BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,117
Haiwezekani kupambana na mafisadi kwa maneno tu wakati huo huo bado mmewakumbatia mafisadi waliojivika ngozi ya uongozi
Posted Date::10/30/2007
Serikali yapigana kujisafisha tuhuma za ufisadi
* Zaendelea kutawala kikao chao na wafadhili
* Maamuzi ya mdajala huo kutolewa Ijumaa
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
HUKU sakata la tuhuma za ufisadi likizidi kutawala mazungumzo yanayoendelea kati ya serikali na nchi 14 wahisani, serikali imejikuta kuwa katika wakati mgumu ya kufafanua kuhusu uchunguzi wa tuhuma hizo, kufuatia wahisani hao kuendelea kuhoji.
Taarifa zilizofikia gazeti hili jana kutoka ndani ya mkutano huo ulioanza juzi zinaeleza pamoja na mambo mengine, tuhuma hizo za ufisadi ambazo zimetolewa na wapinzani bado zimetawala mazungumzo hayo huku serikali ikijipanga vema kuzifafanua.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, kazi kubwa ya serikali pamoja na kueleza mafanikio ya bajeti, imekuwa ikifanya kazi ya kufafanua tuhuma hizo.
Sakata hilo la tuhuma za ufisadi ambalo liliibuliwa katika siku ya kwanza ya mkutano huo ulioanza juzi, ziliendelea kuwa ajenda nzito hadi jana.
Balozi wa Uingereza nchini Philip Perham, ambaye ni Mwenyekiti wa nch14 wahisani, aliibua upya sakata hilo siku ya kwanza ya mkutano huo, wakati wa kujadili taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2006/07.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili jana, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji alisema serikali haijapuuza tuhuma hizo na kwamba siku zote imekuwa ikizichunguza.
"Tuhuma zinazotolewa siyo kwamba hazifanyiwi kazi, tunazifanyia kazi na ndiyo maana tumeanza uchunguzi hata kuhusu EPA -(Akaunti ya Madeni ya Nje),"alisema Meghji.
Meghji alisema serikali pia imewaeleza wahisani hao kwamba hatua nyingine ambazo serikali imechukua ni pamoja na kuangalia kwa karibu mzunguuko wa fedha chafu nchini.
Alisema katika kufanikisha hilo, serikali kupitia kitengo chake maalumu cha Kuangalia Mzunguuko wa Fedha nchini (Financial Inteliigency Unit), imekuwa ikichunguza fedha zilizopatikana kwa njia chafu.
"Tumewaeleza kuwa tuna kitengo chetu cha Financial Intelligency Unit, amabcho kazi yake kubwa ni kuangalia mzunguuko wa fedha chafu, ikiwemo zilizopatikana kinyume cha sheria," alifafanua Meghji.
Waziri Meghji alisema tuhuma hizo mpya kuhusu Sh 10 bilioni zinazoelezwa kuchotwa kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa Uchaguzi mkuu wa 2005, zote zinahusu uchunguzi katika EPA.
"Utakuta mambo mengine yapo yote, yanahusu EPA na serikali inafanya uchunguzi, hakuna kiti kipya zaidi," alisisitiza Meghji.
Alisema serikali iko makini na imekuwa ikifuatilia na kuzifanyia kazi tuhuma zote hatua kwa hatua.
Meghji aliongeza kwamba majumuisho ya mkutano huo wa ndani unaondelea yatatolewa Ijumaa wiki hii.
Kuhusu uhusiano kati ya serikali na nchi hizo alisema:, " Mbona hakuna tatizo, mazungumzo yanaendelea vizuri, Ijumaa majumuisho yatatolewa, hakuna tatizo kabisa".
Hii si kauli ya kwanza kutolewa na nchi wahisani kuishinikiza serikali, kwani tayari kauli kama hiyo walikwisha itoa siku za nyuma. Baada ya kutoa msimamo huo, Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe aliwataka kutulia ili vyombo vya dola viweze kuchunguza tuhuma za ufisadi BoT.