yoyote ile,tunauonya uongozi wa chuo wasiwe vinara wa kupanda mbegu ya ubaguzi. Kwa mujibu wa Katiba ya Serikali ya Wanafunzi hakuna kipengele kinachomzuia raia kutoka nje ya Tanzania kuwa kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi,"alisema Bw. Edwin

Bw. Edwin alisema kuwa inashangaza kuona kila kukicha Bw. Odongo Odwa wa Uganda anahujumiwa. Katika vyuo mbalimbali duniani imetokea viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka nchi tofauti na kwamba inashangaza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumkana mwanafunzi ambaye wao walimdahili na kuhoji shutuma hizo kuibuliwa wakati wa uchaguzi.

Pia Bw. Edwin aliushangaa uongozi wa chuo kumsimamisha masomo kwa siku 30 badala ya kumpa ruhusa yenye muda wa kutosha kuwasilisha vyeti hivyo.


Alisema kuwa TAHLISO inaamini kuwa jamii bora hujengwa kwa maridhiano na sio kwa nguvu za polisi, mahakama na vitisho na kwamba mtindo wa kuwatisha, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha vijana wasomi utaipeleka nchi pabaya.


"Tunamshauri Bw. Rwambow (Jamal, Kamanda wa Polisi Kinondoni ) kuwa ni vema angetumia nguvu hizo kuwakamata mafisadi na kuwapeleka mahakamani badala ya kuwaonea vijana hawa wahanga wa umaskini na utawala mbya wa nchi hii

Naye Reuben Kagaruki anaripoti kuwa wanafunzi 62 wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wamefukuzwa masomo na wengine 415 wanachunguzwa kufuatia vurugu zilizoibuka chuoni hapo tangu Jumatatu, wiki hii na kusitisha shughuli za masomo.

Uamuzi huo ulitangazwa ana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Mukandala, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua zilizochukuwa na uongozi kufuatia vurugu zilitokea chuoni.

Alisema wanafunzi waliofukuzwa masomo wataruhusiwa kuomba upya udahili iwapo watashinda kesi zao zinazowakabili mahakamani.

Alitaja kundi la kwanza la wanafunzi waliofukuzwa kuwa ni 15 ambao walihusika na vurugu zilizotokea chuoni hapo na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja.

Profesa Mukandala alitaja kundi jingine la wanafunzi waliofukuzwa kuwa ni 38 ambao walihusika kwenye vurugu za Jumatatu ambao walifikishwa juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Alisema makundi hayo mawili ya wanafunzi wataruhusiwa kuomba upya udahili pindi wakisha kesi zao.

Wanafunzi hao 38 walisomesha shitaka kula njama kufanya vurugu lakini walikana shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Bw. Said Msuya, shitaka ambalo wote walilikana.

Wanafunzi wengine wanne wamefutiwa udahili kabisa baada ya kubainika waliingia darasani na kumfanyia fujo mhadhiri. Wanafunzi hao ni Bw. Stephano Owawa, Bw. David Silinde, Bw. Ally Selleman na Bw. Ally Salum.

Alisema wanafunzi watano waliokamatwa wakivuta bangi nao wamefutiwa udahili na wataruhusiwa kuomba kudahiliwa upya iwapo watashinda kesi zao. Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Godson Emmanuel, Adili Mwang'onda, Batenga Jimson, Joshua Mwanjwango na Soka Eliphance.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Profesa Mukandala kutoa uamuzi wa chuo, Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bw. Deo Daud, alisema hatua hiyo ni ya kibabe kwani uongozi wa chuo hicho ulikuwa na nafasi ya kukaa nao na kuzungumza.
 
Mambo ya kufichana yamepitwa na wakati mtu kama ni Mnazi nitamuita mnazi mpaka kieleweke.Ni kama walivyo kwa mafisadi kama ni fisadi ni fisadi hakuna tasifida hapa.

Matatizo gani wewe unayosema yamepatiwa ufumbuzi??? MAMA acha kuhadaa watu.
statistics toka mwaka 2000 udsm wameshagoma na kusimamishwa zaidi ya mara NNE na wamegoma mfululuzo zaidi ya miaka 3 kutokea leo na ukirudi nyuma.Sasa wewe unasema yamepatiwa ufumbuzi yepi hayo??

.

Hujui hata tatizo moja lililopatiwa suluhisho!hapo unathibitisha jinsi unavyochukulia mambo juu juu. Hebu toa hizo statistics hapa kama unazo. Kila mgomo una chanzo chake. Tumia akili kufikiri. Unadhani watu hawajui kuita hayo majina, na wewe una uhakika gani kama bado hujaitwa jina. Kuheshimu uhuru wa mawazo yako hata kama ni mawazo mgando hupewi jina, however jina lako utajipa mwenyewe kwa vile wewe ni bingwa wa kutoa majina.
 
