Serikali yalaani maoni ya Mhariri wa gazeti Mwananchi

Bukanga

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
2,857
1,936
Oktoba 3, 2015 MWANANCHI: Serikali imelaani maoni ya Mhariri wa Mwananchi katika toleo la juzi ikidai yalikuwa na lengo la kupotosha mafanikio ya Rais Jakaya Kikwete na haiba ya Tanzania mbele ya Jumuiya ya Kimataifa.

Madai hayo yalitolewa jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, wakati Mhariri Mtendaji wa Mwananchi akiwa ameomba radhi jana kwenye ukarasa wa tatu wa gazeti hili kuhusiana na maoni hayo yaliyokuwa na kichwa cha habari ‘Rushwa inazidi kutudhalilisha mbele ya dunia'. "Katika ukurasa wa 10 wa gazeti letu jana (juzi), Jumatano, tulikuwa na maoni yaliyokuwa yanasomeka; Rushwa inazidi kutudhalilisha mbele ya dunia.

"Hatukuwa na nia mbaya ya kuonyesha kuwa viongozi wetu wa Serikali walikwenda kuomba msaada Marekani, bali lengo letu lilikuwa ni kuonyesha kwamba Tanzania bila rushwa inawezekana. Tunaomba radhi kwa wote ambao walikwazika na maoni hayo."

Hata hivyo, licha ya Mwananchi kuonyesha msimamo wake huo, bado Mwambene aliendelea kulilaani akisema maoni hayo yalikuwa na makosa ya uhalisia na kujaa upotoshwaji.

"Kwa lugha ya kawaida tunasema tahariri hiyo imeongea uongo wa wazi, inao ukweli wa nusu na imejaa upotoshwaji ambao tunaamini umefanywa kwa makusudi ili kutia doa mafanikio ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na haiba ya Tanzania mbele ya Jumuiya ya Kimataifa," alisema.

Mwambene alisema maoni hayo yanaonyesha ni jinsi gani Mwananchi limejipambanua kuwa halifurahii mafanikio ya Tanzania.

Alisema Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Milenia (MMC) haikuwa imezuia kutoa msaada wa dola 472 milioni za Marekani na kwamba kwenye kikao chake cha Septemba iliipongeza Serikali kwa kufanya vizuri katika vigezo vyote vinavyostahili kupata misaada kupitia MMC.

Alisema isipokuwa MCC walitoa tahadhari kuwa iwapo tathimini ya kupiga vita rushwa itaonyesha Tanzania imeshuka zaidi katika kigezo hicho msaada kwake utaahirishwa.

"Ukweli Bodi ya MCC haikuwa imefanya maamuzi kuhusu kutoa misaada bali ilikuwa imetoa angalizo," alisema Mwambene.

Alisema Rais Kikwete hakukutana na kiongozi wa MCC nchini Marekani kwa lengo la kumbembeleza aionee Tanzania huruma na kuipatia misaada kama ilivyodaiwa.

Alifafanua kuwa kiongozi huyo aliomba ahadi ya kukutana na Kikwete na kumueleza MCC haina kikwazo kwa Tanzania kupata msaada huo baada ya kufanya vizuri katika kigezo cha kupambana na rushwa.

Hata hivyo alisema tathimini ya upigaji vita rushwa haifanywi na MCC, bali huomba kazi hiyo ifanywe na Benki ya Dunia (WB) na taasisi nyingine duniani. "Hivyo kama ni kubembeleza Rais angeenda Benki ya Dunia," alisema Mwambene.



MAONI YALIYOLAANIWA


Septemba 30, 2015, MWANANCHI: Hatua iliyokuwa imechukuliwa hivi karibuni na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) ya Marekani kuzuia msaada wa Dola 472 milioni kwa Tanzania kwa maelezo kwamba nchi yetu imeshindwa kuchukua hatua za kuridhisha kupambana na rushwa, bila shaka itakuwa iliwasononesha na kuwaghadhibisha wananchi wengi kutokana na aibu ya Tanzania kuonekana mbele ya jumuiya ya kimataifa kama moja ya nchi vinara wa rushwa duniani.

Itakumbukwa kwamba wiki mbili zilizopita, Ubalozi wa Marekani nchini ulitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba bodi hiyo ya MCC ilionyesha wasiwasi juu ya mwenendo wa mapambano ya Serikali ya Tanzania dhidi ya rushwa, hivyo kuzuia kutolewa kwa fedha hizo hadi itakapofuzu kigezo cha udhibiti wa rushwa katika tathmini ya shirika hilo iliyopangwa kufanyika mwaka ujao.

Kama tulivyosema hapo juu, uamuzi huo wa MCC ulipokewa na wananchi wengi kwa masikitiko makubwa, siyo kwa sababu ya kukosa fedha hizo, bali kutokana na ukweli kwamba nchi yetu iliyokuwa ikiheshimika na kusifika duniani kote kama ya mfano, sasa imo katika kundi la mataifa yanayotajwa kwa rushwa.

Hata hivyo, katika hali nyingine, siku 10 baada ya taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani, Serikali ilitoa taarifa kwamba Bodi ya MCC imeridhia kuipatia Tanzania msaada huo uliokuwa umezuiliwa na kwamba fedha hizo zitaanza kutolewa mapema mwakani. Taarifa hiyo ilisema kwamba hatua hiyo ilifikiwa wiki iliyopita baada ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi waandamizi wa MCC jijini New York, akiwamo Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCC, Dana Hyde na kuelezwa kwamba Tanzania imetimiza masharti ya kupata fedha hizo, kikiwamo kigezo cha kukabiliana na rushwa kilichokuwa kikwazo hapo awali.

Sisi tunasema kama Bodi ya MCC imechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha pasipo kuacha shaka kuhusu dhamira ya Serikali ya Tanzania kupambana na rushwa, hakika inastahili pongezi.

Bodi hiyo ya MCC itakuwa imetambua kwamba fedha inazotoa kama msaada kuendesha miradi ya maendeleo kamwe haziwezi kufanya kazi iliyokusudiwa katika mazingira ya rushwa, ambayo vitendo hivyo vinafanywa kuwa utamaduni katika mifumo ya utendaji wa serikali na taasisi zake ndani ya nchi husika.

Hatua ya Bodi ya MCC ghafla kukubali kutoa msaada huo kwa Tanzania baada ya kuuzuia, bila shaka imeacha maswali mengi kwamba pengine haikuwa imefanya utafiti wa kutosha. Sisi hatuna nia ya kujadili suala hili kwa undani, isipokuwa kusema tu kwamba taarifa zilizotolewa na Serikali ya Tanzania na ubalozi wa Marekani hapa nchini hazijitoshelezi, kwani zinajenga picha kwamba pengine viongozi wetu waliomba kwa MCC na kufanikiwa kufikia makubaliano maalumu mjini New York, hivyo MCC ikakubali kutengua uamuzi wake wa awali. Hata hivyo, hatua hiyo itatoa ahueni kwa Serikali, kwani itatekeleza miradi mbalimbali kama usambazaji wa umeme wa gharama nafuu na uimarishaji wa taasisi zinazosimamia nishati hiyo.

Tunaishauri Serikali ijifunze kutokana na aibu tuliyoipata kutokana na sakata hilo. Jina na sifa ya Tanzania vinazidi kuporomoka mbele ya jumuiya ya kimataifa kutokana na madai ya rushwa. Serikali sasa idhamirie kwamba Tanzania bila rushwa inawezekana. Vinginevyo tutaendelea kudhalilika kama ilivyotokea katika sakata hili la MCC.
 
Kinachochekesha ni kwamba mwezi wa nane MCC walizuia huo msaada kwa kisingizio cha serikali ya Tanzania kugubikwa na rushwa na ufisadi.
Mwezi wa 9 baada ya JK kwenda Marekani tunaambiwa MCC wameachia huo msaada.
Maswali ya kujiuliza;
Inamaana ndani ya mwezi mmoja swala la ufisadi limeshughulikiwa na serikali ya JK?
Je, ilikuwa ni shake down ya Obama ku-draw attention kwa watanzania kuwa watazuia hiyo misaada?
JK alivyoenda kuhakikisha huo msaada alitoa nini in return?
 
Kinachochekesha ni kwamba mwezi wa nane MCC walizuia huo msaada kwa kisingizio cha serikali ya Tanzania kugubikwa na rushwa na ufisadi.
Mwezi wa 9 baada ya JK kwenda Marekani tunaambiwa MCC wameachia huo msaada.
Maswali ya kujiuliza;
Inamaana ndani ya mwezi mmoja swala la ufisadi limeshughulikiwa na serikali ya JK?
Je, ilikuwa ni shake down ya Obama ku-draw attention kwa watanzania kuwa watazuia hiyo misaada?
JK alivyoenda kuhakikisha huo msaada alitoa nini in return?

Ukistaajabu ya zawadi ya gesi yetu kwa wachina utayaona ya MCC.....
 
Rushwa ni janga katika nchi hii. Hajawahi kupungua hata kidogo, zaidi imezidi kushamiri. Waukubali huu ukweli mchungu.
 
Hiyo ndio CCM, ichagueni tena mwezi huu muone moto zaidi ya huu wa Kikwete. Escrow ndio imesababisha yote haya na hela ya escrow ilitafunwa hadi na watu wa Ikulu
 
kama jitu moja linataka uongozi wa juu kabisa kwenye nchi kwa kutoa rushwa, tena mabilion, unategemea rushwa itaisha! UJINGA KABISA.
 
Ukweli una tabia ya kuelemea upande fulani, kwa kawaida ukweli huwa haupo katikati. Kwa hiyo ukisikia kelele za malalamiko kutoka upande fulani, basi ujue upande huo haupendi ukweli ujisimamie bali usimamiwe.
 
Ukweli ni kwamba rushwa imekuwepo tz mda mrefu ila katika serikali ya jk ndo emezidi na wameshindwa kuicontroll
 
Kuna watu wao wanadhani kuwa mwajiriwa serikalini , basi wewe unasupport tuuu kila kitu, unatetea tuu uchafu wowote. The likes of Assah are a very big blocking stone towards changes in our country. Changes in meaning of how the civil servants are supposed to be working and behave. Assah and others should remember that " the wind of change is blowing across Africa and Tanzania can not remains unchanged.
 
Hizi fedha za MCC zilizuwiwa kwa kigezo kuwa tanzania haijafanya vya kutosha kupambana na rushwa,mbona hilo liko wazi kabisa!!?? Au mwambene alikuwa safarini akhera wakati hayo yanatokea?
 
MWANANCHI ni gazeti la KENYA na ambalo katika uhaguzi wa sasa linashabikia UKAWA.

bora mwananchi la kenya linalosema ukweli kuliko uhuru la tanzania lililojaa unafiki.
 
hivi tunavyoongea hakuna umeme na ndio utawala wa kikwete wako unayemtetea. tatizo kubwa tanzania mizigo isiyochukulika ni mingi
 
MWANANCHI ni gazeti la KENYA na ambalo katika uhaguzi wa sasa linashabikia UKAWA.

mungu atafanya njia na mlango mkubwa wa kutoka katika huu utumwa na unyanyasaji ndani ya nchi hii wewe endelea na ushabiki kwa sababu kuna matunda yasiyo ya haki unayojipatia kutoka kwa hawa wanyonyaji wa hii nchi, ila hamtapigwa na mwanadam na haya yatatimia na wakati umefika nao ni baada ya uchaguzi
 
kama jitu moja linataka uongozi wa juu kabisa kwenye nchi kwa kutoa rushwa, tena mabilion, unategemea rushwa itaisha! UJINGA KABISA.

Umeambiwa serikali imeshindwa kupambana na rushwa, unaelewa content ya maoni ya mhariri au unahara tu hapa?
 
Back
Top Bottom