Serikali yapiga ‘stop’ posho za madiwani Arusha

Yaani Gambo na huyu Mkurugenzi wanataka kucheza siasa za Magazetini,ambazo ni rahisi sana sana.
Hii posho ya nauli imekuwapo toka mwaka 2005 na wakati huo Jiji lilikuwa la CCM....na hii posho ya mafuta toka Baraza la Madiwani la mwaka jana chini ya Meya Lyimo mwenye mikono ya damu za watu wa Arusha lilipitisha.

Hapa Gambo anafikiri kacheza karata ya kuwauwa CHADEMA ARUSHA,anaweza akapotea mwenyewe kisiasa.Mkurugenzi kashaambiwa aijibu hiyo barua ndani ya muda muafaka sbb yeye mwenyewe anajuwa kuwa kuna upotoshaji.Hizi siasa za Gambo zinaenda kumpoteza yeye na sio CHADEMA.Ndani ya utawala wa Chadema mianya kibao ya wizi imepigwa chini na sasa watu wanatafuta mbinu kuichafua Chadema.Wakuu CHADEMA kwa Arusha ni sawa na CCM kwa Dodoma ya Wagogo!!

Wagogo hata wapatwe na njaa na kula viwavi jeshi,hawapati akili za mabadiliko,hata waangamie kwa ugonjwa wa kope na kukosa huduma za afya hawaiachi CCM....Sasa siasa za Uvinza hazishabiani na za Arusha.Mrisho Gambo jaribu kutoka kivingine
kambitza, majibu umeyaona?
Ahhh!. Historia yake ya nini hapa. Uzi huu ni kuhusu hilo tukio la posho, au ndiyo mnataka kuhamisha mjadala? Fungua uzi mwingine wa hiyo historia yake tuje kujisomea huko huko.
 
Sishangai wanatumia nguv kubw kudhoofsha cham lkin haturud nyum
 
Ha, ha, ha, kumbe Arusha Mjini kuna diwani mmoja tu wa Magamba kati ya madiwani 25! Infact Arusha Mjini is for CHADEMA. Gambo kazi anayo.
 
KWANI MSHAHARA WA DIWANI NI KIASI GANI? NAONA HIZO POSHO UKIZIJUMLISHA UNAPATA 330,000/=(LAKI TATU NA THELATHINI ELFU).
HEBU TUJUMLISHE NA MSHAHARA WAKE NDIYO TUTAWEZA KUFAHAM WANAPOKEA KIASI GANI KWA MWEZI. INAWEZEKANA HATA LAKI SABA ISIFIKE!
THEN TUANGALIE HAO WANAOKATAZA HIZO POSHO WAO WANAPOKEA KIASI GANI MWISHO WA MWEZI?
INAWEZEKANA HAO TAMISEMI MISHAHARA YAO NI KUFURU, ALAFU WANAZIONA HIZO POSHO ZA WENZAO NDIYO ZA KUPELEKA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO!
 
KATA la madiwani wa Jiji la Arusha kujiongezea posho kinyemela limechukua sura mpya baada ya serikali kupiga kupiga “stop” ulipaji wa posho hizo.

Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha linaundwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015 katika kata 24 kati ya 25 za Jimbo la Arusha Mjini.

Madiwani hao wanalalamikiwa kujiongezea posho hizo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 bila kuridhiwa na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) hatua ambayo inatafsirwa kuwa ni kwenda kinyume cha sheria na kanuni zinazoongoza serikali za mitaa.

Hatua ya serikali

Taarifa zilizopatikana juzi Jumatatu kutoka ndani ya Jiji la Arusha na kuthibitishwa na vyanzo vya uhakika zinaeleza kuwa tayari serikali imesitisha ulipwaji wa posho hizo kupitia barua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Tamisemi, Musa Iyombe.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CCE.17/443/01/109 ya Agosti 4 mwaka huu, Katibu Mkuu huyo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia kusitisha ulipwaji wa posho hizo.

