Serikali yashindwa kulipa wafanyakazi, yapunguza maslahi kimyakimya

Sio kama hawajalipwa ila walichelewa kulipa kwa sababu ambazo siye hatuzifahamu labda watuambie ila inasemekana hata mshahara wa mwezi uliopita walikopa crdb ila sina proof na hilo...
 
mbona inakuwa haieleweki? nafika hadi kwenye hiyo Gazette lakini sioni hicho kitu. Naomba mtoa mada utuwekee hiyo article tuisome vizuri.
 
INawezekana na tatizo la mshahara wa Dk Slaa kutolipa kodi imepelekea serikali kufikia namna hii??
 
Wewe ulikuwa unategemea nini chini ya uongozi wa nchi.....unaotegemea waganga na watabiri wa nyota?......na bado!!!!!....Maondiko yanasema amtumainiye mwanadamu na kumfanya kuwa kinga yake amelaaaniwa......full stop.......Sasa wanaoongaza wapo chini ya laaana...unaionaje hii hesabuuu..................... Tafakari chukua hatua....
 
It doesn't surprise me.

Kikwete's mind is on how he, and his henchmen, will benefit from his presidential position. As long as the wafanyakazi are not part of his mtandao, forget about their well-being. He had told them that he did not want their votes, so I wonder if they voted for him.

Sasa ni dhahiri, KIKWETE nchi imemshinda. Serikali yake imeshindwa kulipa watumishi stahili zao. Mishahara yashushwa, posho zapukutishwa na hakuna malipo kwa wafanyakazi wapya wanaoanza kazi. Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing Orders) zafanyiwa marekebisho.

Kwa mujibu wa Gazeti la Serikali Namba 10 vol. 92 la 11/3/2011 na Government Notice (GN) 104 ya 11/03/2011, Standing Orders za 2009 zimefanyiwa marekebisho ambapo pamoja na mambo mengine sasa mtumishi wa serikali anayeanza kazi HATALIPWA gharama za kuhamisha mizigo yake na posho yake ya kujikimu sasa itakuwa ni kwa siku saba (7) badala ya 14 kama ilivyokuwa kabla ya marekebisho hayo (tazama kif. L.6 na jedwali J/I kolamu ya [vi] na GN 104 ya 11/3/2011). Ikumbukwe kuwa ni mwaka jana tu yaani kuanzia Julai 1, 2010 ndipo (bila shaka ili kupata kura za wafanyakazi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge 2010) Serikali ilipopandisha viwango vya posho kwa watumishi wapya na wale wanaohamia vituo vipya. Kabla ya Julai 1, 2010 mtumishi alipokuwa akihama alikuwa analipwa TSh 1,000/= kwa tani-km x tani 3 [kwa maafisa] (au tani 1.5 kwa watumishi wa kada ya chini) x km y (umbali kwenda kituo kipya); na posho ya kujikimu kwa mujibu wa stahili yake (siku 14 kwa kuhama na siku 7 kwa watumishi wapya). Lakini Serikali kuanzia Julai 1, 2010 ilipandisha pesa hizo kwa kuongeza tani kuwa 5 kwa maafisa na tani 3 kwa hao wengine (tazama Standing Orders za 2009 zilizoanza kutumia Julai 1, 2010) na posho ya kujikimu kuwa ya siku 14 kwa wote yaani watumishi wapya na wale wanaohamia vituo vipya vya kazi.

Kama hilo halitoshi Serikali tena imeshusha mishahara ya watumishi wa kada mbali2 ikiwa ni pamoja na kada ya afya kimya2 bila kutangazia umma kwa kuunganisha MADARAJA ya mishahara ambapo daraja la juu linateremshwa na kuunganishwa na daraja la chini yake. Kwa mfano kwa watumishi wa afya waliokuwa ktk ngazi ya mshahara TGHS B.1 (425,290/=) sasa wamerundikwa ktk TGHS A. 1 (260,400/=): haya ni maangamizi. Wafanyakazi mko wapi? Na viongozi wa wafanyakazi je, na nyie mko wapi? Nicolas Mgaya uko wapi? Ninamkumbuka mpanganaji marehemu RWEGASIRA wa TRAWU ... Cha ajabu ni kuwa wafanyakazi wa chini ndio wanaoguswa na makato haya. Wakubwa kama vile Wabunge, Mawaziri nk wanazidi kurundikiwa mihela tena pasipo kufanya kazi ya maana.

