real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Serikali imepanga kukarabati na kuboresha shule 88 za vipaji maalum, waziri wa elimu Profesa Joyce Ndalichako aliyasema hayo siku ya jumanne tarehe 28/06/2016 katika maadhimisho ya siku ya elimu nchini iliyofanyika katika shule ya sekondari Mzumbe iliyopo wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro.
''Tutaanza na shule hii (Mzumbe), Ilboru na Weruweru katika hatua za kurudisha heshima zilizokuwa nazo zamani''
Amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 33 kwa awamu ya kwanza utakaoanza na shule 33
''Tunatarajia kufanya maboresho haya katika awamu tatu, pamoja na kuzipa shule hizi walimu wenye vigezo. Tumeongea na washirika wa kimaendeleo kushirikiana nasi na tutaanza wiki ijayo'' aliwaambia wageni waalikwa katika maadhimisho hayo