Kwa mujibu wa barua hiyo posho zilizositishwa ulipwaji wake ni pamoja na posho ya mafuta shilingi 100,000, posho ya simu shilingi 150,000 na posho ya nauli shilingi 80,000.

Katika kipindi cha miezi saba tangu kuanza kulipwa kwa posho hizo Halmashauri ya Jiji la Arusha imekwishakutumia milioni 85 kuwalipa madiwani wake 34.

Katibu Mkuu ameagiza fedha zielekezwe katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa Arusha badala ya fedha za serikali kutumika kunufaisha kundi la watu wachache.

Aidha Katibu Mkuu huyo katika barua yake ameainisha kuwa katika majiji mengine kama Dar es Salaam na Mwanza posho ya nauli ni kati ya shilingi 10,000 na 25,000 hivyo hakuna mantiki ya madiwani wa Arusha kujilipa posho ya nauli ya shilingi 80,000.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Jiji aliwasomea barua hiyo wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango jumatatu wiki hii saa nne asubuhi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jiji.

“Baada ya kusomwa kwa barua hiyo wajumbe wa kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake, Kalist Lazaro, pamoja na Mbunge Godbless Lema walishikwa taharuki wakilalamikia hatua hiyo ya serikali,” kinaeleza chanzo chetu kutoka ndani ya kikao hicho.

Aliongeza mtoa taarifa wetu, “Hali ilikuwa tete kutokana wajumbe wa kamati hiyo kuilamu serikali kuwa imefanya uamuzi huo kwa malengo ya kuwakomoa kisiasa.”

Mkurugenzi abana matumizi

Katika hatua nyingine chungu kwa madiwani na watumishi wa Jiji la Arusha Mkurugenzi, Athuman Kihamia, amepiga marufuku malipo ya fedha za malipo ya saa za ziada kazini (over time).

Taarifa ambazo hata hivyo hazikuthibitishwa zinaeleza kuwa hatua hiyo ya kufuta utaratibu wa watumishi kujilipa malipo ya saa za ziada kazini itaokoa fedha nyingi kwani halmashauri hiyo ilikuwa ikitumia zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa watumishi kujilipa fedha hizo.

Mkurugenzi huyo pia amepiga marufuku safari za watumishi nje ya halmashauri mpaka ithibitike kuwa safari hiyo ni muhimu sana na inaweza kuathiri shughuli za halmashauri au serikali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Jiji, mkurugenzi huyo pia amepiga marufuku magari ya halmashauri kufanya kazi zilizo nje ya mipango ya serikali.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Kihamia alithibitisha kuchukua hatua hizo kwa malengo ya kubana matumizi yasiyo na lazima na kuongeza kuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kuhusu malipo ya posho za madiwani mkurugenzi huyo alijibu: “Kwa sasa niko kwenye kikao cha Kamati ya Fedha lakini pia maadili hayaruhusu taarifa za kikao hiki kutolewa kwa vyombo vya habari au watu wasiohusika.”

Juhudi za kumpata Meya Kalist Lazaro hazikuweza kufanikiwa lakini Mbunge wa Arusha Mjini, Lema akizungumzia suala hilo alisema; “Katibu Mkuu (Wizara ya Tamisemi) amepotoshwa kwa sababu posho kama ya nauli ilikuwapo tangu mwaka 2005 wakati baraza la madiwani ni la CCM na posho ya mafuta ilipitishwa na baraza lililopita ambalo meya alikuwa wa CCM, Gaudance Lyimo. Kwa hiyo tumemwagiza mkurugenzi ajibu barua ya katibu mkuu ndani ya saa 24.”

Katika hatua nyingine, taarifa zaidi zinaeleza kuwa tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Arusha imekwishaanza uchunguzi wa malipo ya posho hizo na madiwani wamekwishapewa maagizo ya kuzirejesha.

Raia Mwema
Machadema ni mafisadi yasiyojali wanyonge
 
Posho ya simu 150,0000 kwa mwezi? uwiii mbona ukijiunga na kifurushi cha elfu kumi na tano tu unaongeaa mfululizo mwezi mzima hadi unachokwa.DIwani simu laki na hamsini Aiseeee.Wezi kweli hawa.
acha ushabiki mandazi jibu hoja hii ambayo ndio chanzo cha tatizo---- amepotoshwa kwa sababu posho kama ya nauli ilikuwapo tangu mwaka 2005 wakati baraza la madiwani ni la CCM na posho ya mafuta ilipitishwa na baraza lililopita ambalo meya alikuwa wa CCM, Gaudance Lyimo
 
Machadema ni mafisadi yasiyojali wanyonge
amepotoshwa kwa sababu posho kama ya nauli ilikuwapo tangu mwaka 2005 wakati baraza la madiwani ni la CCM na posho ya mafuta ilipitishwa na baraza lililopita ambalo meya alikuwa wa CCM, Gaudance Lyimo
 
Hizi ni Njama za ccm kuichafua CDM, CDM ni Chama cha wananchi wapo hata tayari kufanya kazi bila Posho , na kuanzia sasa Hiyo Posho hatuchukui hata ikiwa 10,000?
Machadema bana bana! Yaani posho mjiongezee nyinyi wenyewe na lawama muwape ccm! Ha kweli akili zenu sawa na za Ng'ombe
 
KATA la madiwani wa Jiji la Arusha kujiongezea posho kinyemela limechukua sura mpya baada ya serikali kupiga kupiga “stop” ulipaji wa posho hizo.

Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha linaundwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015 katika kata 24 kati ya 25 za Jimbo la Arusha Mjini.

Madiwani hao wanalalamikiwa kujiongezea posho hizo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 bila kuridhiwa na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) hatua ambayo inatafsirwa kuwa ni kwenda kinyume cha sheria na kanuni zinazoongoza serikali za mitaa.

Hatua ya serikali

Taarifa zilizopatikana juzi Jumatatu kutoka ndani ya Jiji la Arusha na kuthibitishwa na vyanzo vya uhakika zinaeleza kuwa tayari serikali imesitisha ulipwaji wa posho hizo kupitia barua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Tamisemi, Musa Iyombe.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CCE.17/443/01/109 ya Agosti 4 mwaka huu, Katibu Mkuu huyo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia kusitisha ulipwaji wa posho hizo.

Kwa mujibu wa barua hiyo posho zilizositishwa ulipwaji wake ni pamoja na posho ya mafuta shilingi 100,000, posho ya simu shilingi 150,000 na posho ya nauli shilingi 80,000.

Katika kipindi cha miezi saba tangu kuanza kulipwa kwa posho hizo Halmashauri ya Jiji la Arusha imekwishakutumia milioni 85 kuwalipa madiwani wake 34.

Katibu Mkuu ameagiza fedha zielekezwe katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa Arusha badala ya fedha za serikali kutumika kunufaisha kundi la watu wachache.

Aidha Katibu Mkuu huyo katika barua yake ameainisha kuwa katika majiji mengine kama Dar es Salaam na Mwanza posho ya nauli ni kati ya shilingi 10,000 na 25,000 hivyo hakuna mantiki ya madiwani wa Arusha kujilipa posho ya nauli ya shilingi 80,000.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Jiji aliwasomea barua hiyo wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango jumatatu wiki hii saa nne asubuhi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jiji.

“Baada ya kusomwa kwa barua hiyo wajumbe wa kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake, Kalist Lazaro, pamoja na Mbunge Godbless Lema walishikwa taharuki wakilalamikia hatua hiyo ya serikali,” kinaeleza chanzo chetu kutoka ndani ya kikao hicho.

Aliongeza mtoa taarifa wetu, “Hali ilikuwa tete kutokana wajumbe wa kamati hiyo kuilamu serikali kuwa imefanya uamuzi huo kwa malengo ya kuwakomoa kisiasa.”