Wachambuzi wa mambo wanabaini kuwa haya ni matokeo dhahiri ya KIKWETE kushindwa kuongoza nchi na kwamba hajui la kufanya ili kuikwamua nchi kutoka hapa ilipo. Tungoje tuone, bila shaka kuna mengine mengi.
 
Kwa uelewa wangu finyu najua serikali haiwezi kumshusha mtu mshahara ila kinachofanyika ni kuwa mhusika anabaki nao ila yule anayeajiriwa first time ndo ataanza na huo mpya kama kweli wameshusha. Imeshatokea kwa ngazi ya maafisa tarafa mishahara imeshushwa alikni watumishi husika wamebaki na mishahara yao inayoitwa mishahara binafsi ila wale wapya huanza kwa TGS D. Suala la usafiri hilo no kweli kunamabadilko yamefanyika. Mimi naunga mkono hoja kwa hili ni matumizi mabaya ya rasilimali pesa.
 
Sio kama hawajalipwa ila walichelewa kulipa kwa sababu ambazo siye hatuzifahamu labda watuambie ila inasemekana hata mshahara wa mwezi uliopita walikopa crdb ila sina proof na hilo...
Sijakuelewa Mkuu hawajalipwa nini? Kina nani? Samahani naomba ufafanuzi
 
Kwa uelewa wangu finyu najua serikali haiwezi kumshusha mtu mshahara ila kinachofanyika ni kuwa mhusika anabaki nao ila yule anayeajiriwa first time ndo ataanza na huo mpya kama kweli wameshusha. Imeshatokea kwa ngazi ya maafisa tarafa mishahara imeshushwa alikni watumishi husika wamebaki na mishahara yao inayoitwa mishahara binafsi ila wale wapya huanza kwa TGS D. Suala la usafiri hilo no kweli kunamabadilko yamefanyika. Mimi naunga mkono hoja kwa hili ni matumizi mabaya ya rasilimali pesa.
Hopeless! Vipi hao Maafisa Tarafa wasio na kazi yoyote zaidi kukisaidia Chama Cha Mapinduzi sio matumizi mabaya ya fedha?
 
Teh tehe teheeee he. Thi ni nyinyi wafanyakazi mlimchagua Jk miezi michache tu iliyopita wakati keshawatangazia kutokuzihitaji kura zenu?
Nyerere aliwafunga baba zetu mikanda, ila yeye alikuwa na sababu ya vita ya Uganda.
Jk yeye ana sababu gani ya kuwafunga wafanyakazi mkanda? ni vita ya kujivua gamba? Mbona hao mafisadi ni swahiba zake na wala hajathubutu kuwachukulia hatua za kisheria ila propaganda za kisiasa?
MTAKOMA KUMCHAGUA ****** KTK NAFASI YA JUU YA NCHI.
MTAFUTENI MGAYA HUENDA AKAWAPA ZA MBAYUWAYU.
.
 
Hizi ni habari za kweli.Mimi nimeajiriwa january 24-2011.Wakati nafuatilia madai ya nauli na fedha ya mizigo ambayo sikumaliziwa kulipwa mkuu wangu wa idara akaniambia standing order(waraka) ume badiliswa hivi karibuni.Kwasababu kwamba mtu anaye anza kazi ana mzigo gani?.Nchi ime uzwa wana badili waraka(standing order)kwakuwa hawana fedha.Mani yangu ni kwamba mimi nadhani tuwapeleke mahakamani(tuishitaki serikali)wale wote tulio ajiriwa kwa standing order ya mwaka 2009.
 
Kama hali ndiyo hii sijui hata tunapoelekea.............kazi ipo mliambiwa wa kumchagua mkazidi kuwaweka kileleni magamba hata kwa kuchakachua. Tuyaone wote sasa
 
Umeishiwa hoja lala ujambejambe kuliko kuleta ushuzi wako humu hakuna kitu kamna hicho posho zote zimelipwa na waliopanda mishahara wamelipwa hakuna aliyeshushwa mshahara we kimavi tu unawanga humu kenge weeeee

Kweli kuna haja ya lugha ya namna hii?
 
