Serikali yakanusha kutokea vifo 50 vya COVID-19 kwa siku jijini Dar

Hivi, ikitokea leo Watanzania wakasambaza taarifa, kwa TV au mitandao ya kijamii kwamba Wakenya 1000 wamekufa kwa Corona, Wakenya wataamini na kushangilia? Inashangaza baadhi ya watu kuamini zaidi takwimu za nje kuliko za ndani. Hata kama una wasiwasi na takwimu za nchi yetu, kwa nini ushangilie takwimu zinazotoka nchi nyingine kuhusu nchi yako. Unafanya hivyo ili iweje? Wakenya wameripoti watu 17 tu ndio wamefarki kwa Corona hadi jana. Unaamini idadi hii? Kama watu wanaweza kusema Mlima Kilimanjaro na Oldvai Goarge viko Kenya, tena wanasema hivyo waziwazi kwenye tv, unatumia akili gani kuamini takwimu wanazotoa kuhusu Corona juu ya nchi yako? Na unaanzaje kuwaunga mkono?
hawa hawajui tz kwa umbea na uzushi haishikiki bara hili.acha mchezo wanaoucheza watajifunza tena kwetu muda si mrefu.subiri tuwaandalie kibomu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wakenya waishio hapa tz wana vipimo kujua mtu amefarki kwa covid19? Unasapot ujinga pia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanataarifiwa kuhusu situation ilivyo ili wajihadhari. Kuwataka watu wenu wajihadhari huo ni ujinga? Au unapenda na kufurahia watu wanapokutana kujadili mambo fulani lakini wanapoongea na wewe wanaongea on the slightly different subject?
 
Hata kama wakifanya hivyo Wakenya hawawezi kutaka ,,kujitetea na kujieleza“ kwetu kama sisi tufanyavyo kwao, isitoshe hizo ni TV binafsi na siyo za Serikali zinaweza kutangaza chochote, sasa kwa nini tujieleze kila mara wakiongea chochote? Hizo TV wanaongelea mambo ya Dunia nzima wanamsema Zuma, Mugabe, Museveni mbona hizo nchi hazianzi kujitetea na kujielezea kwa Wakenya?

Acheni unyonge kwa Binadamu wenzenu, ...

Serikali lazima izionye kwa kuweka sawa dipromasia, vinginevyo kunaweza kuhalibu uhusiano.
 
Tatizo taarifa sio sahihi...
Kufa kwa corona mbona ni kawaida kwani tumeanza KUFA SISI ?
lakini je hyo taarifa ni sahihi?
Mimi naona wakifa ndo vizuri maana wagonjwa wanapungua.
Mtataka mashindano badala ya kujiuliza ni kwa nini taarifa ifike kwao wakati Sisi wenyewe hatujui? Mbona wao kila siku tunatangaza za kwao kila siku hawapingi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali lazima izionye kwa kuweka sawa dipromasia, vinginevyo kunaweza kuhalibu uhusiano.


Mbona wao Wakenya hawafanyi pindi sisi tunapowasema? Kwanza hata hawajali, juzi kati Gwajima hapa kaongea mbovu kuhusu Kenya na ilitrend Kenya karibia yote, ulisikia popote Serikali ya Kenya ikijaribu kujitetea na kujielezea kumjibu Gwajima? Lkn ingekuwa kinyume chake mtu wa Dini maarufu Kenya aliyekaribu na Raisi wa Kenya aongee vile alivyoongea Gwajima kuhusu TZ, ungeona Serikali yetu kuanzia Ubalozi wetu Kenya mpaka Bunge letu lingejadili kujitetea na kujielezea, sasa kwa nini?
 
Kwa hiyo tuamini ya kuwa waliokufa mpaka sasa bado ni 16? Mnatufanya wajinga kiasi hicho? Katika siku chache binafsi nimepoteza watu watatu wa karibu. Mmoja kazikwa na Serikali jana, mwingine anazikwa na Serikali leo. Wa tatu kafariki leo asubuhi kwa changamoto ya upumuaji, hatujajua maziko yake lini. Utatuambia nini tukuelewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Dkt.Hassan Abbasi ameikosoa NTV Kenya na kusema wamechapisha taarifa za uongo baada ya kudai kuwa kwa siku ya jana April 30,2020 pekee wamefariki Watu 50 katika Mkoa DSM kutokana na corona.

“Huu ni uandishi au "uhandisi" wa habari?, inasikitisha kuona jinsi NTV Kenya inavyokuwa wakala wa uongo na uzushi, nawakumbusha wazandiki hawa kuenzi misingi ya taaluma badala ya umaamuma" -Dkt. Abbasi

Mficha maradhi kifo humuumbua








kush and Wisdom
 
Ukikutana na Mhubiri mfanya mazingaombwe anavyojitetea kuhusu "kumfufua" Marehemu ambaye hajawahi kuwa Marehemu, hadi unashangaa ni kwa nini waumini wake wanashangilia kwa kusema "Haleluyaaaa"
He he!
Unajua maana ya taarifa..??
Unajua taarifa inaathiri uchumi au siasa au jamii kiasi gani..?

Walio huko ndo huwa wanaona athari hizo moja kwa moja.. mkuu kitu bora ukakiacha tu
 
Mbona wao Wakenya hawafanyi pindi sisi tunapowasema? Kwanza hata hawajali, juzi kati Gwajima hapa kaongea mbovu kuhusu Kenya na ilitrend Kenya karibia yote, ulisikia popote Serikali ya Kenya ikijaribu kujitetea na kujielezea kumjibu Gwajima? Lkn ingekuwa kinyume chake mtu wa Dini maarufu Kenya aliyekaribu na Raisi wa Kenya aongee vile alivyoongea Gwajima kuhusu TZ, ungeona Serikali yetu kuanzia Ubalozi wetu Kenya mpaka Bunge letu lingejadili kujitetea na kujielezea, sasa kwa nini?
Ni wewe?
 
Tumepamvana na Kenya, sasa tupambane na Aljazeera
Screenshot_20200501-144825.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom