Serikali yatetea mkataba wake na Tanzanite One, wabunge waupinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yatetea mkataba wake na Tanzanite One, wabunge waupinga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 31, 2008.

  1. BAK

    BAK JF-Expert Member

    #1
    Oct 31, 2008
    Joined: Feb 11, 2007
    Messages: 70,609
    Likes Received: 82,187
    Trophy Points: 280
    Date::10/30/2008
    Serikali yatetea mkataba wake na Tanzanite One, wabunge waupinga
    Na Daniel Mjema, Dodoma
    Mwananchi

    SERIKALI imesema madini ya Tanzanite hayawezi kuisha ifikapo 2012 hivyo hakuna sababu ya kufuta mikataba ya uwekezaji na na kampuni ya Tanzanite One inayochimba madini hayo huko Mererani kwa kuhofia kumalizika kwa madini hayo adimu duniani.

    Msimamo huo wa Serikali ulitolewa Bungeni juzi na waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja wakati akijibu michango ya wabunge waliotoa ushauri wao juu ya taarifa ya kamati ya Rais ya kuishauri Serikali kuhusu usimamizi wa Sekta ya madini.

    Kauli hiyo ya Waziri Ngeleja kuhusu kutovunjwa kwa mkataba huo ilionekana kujibu zaidi mchango wa Mbunge wa Same Mashariki,Anna Kilango Malecella aliyetaka Serikali ivunje mkataba na kampuni hiyo hata kabla ya kufikia mwaka 2012.

    Kilango ambaye ni mmoja wa Wabunge wanaozungumza kwa hisia kali alisema wachimbaji wadogo wanao uwezo wa kuchimba madini ya vito kwa kutumia mitambo midogo ikiwamo Tanzanite.

    “Nimefanya utafiti wangu na kugundua kuwa leseni yao (Tanzanite One) inamalizika mwaka 2012 mimi naona huko ni mbali ukilinganisha na hasara tutakayopata tusitishe leseni yao sasa”alisema Kilango.

    Kilango alisema uchimbaji wa madini ya vito kwa kutumia mitambo mikubwa sio endelevu na kuonya kuwa kiasi cha madini kinachochimbwa na kuhifadhiwa Afrika Kusini ni kikubwa huku Tanzania ikiachiwa mashimo.

    Alionya kwa vile kampuni hiyo sasa inafahamu uchimbaji wa madini ya Vito utafanywa na Watanzania kwa asilimia 100 wanaweza kuchimba kwa nguvu ili kufikia 2012 madini ya Tanzanite yawe yamekwisha.

    “siku zote kutoa maamuzi magumu ndio kuendelea na huu ni uamuzi mgumu lakini tumwambie Rais kuwa sisi Wabunge tunamuunga mkono na tuko tayari kuchangia fidia kusitisha mkataba huu”alisema.

    Hata hivyo akijibu michango ya Wabunge, Ngeleja upo muda wa kutosha kurekebisha kasoro zilizojitokeza na kusema hakuna sababu kwa sasa kuwanyang’anya wawekezaji hao migodi.

    “hatuwezi kuwanyang’anya bado hatujafika huko kwa sababu tumeingia nao mikataba tukawapa na leseni…hatujachelewa tutarekebisha hizo dosari’alisema Ngeleja.

    Waziri huyo alisema serikali itaifanyia kazi michango na ushauri wote uliotolewa na Serikali ikiwamo kufanya uchunguzi wa namna ilivyouza hisa zake kama ilivyopendekezwa na kamati ya kudumu ya Bunge la Madini na Nishati pamoja na Wabunge.

    Alisema serikali inakubaliana na mapendekezo ya wabunge ya kutaka madini ya vito yasafishwe hapa nchini na kutoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuungana kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya aina hiyo vitakavyotoa ajira kwa watanzania.

