Serikali yashindwa kulipa wafanyakazi, yapunguza maslahi kimyakimya

Mimi ni miongoni mwao so ujumbe umefika Mkuu. Inawezekana Kikwete ndio kiongozi wa hayo uliyoyataja hapo juu
 

mara unasema hakuna malipo mara yamepunguzwa mbona unachanganya? zibandike hizo standing order tuzione wakati mwingine ni tafsili tu inakuwa si sahihi.
pamoja na mapungufu ya serikali lakini suala la kupunguza mshahara wa mfanyakazi hilo halipo, sanasana ni makosa kiuandishi ya hao ma Human Resource Officers, nakkumbuka hata miaka michache iliyopita kulikuwa na kituko cha namna hiyo ila wahusika walilalamika wakabadilishiwa.
Otherwise mwezi huu pesa inamaliziwa kabla ya kuanza mwaka mpya wa bajeti.
naona ulikuwa na nia ya ku justify mawazo ya wachambuzi wa mambo
 
Pesa wanajilipa wenyewe kupitia Dowans, na mafisadi kama RA, EL, Chenge, Mkapa et al sasa ni lazima wafyeke mishahara ili zitoshe na yeye ndio msimu wake wa mwisho hivyo ni lazima akombe hazina yote ya taifa m k w e r e huyo. Si umesikia hata TRA wameshindwa kukusanya mapato wamewapa mafisadi.
 
km hilo lipo limetokea kimakosa,wasiliana na ofisi ya utumishi kwa hilo la mishahara kushushwa,maana hiyo ni kashfa nzito!kuhusu mizigo kuna ukweli!
 
Mleta hoja katoa alikopata habari:

Gazeti la Serikali Namba 10 vol. 92 la 11/3/2011 na Government Notice (GN) 104 ya 11/03/2011. Wenye uwezo msome kabla hamjasema anadanganya.

Wafanyakazi walikuwa na nafasi nzuri ya kunyosha mapito ya nchi mwaka jana, lakini walirubuniwa kwa temporary salary increment. Inawezekana kuna kuvuna tulichopanda, ila nadhani mambo ni bado kabisa!

Sasa JK afanyeje? Slaa kamnyoshea kidole asithubutu kupandisha kodi za mafuta, sukari, vifaa vya ujenzi. Sasa fedha za kuchota wakubwa na kuwabakizia nyie zitatoka wapi? Something must give.
 
Mbona sijawahi kusikia mshahara unashuswa tangu enzi za TANU, Sasa basi lowasa arudi serikalini.:A S 103:

Mkuu nijuavyo mimi mshahara wa mtu hauwezi kushushwa. Nadhani ndio taratibu hizo hata kama utashushwa cheo ukaenda kada ya chini lakini ulikuwa na mshahara mkubwa basi utabaki nao na utakuwa personal to yourself.
 

nchi imemshnda huyu baba c ajiengue na wafanyakazi wamekaa kimya amkeni daini chenu mapema
 
maafisa waandamizi(wakubwa)wanalipwa utilities(umeme na maji)385,000/= hadi 460,000/= kwa mwezi,housing allowance ni 600,000/= hii ni flat kwa wote kuanzia kwa waziri hadi katibu tawala wa wilaya,..yaani hayo marupurupu yanazidi mshahara wa kuanzia wa any graduate serikalini tena basic salary sio net...we will get there someday,.i believe...
 
Na kwa kuongezea Mwaka ujao wa fedha hakuna kupanda vyeo wala ajira mpya isipokuwa kwa kada za Ualimu,Afya na Kilimo
 
Gazeti la Serikali Namba 10 vol. 92 la 11/3/2011 na Government Notice (GN) 104 ya 11/03/2011

hayapo kwenye website ya Utumishi
 
Gazeti la Serikali Namba 10 vol. 92 la 11/3/2011 na Government Notice (GN) 104 ya 11/03/2011

ya namba na tarehe hiyo hayapo kuna mengine tu, nimejaribu hata kusearch hayapo; kama unayo nakala basi naomba uscan na kutuwekea hapa kama huna usijali hata sisi tutaendelea kuisaka huku makazini kwetu, tukipata tutawajulisha wanajamvi.
 
sina hakika na hili,na kama ni kweli basi tunarudi kulekule kwa MH mbunge Zito kuwa Serikali imefilisika na sasa inatafuta mbinu ya kujiweka sawa

Lakini pia haiwezi kushusha mshahara kwa kiwango cha (425,290/=) hadi TGHS (260,400/=) hiyo haiwezekani,kwani Serikali inatambuwa mfumuko wa bei uliopo na kupanda kwa maisha

kama ni kweli wafanyakazi wa Tanzania si wajinga hawatakubali hilo hata serikali inalijuwa hilo,mwisho wa siku ni kuwa na mgomo usio kuwa na kikomo

eeee mungu tuondolee kikombe hiki cha adhabu,Madhahabu yote tuliyonayo na Matanzanite lakini bado nchi inahangaika kama mtoto yatima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…