Sasa ni dhahiri, KIKWETE nchi imemshinda. Serikali yake imeshindwa kulipa watumishi stahili zao. Mishahara yashushwa, posho zapukutishwa na hakuna malipo kwa wafanyakazi wapya wanaoanza kazi. Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing Orders) zafanyiwa marekebisho.

Kwa mujibu wa Gazeti la Serikali Namba 10 vol. 92 la 11/3/2011 na Government Notice (GN) 104 ya 11/03/2011, Standing Orders za 2009 zimefanyiwa marekebisho ambapo pamoja na mambo mengine sasa mtumishi wa serikali anayeanza kazi HATALIPWA gharama za kuhamisha mizigo yake na posho yake ya kujikimu sasa itakuwa ni kwa siku saba (7) badala ya 14 kama ilivyokuwa kabla ya marekebisho hayo (tazama kif. L.6 na jedwali J/I kolamu ya [vi] na GN 104 ya 11/3/2011). Ikumbukwe kuwa ni mwaka jana tu yaani kuanzia Julai 1, 2010 ndipo (bila shaka ili kupata kura za wafanyakazi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge 2010) Serikali ilipopandisha viwango vya posho kwa watumishi wapya na wale wanaohamia vituo vipya. Kabla ya Julai 1, 2010 mtumishi alipokuwa akihama alikuwa analipwa TSh 1,000/= kwa tani-km x tani 3 [kwa maafisa] (au tani 1.5 kwa watumishi wa kada ya chini) x km y (umbali kwenda kituo kipya); na posho ya kujikimu kwa mujibu wa stahili yake (siku 14 kwa kuhama na siku 7 kwa watumishi wapya). Lakini Serikali kuanzia Julai 1, 2010 ilipandisha pesa hizo kwa kuongeza tani kuwa 5 kwa maafisa na tani 3 kwa hao wengine (tazama Standing Orders za 2009 zilizoanza kutumia Julai 1, 2010) na posho ya kujikimu kuwa ya siku 14 kwa wote yaani watumishi wapya na wale wanaohamia vituo vipya vya kazi.

Kama hilo halitoshi Serikali tena imeshusha mishahara ya watumishi wa kada mbali2 ikiwa ni pamoja na kada ya afya kimya2 bila kutangazia umma kwa kuunganisha MADARAJA ya mishahara ambapo daraja la juu linateremshwa na kuunganishwa na daraja la chini yake. Kwa mfano kwa watumishi wa afya waliokuwa ktk ngazi ya mshahara TGHS B.1 (425,290/=) sasa wamerundikwa ktk TGHS A. 1 (260,400/=): haya ni maangamizi. Wafanyakazi mko wapi? Na viongozi wa wafanyakazi je, na nyie mko wapi? Nicolas Mgaya uko wapi? Ninamkumbuka mpanganaji marehemu RWEGASIRA wa TRAWU ... Cha ajabu ni kuwa wafanyakazi wa chini ndio wanaoguswa na makato haya. Wakubwa kama vile Wabunge, Mawaziri nk wanazidi kurundikiwa mihela tena pasipo kufanya kazi ya maana.

Wachambuzi wa mambo wanabaini kuwa haya ni matokeo dhahiri ya KIKWETE kushindwa kuongoza nchi na kwamba hajui la kufanya ili kuikwamua nchi kutoka hapa ilipo. Tungoje tuone, bila shaka kuna mengine mengi.

Kwa mtumishi wa umma ukisema unampunguzia mshahara na posho haimsumbui kichwa, ndiyo maana kuna baadhi yao wanadiriki hata kusema wapo tayari kufanya kazi serikalini bure. Ukitaka umpe taabu basi weka usimamizi mzuri wa manunuzi ya serikali(ambamo anajipatia 10%), Weka PCCB kila ofisi ya umma inayotoa huduma kwa umma(ambamo wanajipatia Rushwa).
 
Kama wanataka maandamano yasiyo na kikomo wathubutu kufuata hiyo standing order yao.
 
mmmmhh! mleta thread umetoroka mirembe au?!yani umshushe mtu mwenye mshahara wa laki nne na kitu mpaka laki 2. Tena usawa huu wa sukari buku 2 kwa kilo!
Itakua wanataka vita sasa, haiwezekani wewe usitudanganye!
 
Ianwezekana wewe ndio umetoroka Mirembe!!!!!
 
Back
Top Bottom