    Wakati akichangia ripoti hiyo juzi jioni, Mbunge wa Kwela,Chrisant Mzindakaya(CCM) maarufu kama mzee wa mabomu jana aliipasha serikali kwa kuwakumbatia wawekezaji na kuwafanya kama Mungu wa duniani.

    Mzindakaya alisema Tanzania inapaswa kuiga mfano wan chi ya Botswana ambayo imekuwa ikimiliki migodi nusu kwa nusu kati ya Serikali na makampuni yanayohitaji kuwekeza katika sekta hiyo.

    “Serikali isiogope kumiliki utajiri tulionao kwanini tunataka kila kitu raw material(malighafi)…madini tunauza ghafi,kahawa tunauza ghafi kila kitu tunauza ghafi huu ni ugonjwa mbaya sana”alisema.

    Mbunge huyo alitaka Shirika la madini nchini(STAMICO) liwezeshwe kusimamia uchimbaji madini na kusema Tanzania ina wataalamu wazuri wa madini bali kinachogomba ni vifaa.

    Mzindakaya alisema madini sio bidhaa inayoharibika hivyo hakuna haraka ya kutafuta wawekezaji kabla ya kuwa na mazingira yanayoiwezesha nchi kunufaika na rasilimali zake.

    “Botswana wao wanamiliki 50-50, na wanachokifanya ni kwamba wakishaingia mkataba wa namna hii wanakwenda kukopa Benki na hapo sasa ndio unaajiri wataalamu”alisema Mzindakaya.

    Kwa mujibu wa Mzindakaya,Tanzania ingeweza kuiga mfano huo na kumiliki migodi hii kwa ubia wa nusu kwa nusu badala ya kuwaachia wageni wamiliki migodi hiyo kwa asilimia 100.

    Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene(CCM) alisema watanzania wa leo hawajatofautiana na wale wa kabla ya uhuru ambao waliletewa shanga na wazungu na wao kutoa almasi.

    Alisema hivi sasa Watanzania wanadanganywa na Serikali kuwa imeamua kutafuta wawekezaji kwa sababu haifanyi biashara na kusema serikali zote duniani zinafanya biashara na kutoa mfano wa Dubai ambako Taxi zote zinamilikiwa na Serikali.

    “Hivi hii imani kwamba Serikali haifanyi biashara tunadanganywa na nani?...Tufike mahali Serikali yetu ikiri kuwa ilikosea halafu turudi nyuma kumiliki rasilimali zetu”alisisitiza.
     
  2. T

    Tom JF-Expert Member

    #2
    Oct 31, 2008
    Joined: May 14, 2007
    Messages: 472
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Botwana kupata fifty fifty ni uwezo wao wa kujadili kwa ufundi mkubwa mikataba na ni kigezo kuwa nasi tunaweza pata hiyo fifty na hata zaidi endapo tutaongeza uwezo wetu wa kujadiliana mikataba.
    Kuzira na kuacha madini ardhini nalo si jibu, serikali ya Chama Cha Mzindakaya -CCM wametawala miaka yote na waliayaacha hayo madini pamoja na vitu vingine (ardhi, mifugo, misitu, uvuvi nk)kwa muda mrefu sana bila kuendeleleza. Matokeo yake ni papara na kuishia na mikataba ya kupatiwa 3%. Mzindakaya anashindwa kuelewa kua IMF na WB si vyombo vya kiroho na waliishauri serikali kutofanya biashara kwa sababu tayari serikali ilikuwa imeshashindwa kufanya biashara. Chini ya serikali labda hata hayo mapato ya 3% tisingepata.
    Matunda ya serikali ya Dubai kufanya biashara si sawa na serikali ya Tanzanian kufanya biashara, kwani viwango vya uwajibikaji havipo sawa. Nijuavyo, serikali ya CCM haina kawaida ya uwajibikaji wa matendo yake.
    Kwa vyovyote vile wawekezaji ni muhimu na ni shule nzuri tu kwetu. Ni muhimu kula nao sahani moja. Matatizo makubwa ya wachimbaji wetu si vifaa bali maarifa na mbinu hafifu za kiuwekezaji, uchimbaji, utayarishaji, uuzaji, kukua kwa kampuni nk. Yote hayo tuna nafasi nzuri kujifunza toka kwa wawekezaji. Serikali ina wajibu wa kuwasaidia na kuwainua wachimbaji wetu ili waweze baadaye kushindana bega kwa bega ama kuwa joint venture na hao wawekezaji. Lazima tujifunze namna ya kuwatumia vizuri kwa faida yetu.
    Kabla ya kufikiria kuipa serikali umiliki wa makampuni ya kibiashara, Mzindakaya angegombania kuleta utaratibu mzuri wa kuiwajibisha serikali ya chama chake na kupunguza madaraka ya raisi. Mpaka sasa raisi ni fanal ktk mambo karibu yote. Mzindakaya atapayuka weeee, lakini raisi ana veto zote. Hata bunge asemeako, likileta ubishi, raisi ana nguvu ya kulivunja.
     