Sasa jibu umeshapewa na walioacha UNAZI unataka jibu gani tena

Ningefurahi sana hilo tatizo lipatiwe ufumbuzi ,haraka uwezekanavyo.
Nawakulipatia ufumbuzi wa uhakika ni wote waliopita udsm na wakaucha UNAZI na kufuata misingi ya haki na kweli.

Na kutambua kukosolewa ni moja ya taratibu ktk maisha ya mpenda haki na kweli Na maamuzi yote yanafuate misingi ya ubinadamu.
 
Ningefurahi sana hilo tatizo lipatiwe ufumbuzi ,haraka uwezekanavyo.
Nawakulipatia ufumbuzi wa uhakika ni wote waliopita udsm na wakaucha UNAZI na kufuata misingi ya haki na kweli.

Lipatiwe ufumbuzi na nani uliyemwajiri kutoa ufumbuzi ili kukufurahisha?acha uvivu wa mawazo amka hapo ulipo ukatafute ufumbuzi kama sio kutoa ushauri ulionao.
 
Hujui hata tatizo moja lililopatiwa suluhisho!hapo unathibitisha jinsi unavyochukulia mambo juu juu. Hebu toa hizo statistics hapa kama unazo. Kila mgomo una chanzo chake. Tumia akili kufikiri. Unadhani watu hawajui kuita hayo majina, na wewe una uhakika gani kama bado hujaitwa jina. Kuheshimu uhuru wa mawazo yako hata kama ni mawazo mgando hupewi jina, however jina lako utajipa mwenyewe kwa vile wewe ni bingwa wa kutoa majina.


Kuita jina ni moja ya sehemu ya maisha na ndio utaratibu ambao unafanya ID , na kuitwa jina uka act agresivu inaonyesha jinsi gani mtu unakua na elementi ya Kimkandala.

Tatizo silijui ,Na ndio sababu ya kuuliza ,sasa wewe kama unalijua na unashindwa kutoa jibu hii inamanisha yaleyale.

Mimi Hofu yangu na kutumia kufikiri sioni matatizo gani waliyoyapatia majibu Ambayo kila mwaka lazima liibuke jambo jingine Na hata hivyo Mtu anayesolve mambo Kisomi hutafuta jawabu na kuweka kinga ya tatizo jingine linaloweza tokea na wasomi hua wanaliita LONG TERM RESOLUTION .

Sasa kwa kutofikiri kwangu miaka minane mfululizo wanasolve kipi? na hawaangalii yanayoweza tokea kesho na kuyatafutia majibu mpaka yatakapotokea.

Mama wewe naweza kukufananisha na viongozi wetu ambao husubiri njaa itokee ndio wanunue chakula kutoka nje kwa gharama kubwa

huu sio usomi ni usomi mgando kama ulivyosema wewe
 
Lipatiwe ufumbuzi na nani uliyemwajiri kutoa ufumbuzi ili kukufurahisha?acha uvivu wa mawazo amka hapo ulipo ukatafute ufumbuzi kama sio kutoa ushauri ulionao.


Mama mie nadhani wewe ndio uamke hapo ulipo.
Kuna watu tumewaajiri pale udsm kwa shughuri hiyo na tunawalipa mafedha kwa ajiri hiyo na ndio maana nikawaarika wan udsm

Kama na wewe ni mmoja wao pale udsm basi tambue nimekuajiri ili utoe ufumbuzi wa matatizo kama hayo

Na kama hutambui hilo kama kuna watu nimewaajiri kwa kodi yangu basi wewe ni mmoja wa watu wnaodidimiza uchumi wetu
 
Usinifanishe kabisa and on top of that you wont take my dignity, hujui hata maana ya kuita majina asiyejua maana haambiwi maana, kaa hivyo hivyo kalaghabaho. Sina muda wa kukupa jibu maana huelewi king'ang'anizi we. Ufisadi unazidi nchi hii kwa watu wenye akili mnato na ambao ubongo wao uko machoni kama vile wewe. Unataka watu wakupe suluhisho badala ya kulitafuta suluhisho, we wa kutafuniwa. Mtafute Mukandala umuulize tatizo ni nini na mdiscuss suluhisho.
 
