Serikali yashindwa kulipa wafanyakazi, yapunguza maslahi kimyakimya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yashindwa kulipa wafanyakazi, yapunguza maslahi kimyakimya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ADVOCATE NEWBOL, Jun 2, 2011.

 1. A

  ADVOCATE NEWBOL Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa ni dhahiri, KIKWETE nchi imemshinda. Serikali yake imeshindwa kulipa watumishi stahili zao. Mishahara yashushwa, posho zapukutishwa na hakuna malipo kwa wafanyakazi wapya wanaoanza kazi. Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing Orders) zafanyiwa marekebisho.

  Kwa mujibu wa Gazeti la Serikali Namba 10 vol. 92 la 11/3/2011 na Government Notice (GN) 104 ya 11/03/2011, Standing Orders za 2009 zimefanyiwa marekebisho ambapo pamoja na mambo mengine sasa mtumishi wa serikali anayeanza kazi HATALIPWA gharama za kuhamisha mizigo yake na posho yake ya kujikimu sasa itakuwa ni kwa siku saba (7) badala ya 14 kama ilivyokuwa kabla ya marekebisho hayo (tazama kif. L.6 na jedwali J/I kolamu ya [vi] na GN 104 ya 11/3/2011). Ikumbukwe kuwa ni mwaka jana tu yaani kuanzia Julai 1, 2010 ndipo (bila shaka ili kupata kura za wafanyakazi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge 2010) Serikali ilipopandisha viwango vya posho kwa watumishi wapya na wale wanaohamia vituo vipya. Kabla ya Julai 1, 2010 mtumishi alipokuwa akihama alikuwa analipwa TSh 1,000/= kwa tani-km x tani 3 [kwa maafisa] (au tani 1.5 kwa watumishi wa kada ya chini) x km y (umbali kwenda kituo kipya); na posho ya kujikimu kwa mujibu wa stahili yake (siku 14 kwa kuhama na siku 7 kwa watumishi wapya). Lakini Serikali kuanzia Julai 1, 2010 ilipandisha pesa hizo kwa kuongeza tani kuwa 5 kwa maafisa na tani 3 kwa hao wengine (tazama Standing Orders za 2009 zilizoanza kutumia Julai 1, 2010) na posho ya kujikimu kuwa ya siku 14 kwa wote yaani watumishi wapya na wale wanaohamia vituo vipya vya kazi.

  Kama hilo halitoshi Serikali tena imeshusha mishahara ya watumishi wa kada mbali2 ikiwa ni pamoja na kada ya afya kimya2 bila kutangazia umma kwa kuunganisha MADARAJA ya mishahara ambapo daraja la juu linateremshwa na kuunganishwa na daraja la chini yake. Kwa mfano kwa watumishi wa afya waliokuwa ktk ngazi ya mshahara TGHS B.1 (425,290/=) sasa wamerundikwa ktk TGHS A. 1 (260,400/=): haya ni maangamizi. Wafanyakazi mko wapi? Na viongozi wa wafanyakazi je, na nyie mko wapi? Nicolas Mgaya uko wapi? Ninamkumbuka mpanganaji marehemu RWEGASIRA wa TRAWU ... Cha ajabu ni kuwa wafanyakazi wa chini ndio wanaoguswa na makato haya. Wakubwa kama vile Wabunge, Mawaziri nk wanazidi kurundikiwa mihela tena pasipo kufanya kazi ya maana.

  Wachambuzi wa mambo wanabaini kuwa haya ni matokeo dhahiri ya KIKWETE kushindwa kuongoza nchi na kwamba hajui la kufanya ili kuikwamua nchi kutoka hapa ilipo. Tungoje tuone, bila shaka kuna mengine mengi.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  na bado wanakatwa PAYE?!!!!!!!!!!!!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  na wala huwasikii wakilalamika??? nchii hii!!!!!!!!!!! kazi ipo
   
 4. fige

  fige JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Na siyo PAYE peke yake wanalazimishwa kuchukulia fedha benki ambako kuna charges kibao .
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  He he he, hatulalamiki kwakuwa tunaogopa kuitwa mbayuwayu!!
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hebu nielekeze vizuri.
  Kwa ngazi ya watumishi wa kada ya chini ni 3tonne * Tshs 1,000.00 * distance badala ya 1.5tonne *Tshs 150.00* distance & watumishi wa kada ya juu ni 5tonne * Tshs 1,000.00 * distance badala ya 3tonne *Tshs 150.00* distance ambapo kwa ushahidi ni kuwa baadhi ya wizara bado wanatumia rates za zamani kama 3tonne kwa watumishi wa kada ya juu na 1.5tonne kwa watumishi wa kada ya chini. Je hili libakije?

