Serikali yakwama kukusanya madeni dhidi ya kampuni bandia

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Posted Date::5/3/2008
Serikali yakwama kukusanya madeni,kampuni bandia zilikopa
Na Jackson Odoyo
Mwananchi

SERIKALI imegonga mwamba kukusanya dola za Marekani 180 milioni (Sh 207 bilioni) kutoka kwa wafanyabiashara waliokopa kwenye mfuko wa uagizaji bidhaa kutoka nje (CIS).

Habari zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Aggrey Mgonja zimeeleza kuwa kazi ya kukusanya fedha hiyo ni ngumu na kwamba sasa serikali imeamua kutafuta kampuni wakala kukusanya fedha hizo.

Zoezi la kukusanya fedha hiyo bado limekwama pamoja na serikali kutoa tangazo la kuyataka makampuni hayo kuwa yamelipa baada ya miezi mitatu kwa tangazo lilitoka katika magazeti kadhaa ya hapa nchini Januari 26 mwaka huu lililotiwa saini Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ramadhani Khijjah.

Katika tangazo hilo serikali ilitishia kuwachukulia hatua za kisheria wale wote ambao watashindwa kulipa madeni yao katika kipindi hicho , kipindi kilichotolewa na serikali kulipa kiliisha mwezi uliopita.

Habari kutoka ndani ya serikali zinaeleza kuwa ugumu wa kukusanya fedha hizo unatokana na makampuni mengi yaliyokopa fedha hizo yalikuwa feki na kwamba vigumu kuwapata wahusika.

Fedha hizo zilikopwa na wanyabiashara, wanasiasa na baadhi ya viongozi wa serikali ambao walizitumia kwa matumizi mengine na kwamba hivi sasa wanajitahidi kuhakikisha kuwa hawalipi fedha hizo.

Mgonja kwa upande wake aliliambia gazeti hili, kuwa kutokana na kusuasua kwa zoezi hilo serikali imeamua kutafuta wakala wa kukusanya fedha hizo toka kwa wadaiwa sugu wa deni hilo.

Tunahitaji kuteuwa kampuni ya kukusanya hayo madeni na tutatumia utaratibu wa manunuzi na mpaka hivi sasa bodi ya tenda iko kwenye mchakato wa kuandaa utaratibu na hatimaye serikali itangaza zabuni na kampuni itakayo pita ndiyo itapewa kazi hiyo alisema Mgonya.

Kuanzia miaka ya 1980 mpaka 1993 Wahisani kadhaa walitoa fedha kwa ajili ya mpango maalum uliofahamika kama �Commodity Import Support (CIS) kuipa uwezo serikali wa kuimarisha uchumi wake kwa kuzipatia taasisi, makampuni, viwanda, na biashara mbalimbali uwezo wa kuagiza bidhaa na mali ghafi kutoka nje, kwa kuwa wakati ule nchi ilikuwa na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni.

Fedha za CIS zilitolewa kama mikopo yenye masharti nafuu, ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba na kwamba mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18, mkopo unakuwa na riba ya asilimia 17.

Hata hivyo, fedha zinazokusanywa kutokana na malipo ya deni hilo zilikuwa zinachangia mapato ya serikali pamoja na miradi maalum ya maendeleo baada ya makubaliano na mhisani husika.

Makampuni yasiyopungua 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huo, lakini urejeshaji wa mikopo hiyo umekuwa hauridhishi ingawa juhudi za serikali kufuatilia madeni hayo, zimegonga mwamba wakati wadaiwa wengi hawaoneshi nia ya kurejesha mikopo hiyo huku wengine wakidaiwa kufirisika.

Kwa mujibu wa tangazo la Januari 26, mwaka huu wadaiwa waliopata mkopo huo kupitia Benki ya Rasilimali (TIB), walitakiwa kuwasiliana na benki hiyo kupata kumbukumbu hizo na ambao wangeshindwa kupata kumbukumbu hizo walitakiwa kuwasiliana na Wizara ya Fedha, Idara ya Fedha za Nje kwa maelezo zaidi.

Wakati serikali ikishindwa kukusanya fedha hizo, imeshindwa pia kukusanya kiasi cha sh bilioni 133 zilizochukuliwa na wafanyabiashara kutoka katika Akaunti ya madeni ya Nje (EPA).

Pia inakabiliwa na kashfa kadhaa za ubadhirifu wa fedha za umma ikiwamo mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura Richmond ambayo serikali inalipa kiasi cha sh milioni 152 kwa siku.
 
Kutafuta wakala ina maana kwamba mgao wa serikali utazidi kupungua, kwa sababu hao wakala lazima wajikatie chao kwanza. Hii haiingii akilini kabisa utadhani hii serikali ni kibogoyo--haina meno.
 
Lazima iwe hivyo! Kama aliyekopa ndiye anayesema madeni yarudishwe unategemea nini?

Hii ndio sababu nyingine ya Mh. Mgonja kuachia wenzeke sasa kuongoza Hazina; Nina hakika hatakuwa na jipya sasa.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Yaani huu ni upuuzi wa kutafuta wakala eti aisaidie serikali kupata fedha zake.........

Huyo wakala atakuwa na nini zaidi........yaani ican't imagine huyu Mgonja bado anataka kuendeleza room UFISADI HAPA and he is still surviving!!

JK hebu tuondolee huyu Mgonja.....yaani ameshindwa kuunda task force (within serikali)kwa ajili ya kazi hiyo mpaka atafute wakala??.......Mgonja don't give us this S**T........damn
 
Back
Top Bottom