Mama mie nadhani wewe ndio uamke hapo ulipo.
Kuna watu tumewaajiri pale udsm kwa shughuri hiyo na tunawalipa mafedha kwa ajiri hiyo na ndio maana nikawaarika wan udsm

Kama na wewe ni mmoja wao pale udsm basi tambue nimekuajiri ili utoe ufumbuzi wa matatizo kama hayo

Na kama hutambui hilo kama kuna watu nimewaajiri kwa kodi yangu basi wewe ni mmoja wa watu wnaodidimiza uchumi wetu

sasa mumewaajiri kwa nini uswaulize hao chanzo cha tatizo. Kabla ya kuuliza tatizo ni nini nenda kawawekee dhamana wale wanafunzi wenye kesi na pia uwawekee wakili. Baada ya hapo nenda chuo ukauulize uongozi tatizo hasa ni nini. Kumbe na wewe fisadi, maana waliojiri wafanyakazi pale chuo ni mafisadi na mamluki wa chama tawala. Kuanzia sasa sitaki kujibizana na wewe fisadi mkubwa umenipotezea muda. Sasa itabidi nikuulize fisadi wewe, tatizo la UDSM ni nini hasa. Maana ufisadi wako ndio unasababisha wanafunzi wanagoma kila mwaka. Wewe ndio unaodidimiza uchumi kwa kuwa wewe ni fisadi na huna ujualo bali kufuata mkumbo.
 
Acha matusi hii ndio demokrasia ,usidhani mawazo yako ndio yako sahihi


Sijasema mawazo yangu ni sahihi, please get into context. wewe kuwaita wenzio majina ndio waona sahihi sio? na hili ndio ninaloliongelea hapa
 
Badala ya kuwasaidia watoto mnatukanana jaribuni kutumia busara zaidi na kutoa mawazo ya kumaliza matatizo ya watoto wa mlimani na sio kutoleana lugha za matusi wenyewe.
 

Kwa wale wanaodhani migomo na maandamano katika vyuo vikuu ni kwetu tu hebu someni hapa:

1) Wanafunzi wa vyuo vikuu ndiyo waliongoza maandamao,migomo na harakati nyingine kupinga vita vya Vietnam. Katika hawa mmojawapo mashuhuri ni Bw. William Jefferson Clinton.

http://en.wikipedia.org/wiki/Opposition_to_the_Vietnam_War

Kuna wanafunzi walipoteza maisha yao pale Kent State mwaka 1970 katika harakati hizi ( walikuwa wanapinga uvamizi wa Cambodia).

http://en.wikipedia.org/wiki/Kent_State_shootings

Na tusisahau kuwa ni wanafunzi hao hao waliokuwa mbele katika kudai haki sawa na kwa watu weusi. Ni wanafunzi hao hao walioshinikiza vyuo vyao kujitoa katika kuwekeza katika mashirika yanayofanya biashara na serikali ya makaburu wa Afrika ya Kusini. Hii ilichangia kwa kiasi kikubwa juhudi za kuutenga utawala huo dhalimu na hatimaye kudondoka. Na ikumbukwe wanafunzi hao walifanya hivi katika miaka ya 60, maarufu kwa movement ya maHippy wakiweka mbele upendo, amani na utumiaji wa madawa ya kulevya! Jamii iliwaona wahuni tuu lakini ni peke yao waliokuwa tayari kutetea haki ya wanyonge.

2. Nchini ufaransa vyuo vikuu vililipuka mwaka 1968 kupinga utawala wa De Gaulle waliyemwona anawafanya kama watoto wadogo. Inaaminika kuwa huu ndiyo ulichangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko katika jamii ya kifaransa kuwa more liberal na tolerant.

http://en.wikipedia.org/wiki/May_1968

hawa waliungwa mkono na wafanyakazi.

Mwaka 2006, wanafunzi wakifaransa waliingia tena mitaani kupambana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyokuwa yanapendekezwa na serikali.

http://www.spiegel.de/international/spiegel/0,1518,406865,00.html

3. Wanafunzi wa vyuo vikuu Korea ya kusini wamekuwa kila kukicha wanapambana na serikali yao dhidi ya hali ya kisiasa katika yyao na Korea ya kaskazini pamoja na mengineyo.