Mkurugenzi abana matumizi

Katika hatua nyingine chungu kwa madiwani na watumishi wa Jiji la Arusha Mkurugenzi, Athuman Kihamia, amepiga marufuku malipo ya fedha za malipo ya saa za ziada kazini (over time).

Taarifa ambazo hata hivyo hazikuthibitishwa zinaeleza kuwa hatua hiyo ya kufuta utaratibu wa watumishi kujilipa malipo ya saa za ziada kazini itaokoa fedha nyingi kwani halmashauri hiyo ilikuwa ikitumia zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa watumishi kujilipa fedha hizo.

Mkurugenzi huyo pia amepiga marufuku safari za watumishi nje ya halmashauri mpaka ithibitike kuwa safari hiyo ni muhimu sana na inaweza kuathiri shughuli za halmashauri au serikali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Jiji, mkurugenzi huyo pia amepiga marufuku magari ya halmashauri kufanya kazi zilizo nje ya mipango ya serikali.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Kihamia alithibitisha kuchukua hatua hizo kwa malengo ya kubana matumizi yasiyo na lazima na kuongeza kuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kuhusu malipo ya posho za madiwani mkurugenzi huyo alijibu: “Kwa sasa niko kwenye kikao cha Kamati ya Fedha lakini pia maadili hayaruhusu taarifa za kikao hiki kutolewa kwa vyombo vya habari au watu wasiohusika.”

Juhudi za kumpata Meya Kalist Lazaro hazikuweza kufanikiwa lakini Mbunge wa Arusha Mjini, Lema akizungumzia suala hilo alisema; “Katibu Mkuu (Wizara ya Tamisemi) amepotoshwa kwa sababu posho kama ya nauli ilikuwapo tangu mwaka 2005 wakati baraza la madiwani ni la CCM na posho ya mafuta ilipitishwa na baraza lililopita ambalo meya alikuwa wa CCM, Gaudance Lyimo. Kwa hiyo tumemwagiza mkurugenzi ajibu barua ya katibu mkuu ndani ya saa 24.”

Katika hatua nyingine, taarifa zaidi zinaeleza kuwa tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Arusha imekwishaanza uchunguzi wa malipo ya posho hizo na madiwani wamekwishapewa maagizo ya kuzirejesha.

Raia Mwema

Kama watu. Watu Wameuza. Hadi. Nyumba. Kwa ajili. Ya. Udiwani. Unategemea nin
 
amepotoshwa kwa sababu posho kama ya nauli ilikuwapo tangu mwaka 2005 wakati baraza la madiwani ni la CCM na posho ya mafuta ilipitishwa na baraza lililopita ambalo meya alikuwa wa CCM, Gaudance Lyimo
Kwa kiwango gani?
 
acha ushabiki mandazi jibu hoja hii ambayo ndio chanzo cha tatizo---- amepotoshwa kwa sababu posho kama ya nauli ilikuwapo tangu mwaka 2005 wakati baraza la madiwani ni la CCM na posho ya mafuta ilipitishwa na baraza lililopita ambalo meya alikuwa wa CCM, Gaudance Lyimo
Sh ngapi?????
 
huna hoja,Bajeti ya 2016/17 Arusha CCM wanahusikaje? these are mere kicks of a dying horse (in articulo mortis) at the point of death. CHADEMA wanaonekana ni majizi na nia yao ni wizi na sio siasa za utumishi.
kwani umeambiwa maswala ya posho huwa yanarekebishwa kila mwaka wa fedha????
 
Ndio hapo.. wanaanza kuwaibia wananchi... wakati majiji mengine posho zao hazijaongezwa.. wao wamejiongezea kifisadi..

Hata kama wangejiongezea sh. 1 ni uwizi...

Mkuu hapo arusha kuna madiwani wamekomaa kuutafuta huo udiwani kwa nguvu zote., wengine wameuza hadi nyumba sasa wanataka sehemu ya kufidia hizo hela zao
 
Vijana wa Lumumba buku7Fc mnachekesha sana, nanyi mnataka mlipwe sawa na madiwani???
 
Back
Top Bottom