Serikali yapiga ‘stop’ posho za madiwani Arusha

Serikali yapiga ‘stop’ posho za madiwani Arusha

Hii nayo ni habari inayopwaya kwasababu vyanzo vyake vyote kila kimoja kinavutia kwake (Habari ya nani kasema). Tunategemea habari za kichunguzi na uchambuzi sio kama hii inayopelea.

Mwandishi alipaswa kuwa na kumbukumbu za malipo ya posho za madiwani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita nk.
Hiyo habari imepikwa!
 
Lete ya kiuchunguzi mkuu Tuchuje.
Ukitaka kujua habari ni ya kupika na yenye lengo la kupotosha,kwanini posho hizo zisilinganishwe na za hapo jijini Arusha baraza lililopita?Yaani reference gazeti linakimbilia Dar?
 
Suala siyo kuziondoa,suala ni nani chanzo cha posho hizo?.
Kuna watu wanasema ni Ccm katika kipindi kilichopita (ingawa sina uhakika)

Kinachonishangaza ni wapinzani wa Ccm kulialia baada ya viongozi wa serikali kuziondoa!.
 
Ukitaka kujua habari ni ya kupika na yenye lengo la kupotosha,kwanini posho hizo zisilinganishwe na za hapo jijini Arusha baraza lililopita?Yaani reference gazeti linakimbilia Dar?
Lete iliyokuwa sahihi.
 
"Msimamo wetu ni kufuta posho zote za makalio" by Silinde June 2016.
Inashangaza kuona Lema hapendi msimamo wa chama, yeye analilia posho za makalio wakati chama kinakataza posho za makalio.
Ajabu ni kwamba zimekuwa zikilipwa tangu Mkapa anakabidhi madaraka kwa JK, yaani 2005
 
Sasa Lema alikuwa anapambana na mkuu wa wilaya ya Arusha,,sasahivi atapambana na mkuu wa mkoa wa Arusha..hahaaa Hii inaitwa usiye mpenda kaja[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yaani Gambo na huyu Mkurugenzi wanataka kucheza siasa za Magazetini,ambazo ni rahisi sana sana.
Hii posho ya nauli imekuwapo toka mwaka 2005 na wakati huo Jiji lilikuwa la CCM....na hii posho ya mafuta toka Baraza la Madiwani la mwaka jana chini ya Meya Lyimo mwenye mikono ya damu za watu wa Arusha lilipitisha.

Hapa Gambo anafikiri kacheza karata ya kuwauwa CHADEMA ARUSHA,anaweza akapotea mwenyewe kisiasa.Mkurugenzi kashaambiwa aijibu hiyo barua ndani ya muda muafaka sbb yeye mwenyewe anajuwa kuwa kuna upotoshaji.Hizi siasa za Gambo zinaenda kumpoteza yeye na sio CHADEMA.Ndani ya utawala wa Chadema mianya kibao ya wizi imepigwa chini na sasa watu wanatafuta mbinu kuichafua Chadema.Wakuu CHADEMA kwa Arusha ni sawa na CCM kwa Dodoma ya Wagogo!!

Wagogo hata wapatwe na njaa na kula viwavi jeshi,hawapati akili za mabadiliko,hata waangamie kwa ugonjwa wa kope na kukosa huduma za afya hawaiachi CCM....Sasa siasa za Uvinza hazishabiani na za Arusha.Mrisho Gambo jaribu kutoka kivingine

Sasa hivi ni mkuu wa mkoa siameshatoka kivingine?? Au ndio kapotea kisiasa?? SHUBAAABEKKIII!!!!!!
 
KATA la madiwani wa Jiji la Arusha kujiongezea posho kinyemela limechukua sura mpya baada ya serikali kupiga kupiga “stop” ulipaji wa posho hizo.

Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha linaundwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015 katika kata 24 kati ya 25 za Jimbo la Arusha Mjini.

Madiwani hao wanalalamikiwa kujiongezea posho hizo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 bila kuridhiwa na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) hatua ambayo inatafsirwa kuwa ni kwenda kinyume cha sheria na kanuni zinazoongoza serikali za mitaa.

Hatua ya serikali

Taarifa zilizopatikana juzi Jumatatu kutoka ndani ya Jiji la Arusha na kuthibitishwa na vyanzo vya uhakika zinaeleza kuwa tayari serikali imesitisha ulipwaji wa posho hizo kupitia barua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Tamisemi, Musa Iyombe.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CCE.17/443/01/109 ya Agosti 4 mwaka huu, Katibu Mkuu huyo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia kusitisha ulipwaji wa posho hizo.

Kwa mujibu wa barua hiyo posho zilizositishwa ulipwaji wake ni pamoja na posho ya mafuta shilingi 100,000, posho ya simu shilingi 150,000 na posho ya nauli shilingi 80,000.

Katika kipindi cha miezi saba tangu kuanza kulipwa kwa posho hizo Halmashauri ya Jiji la Arusha imekwishakutumia milioni 85 kuwalipa madiwani wake 34.

Katibu Mkuu ameagiza fedha zielekezwe katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa Arusha badala ya fedha za serikali kutumika kunufaisha kundi la watu wachache.

Aidha Katibu Mkuu huyo katika barua yake ameainisha kuwa katika majiji mengine kama Dar es Salaam na Mwanza posho ya nauli ni kati ya shilingi 10,000 na 25,000 hivyo hakuna mantiki ya madiwani wa Arusha kujilipa posho ya nauli ya shilingi 80,000.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Jiji aliwasomea barua hiyo wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango jumatatu wiki hii saa nne asubuhi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jiji.

“Baada ya kusomwa kwa barua hiyo wajumbe wa kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake, Kalist Lazaro, pamoja na Mbunge Godbless Lema walishikwa taharuki wakilalamikia hatua hiyo ya serikali,” kinaeleza chanzo chetu kutoka ndani ya kikao hicho.

Aliongeza mtoa taarifa wetu, “Hali ilikuwa tete kutokana wajumbe wa kamati hiyo kuilamu serikali kuwa imefanya uamuzi huo kwa malengo ya kuwakomoa kisiasa.”

Mkurugenzi abana matumizi

Katika hatua nyingine chungu kwa madiwani na watumishi wa Jiji la Arusha Mkurugenzi, Athuman Kihamia, amepiga marufuku malipo ya fedha za malipo ya saa za ziada kazini (over time).

Taarifa ambazo hata hivyo hazikuthibitishwa zinaeleza kuwa hatua hiyo ya kufuta utaratibu wa watumishi kujilipa malipo ya saa za ziada kazini itaokoa fedha nyingi kwani halmashauri hiyo ilikuwa ikitumia zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa watumishi kujilipa fedha hizo.

Mkurugenzi huyo pia amepiga marufuku safari za watumishi nje ya halmashauri mpaka ithibitike kuwa safari hiyo ni muhimu sana na inaweza kuathiri shughuli za halmashauri au serikali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Jiji, mkurugenzi huyo pia amepiga marufuku magari ya halmashauri kufanya kazi zilizo nje ya mipango ya serikali.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Kihamia alithibitisha kuchukua hatua hizo kwa malengo ya kubana matumizi yasiyo na lazima na kuongeza kuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kuhusu malipo ya posho za madiwani mkurugenzi huyo alijibu: “Kwa sasa niko kwenye kikao cha Kamati ya Fedha lakini pia maadili hayaruhusu taarifa za kikao hiki kutolewa kwa vyombo vya habari au watu wasiohusika.”

Juhudi za kumpata Meya Kalist Lazaro hazikuweza kufanikiwa lakini Mbunge wa Arusha Mjini, Lema akizungumzia suala hilo alisema; “Katibu Mkuu (Wizara ya Tamisemi) amepotoshwa kwa sababu posho kama ya nauli ilikuwapo tangu mwaka 2005 wakati baraza la madiwani ni la CCM na posho ya mafuta ilipitishwa na baraza lililopita ambalo meya alikuwa wa CCM, Gaudance Lyimo. Kwa hiyo tumemwagiza mkurugenzi ajibu barua ya katibu mkuu ndani ya saa 24.”

Katika hatua nyingine, taarifa zaidi zinaeleza kuwa tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Arusha imekwishaanza uchunguzi wa malipo ya posho hizo na madiwani wamekwishapewa maagizo ya kuzirejesha.

Raia Mwema
hapo lema kumtaka mkurugenzi amjibu katibu mkuu ndani ya saa 24 kutetea ufisadi wa madiwani wa cdm ndio udikteta uchwara.
 
"Msimamo wetu ni kufuta posho zote za makalio" by Silinde June 2016.
Inashangaza kuona Lema hapendi msimamo wa chama, yeye analilia posho za makalio wakati chama kinakataza posho za makalio.
Ndo muone hawa hawafai kupewa nchi watafanya ufisadi Mkubwa kwa vile wapo na fisadi kuu
 
Hili suala limekaa kisiasa. Nafikiri kila watu wanaweza kujilipa kutokana na wanavyoingiza. Hivyo si ajabu wao kujilipa posho hizo kama wanaingiza mapato ya kutosha.
Pia ukumbuke walowachagua wanataka maendeleo na halmashauri zinapaswa kuimarisha miundo mbinu kupitia mapato ya ndani si kutegemea serikali kuu tu
 
Sasa hivi ni mkuu wa mkoa siameshatoka kivingine?? Au ndio kapotea kisiasa?? SHUBAAABEKKIII!!!!!!
Hata Mulongo alitoka kuwa DC mpaka RC....Lakn sasa analima ngogwe bonde la Mto Ruvu huko Same,Kijiji cha Mahole
 
Serikali kuu kuingilia serikali za Halmashauri ni ubakaji wa katika utawala.
Pumbavu ccm, posho hizi toka mwaka 2005 lkn kwa kuwa wameshindwa na halmashauri kuchukuliwa na chadema Leo wanajidai posho eti nyingi shame ccm
 
Haya yamekuwa maajabu, chama kilichopinga ufisadi sasa kinatetea ufisafi kwa nguvu zote! Soon kitakuwa chakavu
Posho ni ufisadi, hivi wewe unajua raisi na msafara wake wanachukua shilingi ngapi kwa siku, eti ufisadi posho ni ufisadi
 
Naona mshamba ni wewe ambaye unashindwa kujua kuwa posho hizo ziliwekwa na baraza la madiwani wa CCM,baraza la madiwani wa CHADEMA walichofanya ni kuongeza posho.
Tukundane hujui sera na msimamo wa CDM ni hakuna posho za makalio, ikawaje badala ya kuziondoa wao ndio wakajiongozea kwenye halmashauri zao ?
 
Back
Top Bottom