  Pia ufafanui hapa "Kama hilo halitoshi Serikali tena imeshusha mishahara ya watumishi wa kada mbali2 ikiwa ni pamoja na kada ya afya kimya2 bila kutangazia umma kwa kuunganisha MADARAJA ya mishahara ambapo daraja la juu linateremshwa na kuunganishwa na daraja la chini yake. Kwa mfano kwa watumishi wa afya waliokuwa ktk ngazi ya mshahara TGHS B.1 (425,290/=) sasa wamerundikwa ktk TGHS A. 1 (260,400/=):" hivi kweli hili linawezekana kumshusha mtu mshahara bila kumshusha cheo au kumpa notice ya yeye kushushwa mshahara?
   
 7. k

  kiloni JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa mara ya kwanza toka uhuru mshahara unashushwa!!!
  Na bado; imbeni tena wafanyakazi wat GOT.

  Nambari wani eeh Nambari wani ni ccm; Jamani wafanyakazi tieni tieni kwa moyo mmoja nambari wani ni ccm.
  Imbeni tena kwa sauti au ni mwite mzee wa presha inashuka presha inapanda awafunde?!!
  Cmon you will rip what you sow in october 2010. Mkitetewa CDM wanaleta vurugu. cia0!!!
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Pia naomba unijulishe waraka ulihalalisha malipo ya kutoka tonne tatu kuja tano na 1.5 kuja 3 tonne. Ukiweza niwekee na link ya hiyo Standing Order ni download ili niwe naperezi peruzi kimtindo.
   
 9. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Komeni kulalamika kwani wakati wa uchaguzi mwaka jana mlimpigia kura nani?
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbona sijawahi kusikia mshahara unashuswa tangu enzi za TANU, Sasa basi lowasa arudi serikalini.:A S 103:
   
 11. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Siamini nilichokisoma.Mungu wangu,are we there.Ndio,iko kazi.
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  MM! KUONGOZA NCHI KWELI KAZI!
  Y aani serikali ya JK inaamini inaweza kujiongezea mapato ya maana kwa kuwabana wafanya kazi?
  Ubunifu ziro!
   
 13. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  sitaki kuamini mapema hii habari, na kama itakuwa kweli basi ile rushwa ya nigeria itakuwa ni cha mtoto, jk komaa na msimamo huo huo
   
 14. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hapa siyo ccm wala chadema ni ulafi tu..lini umesikia lema au zito kugoma kuchukua mshahara wa ubunge kwasababu ni mnono mno?wake up tanzanians
   
 15. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hii ni uongo! Acheni kuzusha jamani
   
 16. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kama sio mfanyakazi wa serikali huwezi kuiamini habari hii. To me this is not new. Maafisa Utumishi walikaa Semina Morogoro wakapewa semina Mwezi uliopita kuhusu jambo hili. Msiwe wavivu gazeti la serikali alilotaja mtoa habari na toleo husika linapatika hapa Presidents Office - Public Service Management - Home
   
 17. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Wewe wa wapi bwana? Una ushahidi wote wamelipwa? kabla ya kukurupukia kujibu nenda hapa Presidents Office - Public Service Management - Home tafuta tangazo husika. Muulize Hawa Ghasia kwanini watumishi wapya hawapelekwi orientation kama waraka wa mwaka 2005 unavyotaka? Muulize kwanini hajawalipa watumishi waliojiriwa tangu Agosti mwaka jana pesa zao za kujikimu, mizigo na nauli? Kwanini watu wengine walipanda vyeo tangu mwaka juzi lakini hawajalipwa mpaka leo? Vibaya sana kufikiri kwa kutumia tumbo
   
 18. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hali ya serikali kiuchumi kwa sasa ni mbaya-na naamini itazidi ku-deteriorate kadri siku zinavyokwenda
   
 19. A

  ADVOCATE NEWBOL Member

  #19
  Jun 2, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamii Forum is the home of great thinkers, and thinkers argue, support their arguments with concrete evidence. MOPAOZI sustantiate your claims with evidence. Otherwise, thanks for your comments ... Like you if I were a fool, I would prolong your unreasoned shouts.
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Katika watu waliochangia kuzorota kwa taifa hili kwa asilimia kubwa na ambao wanasababisha serikali ionekane hovyo zaidi ni watumishi wa Umma ambao miongoni mwao zaidi ya nusu ni fake! hawa qualify na hukuwengi wao wakiwa na vyeti vya ndugu na majirani!

  Hawafai hata kulipwa mishara maana sijui wanachofanya, Mkapa alileta mpango wa OPRASS waliogopa sana na kumuomba Kikwete aondoe huo mpango maana walijua wengi wao wamefanya ofisi za serikali kama kijiwe cha kuangalia internet na kunywa kahawa bila tija.

  Ndio kikwete aliwaijia juu na wakanywea hawana confidence wengi ni uzembe na ngono ofisi na kusinzia tu!
   
Loading...