Serikali yasaini mikataba mingine saba CHINA yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.7

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573

SERIKALI ya Tanzania leo imeingia mikataba saba na makampuni sita ya Kichina yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.7 (Sh. trilioni 2.72) ambazo zitawekezwa kwenye ujenzi wa miradi ya umeme na nyumba za makazi na biashara.

Makubaliano ya uwekezaji huo mkubwa yameshuhudiwa leo (Alhamisi, Oktoba 24, 2013) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wengine wa Serikali baada ya kusainiwa kwa mikataba saba ya uwekezaji katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa nchi.
Utiaji saini huo ulifanywa mara baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano la Uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na China (Tanzania China Business Forum) uliofanyika kwenye hoteli ya Dong Fang, jijini Guangzhou jimboni Guangdong, China. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Baraza la Biashara la China Afrika (China Africa Business Council-CABC) linashirikisha wafanyabiashara wa China na Tanzania.
Mikataba iliyosainiwa leo ni kati ya Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya Tabiau Electric Apparatus Stock Co Ltd (TBEA) ambao ni kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme ya msongo mkubwa wa 400kV katika Gridi ya Taifa inayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini Mashariki hadi Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO, Bw. Felchesmi Mramba ndiye aliyesaini mkataba huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 692.7. Bw. Mramba pia alisaini mkataba mwingine na kampuni ya Shanghai Electric Power ambayo ndio itajenga mtambo wa Kinyerezi III.
Mkataba mwingine uliotiwa saini na Mramba ni kati ya Tanesco na kampuni ya China Gezhouba Group Corporation (CGGC) ambao wamekubali kuendeleza mradi wa umeme unaotokana na nguvu ya maji wa Rumakali ambao uko katika mikoa ya nyanda za juu kusini. Miradi hiyo miwili bado iko kwenye ngazi ya upembuzi yakinifu hivyo gharama zake bado hazijajulikana.
Kampuni ya Mkonge Energy Systems Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara wa Tanzania, Bw. Salum Shamte ilitiliana saini mkataba na kampuni ya Sino Hyro Resources Ltd kwa ajili ya kuendeleza umeme wa nguvu za maji wa Masigira. Mradi huo unagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 136.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Nehemia Mchechu aliweka saini mkataba baina ya NHC na kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE) kwa ajili ya kuliwezesha kifedha shirika hilo liweze kujenga nyumba mbalimbali za makazi na biashara nchini. Mradi huo una thamani ya dola za Marekani milioni 500.
Bw. Mchechu pia aliwekeana saini mkataba mwingine na kampuni ya Poly Technologies (POLY) wa kuwa na uhusiano kifedha na kiufundi kati ya kampuni hizo ya kichina na NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi na biashara huko Masaki wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Gharama za mradi huo ni dola za Marekani milioni 200.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo (NDC) Bw. Gideon Nassari kwa niaba ya shirika lake aliingia mkataba na kampuni ya China ya Dalian International Economic & Technical Gooperation Group (CDIG) na Kampuni ya Hydro China Kunming Engineering Corporation kwa ajili ya kujenga kituo cha utafiti na mafunzo ya nishati mbadala. Mradi huo una thamani ya dola za Marekani milioni 136.
Mramba na Mchechu kwa nyakati tofauti walisema kwamba utekelezaji wa miradi hiyo utaanza wakati wowote kwani mambo mengi walishayakamilisha kwenye mazungumzo.
Wakati utambulisho, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bibi Julieth Kairuki alisema jumla ya Makampuni na Taasisi 46 zinazowekeza na kufanya biashara Tanzania zinashiriki katika Kongamano hilo ambapo kwa upande wa China, CABC wameandikisha makampuni 44 yatakayoshiriki kwenye kongamano. Katika Kongamano hilo, TIC imewasilisha mada ya mazingira ya uwekezaji Tanzania na Bodi ya Utalii na Shirika la nyumba la Taifa wamewasilisha mada zinazohusu uwekezaji kwenye sekta ya Nyumba na fursa za utalii nchini Tanzania
Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya nane ya ziara yake ya kikazi kwa mwaliko wa Serikali ya China bado anaendelea na mikutano mbalimbali na leo usiku atazungumza na Watanzania waishio Guangzhou.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 24, 2013
 
Vipi kuhusu mikataba hiyo kuwekwa wazi ili sisi wenye nchi yetu, tunaolipa kodi ya kuendesha hiyo serikali tuone kilichomo ndani ya hiyo mikataba? Nani anawaamini hawa maCCM linapokuja suala la mikataba? Jamani wabunge hebu ilazimisheni hii serikali iweke hadharani hii serikali mikataba, inawezekana ni kwa manufaa yetu lakini tuwekewe hadharani.

