Serikali yakanusha Dkt. Kigoda kufariki dunia

Status
Not open for further replies.

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Ndugu zangu watanzania, mimi si msemaji wa Dr. Kigoda wala familia yake wala serikali. Lakini, nataka kudokeza ninachokijua. Ni kweli kuwa Dr. Kigoda yuko nchini India kwa matibabu. Kwa siku za hivi karibuni,amekuwa akilazwa ICU.

Anasumbuliwa na matatizo makubwa ya figo na ini. Tuzipuuze habari za kifo ingawa zaweza kuthibitishwa na wahusika kama ni za kweli kwa wakati na namna inayopasa. Nijuavyo, Dr. Kigoda anaendelea na matibabu ingawa hali yake si njema. Tumuombee Dr. Kigoda apate nafuu na aungane nasi kujenga Tanzania yetu.

Get well soon Comrade Abdallah Kigoda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
======

Updates:

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Taarifa Rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho ameendeleaa kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.

Imetolewa na Assah Mwambene, Msemaji Mkuu wa serikali.

Asante kwa Ufafanuzi pia kuna meseji hii pigieni simu hii namba:_

Kanusho jingine hilo tena kuna namba ya simu. ALIYESHTUSHWA sana na hii habari aipigie namba hapo chini

Kuna rafiki yangu ana udugu na Kigoda kaposti hii baada ya mm kuulizia kuhusu kifo "
Siyo kweli huo ni uzushi mimi hapa niko na mwanaye bwana Omary Abdallah Kigoda. Namba yake 0716 123 123. Huo ni uzushi wawapinzani. Kigida yuko india anasumbuliwa na maradhi ya tumbo. Na huvi leo asubuhi anaendelea vizuri."
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Taarifa Rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho ameendeleaa kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.

Imetolewa na Assah Mwambene, Msemaji Mkuu wa serikali.
 
MUNGU AMPE NGUVU NA UPONYAJI AREJEE KWA FAMILY YAKE AKIWA NA AFYA NJEMA. MUNGU BABA WA MBINGUNI NINAAMINI MAMBI YETU SISI WATANZANIA TUKIUNGANA NA FAMILIA YA Dr. UNAYASIKIA NA UTAYATENDA KAMA ULIVYO PANGA WEWE KWANI SISI WOTE NI WAKO. TUNAKUOMBA UMREJESHE AKIWA SALAMA. AMEN
 
Duh akidedi kutakua na kitu si bure.....
 
Apone haraka kwa uwezo wa anayetupa punzi Mwenyezi Mungu.
 
Ya kombani yaliletwa kama hivi hivi , yakafutwa vibaya sana lakini nani asiyejua kwamba yalikuwa kweli ?
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Taarifa Rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho ameendeleaa kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.

Imetolewa na Assah Mwambene, Msemaji Mkuu wa serikali.
Ni kweli hii ndiyo taarifa ya serikali? Du majanga!
 
I imagine people like Mwambene have impossible jobs in this country. Kukanusha vifo vya watu...ilhali wewe siyo Dr. au mtaalam wa vifo (kama yupo)? Its tough!
 
Hivi Serikali wameshakanusha juu ya zile picha za Twiga wa Ngoro ngoro? maana official page ya FB ya mwana mfalme inaonesha tarehe 28 na 29 September walikuwa mbugani Serengeti hapa Tanzania.

Wizara husika Come out please maana serikali ikikaa kimya itahisiwa ni kweli.

Kwa anayetaka jina analotumia FB huyo mwanamfalme aniPM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom