Serikali yaongeza makato ya kununua umeme kimya kimya mpaka 2%

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,819
9,171
Habari wadau wa JF,

Serikali yetu inayojali wanyonge imeongeza Tozo hadi kufikia 2% ukinunua umeme kwa kutumia mitandao ya simu na bank. Tatizo sio kuongeza ila wamefanya kimya kimya bila kutoa taarifa kuhusu ongezeko hilo lisilo na kichwa wala miguu.

Serikali nyingine kipindi hiki cha korona wanajaribu kuwaondolea ugumu wa maisha wananchi wao,tumeshuhudia baadhi ya nchi wakigawa chakula na wengine kuwataka landlords wawasamehe kodi etc ila serikali yetu sikivu kipindi hiki cha uchumi wa wananchi kupiga mweleka wameona pia wawaongezee mzigo mwingine.

Inawezekana mimi nilikuwa sijui ila kwasasa unakatwa 2% ya fedha unayonunulia umeme i.e Ukinunua umeme wa Buku make sure una balance ya 1020 Tsh kwenye account yako, chini ya hapo imekula kwako.
 
Nikwel aisee mwanzoni ilikua 1.1% sasa hivi ni 2% .
Huu ni uhuni , sababu zipi zimepelekea huko,
Alafu bongo mambo yakishapanda hua hayashuki , siku nyingine Mara utasikia imefika 3
 
Na wamepeleka kwenye mitandao wanajua huko watz 90% ni zero kabisa, kwanza hawatauliza au kutaka kufuatilia, pili hata ukifuatilia nani atakupa msaada, tatu wengi hatuna nuda na kuibiwa au kukatwa pesa ndogo kiasi cha 2%..!

Hii ndiyo Afrika bana, "i can't breath"
 
Naona yeye kasikia leo(angekuwa mnunuaji asengekuja na huu Uzi)
Tatizo sio kusikia leo wala jana,wakati wanaweka tozo walitangaza watakuwa wanachaji 1.1% ukinunua umeme sasa iweje wawe wanachaji 2% kununua umeme bila kutoa taarifa kwa walaji(consumer)? Kama wewe ulikuwa unajua unaweza kutupa maelezo ya kutosheleza lini walipandisha hiyo tozo? Unaweza kushare link ya hiyo taarifa.
 
Savimbi Jr,

Uko sahihi mkuu nilikuwa Tsh.10000 nikaambiwa salio halitoshi Hadi nilipo kopTimiza tsh.500 ndiyo nikata unit 28 na kubaki na tsh.300
Huu ni wizi kama Wizi wa Services Charges! Yaani nakatwa mara mbili VAT na Pia Tozo ya Manunuzi kununua Umeme!! Tunaona 2% ni ndogo lakini REA wana 3% na wanaweza kusambaza umeme vijijini,Serikali inatuibia sana wanyonge!! Huo umeme wa REA wanaojisifia kusambaza vijiji vyote nchi nzima mapato yao ni 3% sasa ebu fikiria 2% serikali inatuibia Tsh ngapi?
 
Mi nafikiri tofauti kidogo juu ya jambo hili, makato ya 2% hayaendi serikalin ila yanaenda kwa mtoa huduma yaani kampuni ya simu iliyokupa huduma ya kununua umeme na ndiyo maana katika recept hukut hyo charge
 
Ndiyo iwe 2%?!?? Kwani wamenifuata nyumbani!
 
Mi nafikiri tofauti kidogo juu ya jambo hili, makato ya 2% hayaendi serikalin ila yanaenda kwa mtoa huduma yaani kampuni ya simu iliyokupa huduma ya kununua umeme na ndiyo maana katika recept hukut hyo charge
Nilitaka kusema hili.
Watu tunalalamika bila kufikiri kwa kina.
Hebu nenda vituo vya LUKU na ununue umeme wa 10,000 uone kama utakatwa Sh. 200.
Ukikatwa kwenye simu ujue kampuni ya simu ndio imefanya hivyo.
 
Watu walalamishi sana ila sio wafatiliaji wa taarifa sahihi.
 
Watu walalamishi sana ila sio wafatiliaji wa taarifa sahihi.
Kwani Kampuni ya simu inaweza ikakurupuka na kupandisha tu tozo bila baraka za serikali(TCRA)? Lini tulipewa taarifa ya kupanda kwa hiyo TOZO? Mapato yoyote ya kampuni yanakatwa kodi mwisho wa siku na kurejesha serikalini hivyo na hili kuongezeka kwa tozo ni mapato pia yanaenda serikalini kama kodi kutoka kampuni husika.
 
Aliekuuzia token ni tanesco sio kampuni ya simu, kampuni ya simu kawa daraja la kukuunganisha wewe mlaji na mtoa huduma tu, nasisitiza tena, unapokuwa na Tsh 5000.00/= kwenye simu yako ukataka kununua umeme wa hela hyohyo hutopata huduma cos anaekuunganisha na tanesco hatopata kitu
 
Back
Top Bottom