Ninachotaka kusema ni kuwa Chuo Kikuu ni mahali pa mapambano ya kifikra. Ukiangalia tena kuwa wengi wanaokuwepo hapo ni wa umri ambapo wanaamini kuwa wanaweza kufanya lolote na watu wazima magoigoi tu na sell-outs to the system( wengi tumepitia hapa) panahitaji busara kubwa kuhakikisha kuwa hizi eneji zao haziwi destructive. Busara hii si katika kuwa confontational maana watajibu mapigo. Busara ni katika kuwapa nafasi kuelezea kinachowakera, na kuwaheshimu kama watu wazima wengine. Hii inajumuisha vile vile kuweka mipaka ambayo itaheshimiwa na kila mwana jumuia ( mwanafunzi na mkufunzi),k.m. masuala ya unyanyasaji wa kijinsia( mzee panch na wenziwe). Ulaya, Marekani baada ya vurugu za miaka ya sitini wametambua hili, ndiyo maana hausikii migomo ya mara kwa mara. Sisi, kwa bahati mbaya, bado tumejikita katika mtazamo wa miaka sitini, kudai heshima kwa nguvu. hata kwa mtoto wako ukifanya hivi hautafika mbali. Sembuse wa mwingine!

Nadhani wanafunzi wa uhandisi wamekuwa mstari wa mbele kwa hili kwa sababu kuna wakati ni wao tu na wakina mama waliokuwa makiingia chuoni moja kwa moja kutoka JKT (Musoma Resolution). Hao wengine walibidi wafanye kazi kwa miaka miwili kabla ya kuingia chuoni hivyo walijikuta washaonja system. Wahandisi walikuwa bado naive wakiamini bado kuwa wanaweza kupambana na system. Wengine walikuwa na toom much to loose. hii pengine imeendelea mpaka leo. I however stand to be corrected maana hizi ni speculations tu maana sijawahi kupitia hapo UDSM!
 
Nakuunga mkonmo fundi, BUSARA ndio kitu kikubwa kinachopaswa kutawala kwa kila pande, JAZBA na kulazimisha zitatufikisha pabaya, tulishakosea huko nyuma si vema tuendelee kukosea
 
Your talking something irrelevant to the point. What is the correlation between UDSM student strike with Mikataba fake? Please let not politicized something important kama Mlimani. I have respect to that college, but the students are untouchable.Have you ever attended UDSM? Higher learning institutions needs to stay away from politics as much as possible. Ndio maana utaona Colombia University wameweza kumuhoji Ahmadinajad.

Unajichanganya sana wewe. Huwezi kusema kuwa vyuo vikae mbali na siasa na wakati huo huo ukasema kuwa Columbia university walimwalika raisi wa Irani. Kumwalika raisi wa Irani ilikuwa ni siasa tayari.

Kuwatumia wanafunzi kama source za solution za matatizo ya serikali i think ni unfair. Remember kama hujawai kupita Mlimani then you don't have idea about diversity community ndani ya mlimani. Kuna watu wanatoka kwenye familia duni, wamekuja pale kuearn degree so they could support their families. Sasa unapoanzisha mgomo unacost the whole system.

Unatumia sana maneno haya kuwa kama hujapitia mlimani, kumbe wewe umepitia mlimani na unaandika kingereza kibovu namna hii? Unaabisha hicho chuo na afadhali usingesema kuwa umesoma mlimani maana post zako nyingi unatumia english mbofu kabisa. Kama huwezi english si utumie tu kiswahili?

please naomba tusishabikie vitu tusivyo na idea navyo. Kama umepita mlimani then you will understand the effect za migomo. Majority ya hawa waanzisha migomo wapo pale kupoteza muda.

Wewe hujui ni kwanini wao walianzisha huo mgomo kwa hiyo huna sababu ya kuzuia wengine kujadili hapa.
 
wamegoma kwasababu, demokrasia ya wao kuchagua viongozi wa serikali ya wanafunzi wawatakao imepindishwa, wamegoma kwasababu tatizo la maji limekuwa sugu, wamegoma kwasababu umeme unakatika hovyo, lift hazifanyi kazi....mgomo huu ni halali! kama unadhani kukosa calculator ni jambo dogo, basi lazima una matatizo na wanaozihitaji ni wale ambao hawapo pale kwa degree ya history, otherwise maisha ni magumu sana kwa sayansi students bila calculator.

hayo mambo ya pombe, bangi na ngono ni vitu vya kawaida vyuoni dunia nzima! sasa kama hujafanya hayo(kwa walioamua kufanya) wakati ukiwa chuo, watayafanya hayo wakiwa wapi?? ile baa ya wanafunzi ipo kwa ajili ya nani? au ni urembo tu? argument nyingine hapa ni za kilevi kushinda hao wanafunzi mnaowaita walevi!! tuwe wakweli jamani......

Asante sana kwa kukumbusha hili maana naona wengine wanataka kusahau kuwa ufisadi huanza kidogokidogo kwa kuingilia chaguzi za wanafunzi na kisha unaamua kuingilia chaguzi za kitaifa.
 
Back
Top Bottom