Serikali yaongeza kodi kwenye Betting

Serikali yaongeza kodi kwenye Betting

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
5,581
Reaction score
10,110
InShot_20250612_214050444.jpg

Serikali imeongeza kiwango cha kodi kwa washindi wa michezo ya kubashiri (Betting) ambapo Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema Ongezeko la kiwango hiko cha fedha kitakachopatikana, asilimia 70 itaenda katika mfuko wa serikali kupambana na Ukimwi na asilimia 30 kuchangia mfuko wa bima ya afya.

“Kufanya marekebisho kwenye sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41. Kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15,” amesema Waziri Mwigulu Nchemba bungeni Dodoma leo wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026. ✍️
 
10% yenyewe ilitufanya tukose uzalendo kwa kubetia kampuni wa nje, sembuse hiyo 15%
 
Kumbe 15% tu, watu wanakomaa na VAT 18% na bado wanatabasamu
 
Nilikuwa nafikiri bunge ndio lina uwezo wa kuongeza au kupunguza kodi tena baada ya kujadiliwa, kupitishwa na kusainiwa na Raisi, kumbe mtu mmoja tuu kutoka wizarani anaweza kuwapiga kodi mamilioni ya watanzania akiamua tuu
We ngedere waziri ametoa mapendekezo wabunge wataanza kuijadili wiki ijayo. Vijana wa sk hz ni watupu kabisa
 
Hivi tabu tunayopata wakamaria wakati tuna kusanya odds serikali wanazijua?!

Kwa nini serikali nayo isiwe inaweka mkeka ili wapate hizo hela?!

Wanajua uchungu wa kubeti kweli hao viongozi?! Wako bungeni tu! Wawe wanachambua na timu za kuwekea mkeka!
Kmnyoook!
 
Kwa nini serikali nayo isiwe inaweka mkeka ili wapate hizo hela?!

Wanajua uchungu wa kubeti kweli hao viongozi?! Wako bungeni tu! Wawe wanachambua na timu za kuwekea mkeka!? Manyoook!
Haha
 
Nikilipia mkeka wa buku....serikalini inawafikia shilingi ngapi...

Au kodi ya serikalini ni hadi nishinde bet....lini sasa.
Mbona mzaha huu....kushinda kwenyewe ni kibarua.....
Lameki madelu akili hana...
Simwiti Mwigulu Nchemba kwasababu sio jina lake halali.........
 
View attachment 3366167
Serikali imeongeza kiwango cha kodi kwa washindi wa michezo ya kubashiri (Betting) ambapo Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema Ongezeko la kiwango hiko cha fedha kitakachopatikana, asilimia 70 itaenda katika mfuko wa serikali kupambana na Ukimwi na asilimia 30 kuchangia mfuko wa bima ya afya.

“Kufanya marekebisho kwenye sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41. Kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15,” amesema Waziri Mwigulu Nchemba bungeni Dodoma leo wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026. ✍️
Nchi imebarikiwa rasilimali lukuli ila mmeziuza na mna tujazia matozo tupu.
NO REFORMS NO ELECTION
 
Nilikuwa nafikiri bunge ndio lina uwezo wa kuongeza au kupunguza kodi tena baada ya kujadiliwa, kupitishwa na kusainiwa na Raisi, kumbe mtu mmoja tuu kutoka wizarani anaweza kuwapiga kodi mamilioni ya watanzania akiamua tuu
Unaposema mtu mmoja alafu unajua huyo ni waziri na eneo lake lakufikisha ilo pendekezo la kodi ni bungeni una maanisha nini?..au wewe kwako bunge na waziri ni hujui anafanyaje kazi.Muwe mnajielimisha kwanza kabla yakujiandikia jambo kwa kukosoa wakati kumbe wewe ndiye hujui.
 
Back
Top Bottom