Serikali yashindwa kuwalipa wastaafu wake

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Katika hali isiyokuwa ya kawaida serikali imeshindwa kuwalipa wastahafu wake nauli za mizigo na likizo ya mwisho.

Inashangaza zaidi kwa vile hela yenyewe sio nyingi kiasi hicho.Wizara ambayo tuna hakika inahusika ni ya Kilimo kitengo cha Utafiti.

Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu hakuna majibu yanayoeleweka isipokuwa tunaambiwa kwamba serikali haijatoa fedha.

Kinachoshangaza ni kwamba financial year nzima imeshapita sasa na hii tuliyonayo ni ya pili,na wahusika wanasema kwamba hawadhani tutalipwa.

Ni vigumu kuwaza mambo haya,sasa nini kinaendelea,sio haki yetu?Very difficult to comprehend.Tunashindwa kuelewa tufanye nini ili tupate haki yetu.

Hii ni kinyume kabisa na haki za binadamu.Wakati mwingine inashangaza sana,Hawa wanaotufanyia hivi nao watastahafu,sasa sijui wanasahau kwamba unachomfanyia mwenzio na wewe utafanyiwa hicho hicho.

Anae ua kwa upanga na yyeye atauwawa kwa upanga.Frankly sikujua kwamba nchi yetu imefika kwenye kiwango cha juu cha dhuluma namna hii,kudhulumu hata wazee,ni sibu sana.
 
Kuna watumishi wengi wamefariki katika wizara mbalimbali lakini serikali imeshindwa kusafirisha familia zao kwenda makwao! Huu ni unyanyasaji uliopitiliza na hasa ukizingatia viongozi wa serikali wanavyotumbua fedha za umma bila huruma!!

Serikali hii ni laana tupu!!
 
Back
Top Bottom