  3. w

    wajinga Senior Member

    #3
    Oct 31, 2008
    Joined: Jun 25, 2008
    Messages: 148
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Botswana mikataba yao ilifanywa miaka zaidi ya 40 iliyopita. Wakati huo ilikuwa na wasomi wananchi wasiozidi 50. Lakini walifanya kazi nzuri sana na walipenda nchi yao hawakuangalia mifuko yao. hapa tanzania inawezakana not in a million years.
     
  4. M

    Morani75 JF-Expert Member

    #4
    Oct 31, 2008
    Joined: Mar 1, 2007
    Messages: 619
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 0
    Wakuu, tatizo la Tz sio usomi..... ni njaa na ukiritimba wa kimawazo!! Jamani kuna makosa ambayo watu/wahusika wamekuwa wanayafanya ambapo mtu wa kawaida tu ukisoma/ukiona unajua kabisa kwamba ni madudu lakini watu wanapeta!!!!

    Mkuu wajin...., unajua mabadiliko yaliyotokea katika kipindi cha chini ya miaka miwili (especially after 2007 mwanzoni) ni mengi sana hasa katika swala zima la usiri, uchafu na madudu ya watendaji wetu....Nina imani kuwa ndani ya miaka mingine mitatu (kuweka 5 kamili) mambo yatakuwa mazuri sana au mabaya sana.... Lazima kuwe na extremities na sio otherwise....

    Mungu bariki Tanzania na watu wake!!
     
  5. F

    Fundi Mchundo JF-Expert Member

    #5
    Oct 31, 2008
    Joined: Nov 9, 2007
    Messages: 4,706
    Likes Received: 61
    Trophy Points: 145
    Hao wachimbaji wadogo wanachangia kiasi gani mfuko wa taifa? Si ndio hao ambao wakizipata wazitapanya tu? Si ndio hao ambao wako heri kuzipeleka kwa kupitia njia za panya kwa jirani zetu Kenya? Si ndio hao ambao hawataki kuwekeza katika usalama wa machimbo yao hadi kupelekea maafa yaliyowakuta hivi karibuni? Si ndiyo hao wanaoendekeza imani kuwa viungo vya albino ni dili na vinaweza kukuletea neema? Kuna ajabu gani Tanzanite kuuzwa kwa wingi Afrika Kusini? Mbona kitovu cha biashara ya almasi kiko ubelgiji Antwerp na si Afrika Kusini, Botswana au Namibia?

    Tusifumbie macho maovu na mapungufu ya watu wetu kwa sababu ya uzalendo feki!
     
  6. s

    sheshe New Member

    #6
    Nov 2, 2008
    Joined: Oct 30, 2008
    Messages: 4
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Swala lanjia zapanya ni uzembe serekali,kuusu albino nimesikia kwako, wachimbaji wadogo wanafaida kubwa sana,mzawa akipata madini atajenga,atanunua gari nk,kwaiyo kila atacho nunua serekali itanufaika kupitia vat nk.
     
Loading...