Serikali yapiga ‘stop’ posho za madiwani Arusha

Serikali yapiga ‘stop’ posho za madiwani Arusha

Posho ya simu 150,0000 kwa mwezi? uwiii mbona ukijiunga na kifurushi cha elfu kumi na tano tu unaongeaa mfululizo mwezi mzima hadi unachokwa.DIwani simu laki na hamsini Aiseeee.Wezi kweli hawa.[/QUONakuunga mkon mkuu mie kwa elfu 15/mwezi naongea hadi kieleweke
 
Yaani Gambo na huyu Mkurugenzi wanataka kucheza siasa za Magazetini,ambazo ni rahisi sana sana.
Hii posho ya nauli imekuwapo toka mwaka 2005 na wakati huo Jiji lilikuwa la CCM....na hii posho ya mafuta toka Baraza la Madiwani la mwaka jana chini ya Meya Lyimo mwenye mikono ya damu za watu wa Arusha lilipitisha.

Hapa Gambo anafikiri kacheza karata ya kuwauwa CHADEMA ARUSHA,anaweza akapotea mwenyewe kisiasa.Mkurugenzi kashaambiwa aijibu hiyo barua ndani ya muda muafaka sbb yeye mwenyewe anajuwa kuwa kuna upotoshaji.Hizi siasa za Gambo zinaenda kumpoteza yeye na sio CHADEMA.Ndani ya utawala wa Chadema mianya kibao ya wizi imepigwa chini na sasa watu wanatafuta mbinu kuichafua Chadema.Wakuu CHADEMA kwa Arusha ni sawa na CCM kwa Dodoma ya Wagogo!!

Wagogo hata wapatwe na njaa na kula viwavi jeshi,hawapati akili za mabadiliko,hata waangamie kwa ugonjwa wa kope na kukosa huduma za afya hawaiachi CCM....Sasa siasa za Uvinza hazishabiani na za Arusha.Mrisho Gambo jaribu kutoka kivingine
Mkuu Gambo bado sana, siasa zake ni za kukomoana na viongozi wengine, Mwaka 2014 alisumbuana sana na aliekua mkurugenzi wa korogwe mji Mzee Kalinjuna kuhusu mabilioni ya viwanja vilivyouzwa Korogwe mji, aliongea unafiki mbele ya JK ila JK alimshushua mbele ya hadhara na kiherehere kilimshuka
 
Ahhh!. Historia yake ya nini hapa. Uzi huu ni kuhusu hilo tukio la posho, au ndiyo mnataka kuhamisha mjadala? Fungua uzi mwingine wa hiyo historia yake tuje kujisomea huko huko.
Nahisi napoteza muda
 
[emoji23][emoji23] Sijaona swali pale mkuu hamna cha maana ulichoandika. Acha maneno mengiii, ukiona jambo lina kasoro leta la kwako lisilo na kasoro tutasoma tutachuja.
Huo ndiyo mwisho wako wa kufikiri. Kama huwezi kuchambua jambo kwa umoja wake kutokana na mazingira yanayoleta jambo hilo na mahusiano yake na nyakati husika, nasadiki wewe ni miongoni mwa mbumbumbu wa habari nchini.
 
Hili suala limekaa kisiasa. Nafikiri kila watu wanaweza kujilipa kutokana na wanavyoingiza. Hivyo si ajabu wao kujilipa posho hizo kama wanaingiza mapato ya kutosha.
 
Kwa nini serekali inapofanya makosa haitaki kukubali kuwa walifanya makosa,makosa Yao wanayatupia kwa watumishi umma Ili waonekane kuwa Wao ndio wenye makosa,wanaposema kuwa wafanya kazi walikuwa wanajilipa overtime wana maanisha nini?.

Ina maana kuwa wafanya kazi ndio waliojiwekea utaratibu wa kulipa overtime?na wakishafanya overtime kwa maamuzi yao wenyewe wanakwenda kuchukua fedha bank na kujilipa?pasipo serekali kuhusika?Kama watumishi walikuwa wanajilipa wenyewe overtime kwa kutumia fedha za umma ni kwa nini serekali haijawapeleka Mahakamani kwa kosa la wizi?.

Mpango wa masaa ya ziada yaliwekwa na serekali kwa mtumishi wa umma kwa ajili ya kumalizia zile kazi ambazo zimeshindikana kumalizwa ndani muda uliopangwa au Kama kutatokea zarula yoyote ambayo itamfanya mtumishi wa umma kuitwa akiwa mapunzikoni baada ya muda wa kazi kupita kwenda kufanya hiyo kazi ya zarula iliojitokeza.

Muda wa saa za kazi unapokwisha na wakati huohuo Kuna kazi ambazo zilitakiwa zifanyike na kumalizika siku hiyo hiyo,baada muda huo kumalizika,mtumishi wa umma aondoke kurudi nyumbani huku akiwaamewaacha wananchi ambao walikuwa bado kuhudimiwa ndani ya muda unaotakiwa wakiwa wamepanga foleni kusubiri huduma hiyo?.

Na vipi itakapotokea zarula wakati mtumishi wa umma Yuko nyumbani kupunzika baada ya muda wa kuwepo kazini kumalizika,Ina maana asiende kwenye zarula hiyo kwa kuwa siyo muda wa kazi?.
 
Wakati Gambo na CCM yake wakiendeleza majungu Chadema inatekeleza ahadi zake kama kawaida. Kwenye hafla hii Mkurugenzi wa jiji atakuwepo hata Gambo akitaka anaweza kuja kushuhudia watu wanavyofanyakazi.
=======================

Halmashauri ya Jiji la Arusha ambayo inayoongozwa chama Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) leo itagawa zaidi ya milioni 400 kwa vikundi 96 vya ujasiriamali kutoka katika kata 25 ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi

Zoezi hili ni la awamu ya kwanza, na linafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Halmashauri ya Arusha Mjini. Haijawahi kufanyika katika kipindi chote cha uongozi wa CCM zaidi ya miaka 50 iliyopita, ambapo wamekuwa wakizitumia kwa matumizi wanayojua wenyewe badala ya walengwa.

Katika hafla hiyo ya makabidhiano ya hundi mikopo hiyo nafuu kwa umma wa Arusha Mjini, itafanyikia katika ukumbi wa Azimio kuanzia saa tano asubuhi.

Mh Meya wa Jiji Kalisti Lazaro ndiye atakayesimamia zoezi hili kama Meya wa Jiji linaloongozwa na Chadema akiataambatana Mkurugenzi, na maofisa wengine wa Jiji.

Meya Kalisti amesema zoezi hili ni endelevu na Halmashauri yake itahakikisha lengo kuu la kuwatumikia wananchi na kuinua hali zao za kimaisha linatimia kama walivyoahidi sambamba na kuhakikisha kero za msingi kama maji, huduma za afya, barabara na umeme zinamalizwa kabisa.

Wanaarusha na wapena Maendeleo mnakaribishwa!!.
=======================
 
Posho ya simu 150,0000 kwa mwezi? uwiii mbona ukijiunga na kifurushi cha elfu kumi na tano tu unaongeaa mfululizo mwezi mzima hadi unachokwa.DIwani simu laki na hamsini Aiseeee.Wezi kweli hawa.
Ngoja nikitafute kifurushi cha 150K, lazima watakuwa wanapiga simu kuongea na watalii,
 
Huo ndiyo mwisho wako wa kufikiri. Kama huwezi kuchambua jambo kwa umoja wake kutokana na mazingira yanayoleta jambo hilo na mahusiano yake na nyakati husika, nasadiki wewe ni miongoni mwa mbumbumbu wa habari nchini.
Lete yako iliyokamilika Mkuu [emoji23][emoji23] wala sioni shida iko wapi!. Hahahaha kudadeki watu mnaojifanya kila sehemu mnaigiza kujenga hoja mnanichekeshaga kweli hahaha mnavyojifanya kuyapanga maneno basi ili muonekane mnajua [emoji23][emoji23][emoji23] Siasa inatuharibia sana watu.
 
huna hoja,Bajeti ya 2016/17 Arusha CCM wanahusikaje? these are mere kicks of a dying horse (in articulo mortis) at the point of death. CHADEMA wanaonekana ni majizi na nia yao ni wizi na sio siasa za utumishi.
Ina maana kuwa hata kilicho andikwa kwenye thread hujakisoma?kwani mimi nimenukuu kilicho andikwa.
 
BREAKING NEWS.
MRISHO GAMBO ATEULIWA MKUU WA MKOA ARUSHA.
-------------------------

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU MPYA WA MKOA WA ARUSHA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.
 
Acha ushamba, posho hizo zimewekwa na baraza la CDM, ndiyo kisa cha ugomvi kati ya Gumbo na Lema.
Naona mshamba ni wewe ambaye unashindwa kujua kuwa posho hizo ziliwekwa na baraza la madiwani wa CCM,baraza la madiwani wa CHADEMA walichofanya ni kuongeza posho.
 
Back
Top Bottom