Sitaki kuamini kuwa wachina wanatupenda sana hadi kusaini mikataba 7 + 17 only in 2013.
 
7+19=26.....???? Kama una macho na akili itumie kuifatilia serikali kwa jicho la 3:

Kuna uwezekano mpya wa kupokea silaha toka china pamoja na makombora, wachina sio wajinga kuwa waje kuwekeza tanzania wakati chama kinaelekea kifa, najua wamehakikishiwa usalama wa mali zao na wao wakaahidi kuongezea serikali vifaa maalumu kwa kazi maalumu, tungekuwa tunanufaika na hii mikataba direct wala tusingekuwa na mswali kama haya vichwani mwetu ila since ni indirect lazima tuhoji sana.

Wachina ndiyo watakao chelewesha mabadiliko hapa nchini, wamejiingiza kila sehemu na wengi wao wanaipaka serikali mafuta kwa mgongo wa chupa, pamoja na yote tutaikomboa jamii ili ifaidi rasimali zake kwa uhuru na upana Inshaallaaah
 
7+19=26.....???? Kama una macho na akili itumie kuifatilia serikali kwa jicho la 3:

Kuna uwezekano mpya wa kupokea silaha toka china pamoja na makombora, wachina sio wajinga kuwa waje kuwekeza tanzania wakati chama kinaelekea kufa, najua wamehakikishiwa usalama wa mali zao na wao wakaahidi kuongezea serikali vifaa maalumu kwa kazi maalumu, tungekuwa tunanufaika na hii mikataba direct wala tusingekuwa na mswali kama haya vichwani mwetu ila since ni indirect lazima tuhoji sana.

Wachina ndiyo watakao chelewesha mabadiliko hapa nchini
 
SERIKALI ya Tanzania leo imeingia mikataba saba na makampuni sita ya Kichina yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.7 (Sh. trilioni 2.72) ambazo zitawekezwa kwenye ujenzi wa miradi ya umeme na nyumba za makazi na biashara.

Makubaliano ya uwekezaji huo mkubwa yameshuhudiwa leo (Alhamisi, Oktoba 24, 2013) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wengine wa Serikali baada ya kusainiwa kwa mikataba saba ya uwekezaji katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa nchi.
Utiaji saini huo ulifanywa mara baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano la Uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na China (Tanzania China Business Forum) uliofanyika kwenye hoteli ya Dong Fang, jijini Guangzhou jimboni Guangdong, China. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Baraza la Biashara la China Afrika (China Africa Business Council-CABC) linashirikisha wafanyabiashara wa China na Tanzania.
Mikataba iliyosainiwa leo ni kati ya Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya Tabiau Electric Apparatus Stock Co Ltd (TBEA) ambao ni kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme ya msongo mkubwa wa 400kV katika Gridi ya Taifa inayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini Mashariki hadi Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO, Bw. Felchesmi Mramba ndiye aliyesaini mkataba huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 692.7. Bw. Mramba pia alisaini mkataba mwingine na kampuni ya Shanghai Electric Power ambayo ndio itajenga mtambo wa Kinyerezi III.
Mkataba mwingine uliotiwa saini na Mramba ni kati ya Tanesco na kampuni ya China Gezhouba Group Corporation (CGGC) ambao wamekubali kuendeleza mradi wa umeme unaotokana na nguvu ya maji wa Rumakali ambao uko katika mikoa ya nyanda za juu kusini. Miradi hiyo miwili bado iko kwenye ngazi ya upembuzi yakinifu hivyo gharama zake bado hazijajulikana.
Kampuni ya Mkonge Energy Systems Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara wa Tanzania, Bw. Salum Shamte ilitiliana saini mkataba na kampuni ya Sino Hyro Resources Ltd kwa ajili ya kuendeleza umeme wa nguvu za maji wa Masigira. Mradi huo unagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 136.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Nehemia Mchechu aliweka saini mkataba baina ya NHC na kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE) kwa ajili ya kuliwezesha kifedha shirika hilo liweze kujenga nyumba mbalimbali za makazi na biashara nchini. Mradi huo una thamani ya dola za Marekani milioni 500.
Bw. Mchechu pia aliwekeana saini mkataba mwingine na kampuni ya Poly Technologies (POLY) wa kuwa na uhusiano kifedha na kiufundi kati ya kampuni hizo ya kichina na NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi na biashara huko Masaki wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Gharama za mradi huo ni dola za Marekani milioni 200.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo (NDC) Bw. Gideon Nassari kwa niaba ya shirika lake aliingia mkataba na kampuni ya China ya Dalian International Economic & Technical Gooperation Group (CDIG) na Kampuni ya Hydro China Kunming Engineering Corporation kwa ajili ya kujenga kituo cha utafiti na mafunzo ya nishati mbadala. Mradi huo una thamani ya dola za Marekani milioni 136.
Mramba na Mchechu kwa nyakati tofauti walisema kwamba utekelezaji wa miradi hiyo utaanza wakati wowote kwani mambo mengi walishayakamilisha kwenye mazungumzo.
Wakati utambulisho, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bibi Julieth Kairuki alisema jumla ya Makampuni na Taasisi 46 zinazowekeza na kufanya biashara Tanzania zinashiriki katika Kongamano hilo ambapo kwa upande wa China, CABC wameandikisha makampuni 44 yatakayoshiriki kwenye kongamano. Katika Kongamano hilo, TIC imewasilisha mada ya mazingira ya uwekezaji Tanzania na Bodi ya Utalii na Shirika la nyumba la Taifa wamewasilisha mada zinazohusu uwekezaji kwenye sekta ya Nyumba na fursa za utalii nchini Tanzania
Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya nane ya ziara yake ya kikazi kwa mwaliko wa Serikali ya China bado anaendelea na mikutano mbalimbali na leo usiku atazungumza na Watanzania waishio Guangzhou.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 24, 2013

mbona ule wa uswiz wa kurudisha fedha hawataki kusaini?
 
Serikali sikivu inawatumikia watu wake kwa usikivu mwisho wa siku wanaopinga wataona aibu wenyewe.
 
TANUNU YOTE TANZANIA NZIMA CCM TIARI IKO FUKONI,LENGO KUPWA NUNUA MPAKA MTU MOJA MOJA SABABU MENYEWE PENDA ZANA 10% TAKA 2020 NUSU IWE CHiNA NUSU IWE TANZANIA SAWASAWA ELEWA JUMBE HIYO,MALALA SANA SANA NIE
 
Serikali sikivu inawatumikia watu wake kwa usikivu mwisho wa siku wanaopinga wataona aibu wenyewe.

Na wewe kila siku unasifia sifia tu, wekeni mikataba wazi hata 5 tu kati ya hyo 26 walau tujitathimini, haya mambo yakutufanya sie mapoyoyo tumechoka nayo
 
Tunawakabidhi wachina na wageni wengine kila sector, Nina wasi wasi na Terms za kwenye hiyo mikataba lazima Kuna vipengele vigumu sana kufanya pesa zao kuwa salama, yaani kutufunga tusije kuwa na sauti ikitokea mgongano...kumbuka richmond?!!!!!! Itafika wakati kila kitu kitamilikiwa na wageni sijui titaishije..... Nina hofu iliyo kuuu.
 
7+19=26.....???? Kama una macho na akili itumie kuifatilia serikali kwa jicho la 3:

Kuna uwezekano mpya wa kupokea silaha toka china pamoja na makombora, wachina sio wajinga kuwa waje kuwekeza tanzania wakati chama kinaelekea kufa, najua wamehakikishiwa usalama wa mali zao na wao wakaahidi kuongezea serikali vifaa maalumu kwa kazi maalumu, tungekuwa tunanufaika na hii mikataba direct wala tusingekuwa na mswali kama haya vichwani mwetu ila since ni indirect lazima tuhoji sana.

Wachina ndiyo watakao chelewesha mabadiliko hapa nchini
Mbona wa hakuna mkataba wa kujenga upya reli ya kati? Anyway tujiandae kwa mabomu zaidi ya kichina.
 
Wachina kwao hatutaki na wanatubagua. Kibaya zaidi hata wakija hapa hawatupendi na wanatubagua ingawa tuko kwenye nchi yetu. Hakuna ukoloni mbaya kama wa Kichina...
 
Back
Top Bottom