Serikali yasisitiza wasanii kujisajili BASATA

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Imesema endapo msanii yeyote atabainika anajihusisha na shughuli hizo bila kuwa na usajili, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa kongamano la Fursa kwa Wasanii wa Wilaya ya Siha lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa RC Siha.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali la Tagoane na kuwashirikisha zaidi ya wasanii 400 likiwa na kauli mbiu ya "Kipaji Changu Fahari Yangu".

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji huyo, Ofisa Michezo Mkoa wa Arusha Benson Maneno, alisema Basata halitavumilia kwa namna yoyote kuona mkuzaji sanaa (Promota) akitumia wasanii wasiosajiliwa na kuwa na vibali kutoka baraza hilo.

Alisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi namba 23 ya mwaka 1984 inayoelekeza usajili na utoaji vibali kwa wadau wote wa sanaa.

"Serikali inasisitiza kuhusu kujisajili wasanii na imekuwa ikipita kila maeneo ya kanda na mikoa kuwahamasisha wasanii kujisajili, hivyo kupitia kongamano hili tunapenda kuwahamasisha wasanii wote wa mkoa wa Kilimanjaro kujisajili kupitia Basata,” alisema Maneno.

Aidha, Basata imewaagiza mapromota wote wanaoendesha matukio ya sanaa kama vile matamasha, mashindano, maonyesho na utoaji tuzo nchini, kuhakikisha wanafanya kazi na wasanii waliosajiliwa na wenye vibali vya Basata na si vinginevyo.

"Rai yangu kwenu wasanii hakikisheni mnakwenda kujisajili Basata. Ukimaliza huko unakwenda Cosota (Chama cha Hakimiliki Tanzania) hao watakupa hatimiliki ya kufanya kazi yako, ambayo itatambuliwa kisheria," alisema.

Awali, Rais wa Tagoane, Dk. Godwin Maimu, alisema kongamano hilo la vijana wasanii kutoka Wilaya ya Siha limelenga kuibua vipaji kwa vijana hao vilivyokuwa havionekani kwa kuwa kuna wasanii wengi waliokuwa hawatambuliki, lakini kupitia kongamano hilo, wataibuliwa na kung’ara.

Dk. Maimu aliwataka wasanii kuendelea kuwa kioo kwa jamii kwa kutunga nyimbo zenye maadili ya taifa, nyimbo zenye kuhamasisha upendo, amani kwa nchi na vivutio vilivyoko katika wilaya husika, ili kuvitangaza kupitia sanaa hiyo.

Naye Mkufunzi wa Ubunifu kwa Vijana, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Dk. Eliamani Laltaika, aliwataka wasanii kuanzisha miradi ya kiuchumi ambayo itawawezesha kujikwamua na lindi la umaskini, huku akiwataka kuwa wabunifu katika kazi zao wanazozifanya za sanaa.

"Kumekuwapo na malalamiko mengi kwa vijana kuhusu kazi zao kudurufiwa na hazilindwi kisheria sababu ni kwamba wao wenyewe hawaifahamu sheria, hivyo niwaombe kujisajili ili kazi zao wanazozizalisha ziweze kulindwa kisheria," alisema Laltaika.

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu, aliwataka wasanii kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa zinasababisha akili ya msanii kutokufanya vizuri, hivyo kufanya muunganiko wa akili ya ujuzi, maarifa na ubunifu kupotea.

Buswelu alisema baadhi ya wasanii wamekuwa wakishiriki kutumia dawa za kulevya na wengine hata kutumiwa kama wasafirishaji kutoka nchi moja kwenda nyingine na wengine wamekuwa wakipoteza kabisa hata uwezo wa kufanya kazi zao za sanaa kutokana na matumizi hayo ya dawa za kulevya.


1578042832350.png

CHANZO: IPP Media
 
Msanii ni nani!?
hata hawa wa kufinyanga vyungu!!?
na kuchonga vinyago.....
ama ni mziki tu.....?
 
Back
Top Bottom