NW Katimba: Bilioni 6.7 Zimetumika Kuboresha Ujenzi wa Shule za Sekondari 10 Muheza (W), Tanga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,851
1,310

NW KATIMBA: BILIONI 6.7 ZIMETUMIKA KUBORESHA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI 10 MUHEZA (W), TANGA

Takribani shilingi Bilioni 6.7 zimetumika katika ujenzi wa shule za sekondari 10 katika Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Shule hizo zimejengwa katika kata 10 kati ya 13 za wilaya hiyo ili kusogeza huduma kwa wakazi wa maeneo hayo ambao watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata masomo, hali iliyokuwa inasababisha kupata matokeo mabaya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Zainab Katimba wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mtoto wa Leo Samia wa Kesho inayolenga kuibua vipaji vya watoto na kuwatambua watoto wenye ulemavu katika wilaya ya Muheza.

“Hapo awali kulikuwa na kata 13 ambazo hazikuwa na shule za sekondari lakini alivyoingia madarakani Rais Samia Suluhu Hassan ameshaleta fedha ambazo zimejenga shule za sekondari katika kata 10 na mwaka huu wa bajeti kuna Kata nyingine ya Kwezitu ambayo na yenyewe imeletewa Milioni 580 kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari. Tafsiri yake zimebaki kata mbili tu" - Naibu Waziri Katimba

Naibu Waziri Katimba Amesema Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa walimu, ya kuwajenga uwezo na kujenga nyumba za kuishi ili waweze kufanya kazi kwa bidii na ubunufu katika sekta ya elimu.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-10-01 at 15.36.20.mp4
    25.8 MB
  • GYyuHqEWUAIYIjJ.jpg
    GYyuHqEWUAIYIjJ.jpg
    177.2 KB · Views: 6
  • GYyuHqCXAAIpDAL.jpg
    GYyuHqCXAAIpDAL.jpg
    354.6 KB · Views: 7
  • GYyuHqPW8AAW7f-.jpg
    GYyuHqPW8AAW7f-.jpg
    381.5 KB · Views: 5
  • GYyuHqOWcAEAcEL.jpg
    GYyuHqOWcAEAcEL.jpg
    304.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom