PreGE2025 Serikali yajipanga kuongeza mikopo ya wanafunzi wa stashahada

PreGE2025 Serikali yajipanga kuongeza mikopo ya wanafunzi wa stashahada

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali imejipanga kuongeza wigo wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati vinavyotoa stashahada lengo ni kuongeza idadi ya wataalamu.

Utoaji wa mikopo katika ngazi za stashahada kwa wanafunzi wa ngazi hiyo ya elimu ulianza mwaka 2023/24, kwa fani sita za kipaumbele ambazo zina uhitaji mkubwa wa wataalamu ambazo ni afya na sayansi shirikishi, ualimu wa hisabati.

Fani nyingine ni fizikia na mafunzo ya amali, uhandisi na nishati, madini na sayansi ya ardhi, kilimo na mifugo ambapo Sh48 bilioni zilitengwa kwa ajili ya wanafunzi 8,000.

Pia soma Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Akizungumza Jumanne Aprili 29,2025 wakati wa kufungua mkutano mkuu wa Shirika la Mtetezi wa Mama, Profesa Mkenda amesema Serikali ya awamu ya sita, imefanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya elimu ikiwamo ya kutoa mikopo kwa ngazi ya stashahada.

Amesema katika kuzalisha vijana wenye ujuzi, Serikali iliamua kuanza kutoa mikopo ngazi ya stashahada kwa kozi za kipaumbele na mpango wa sasa ni kuongeza wigo wa kozi zitakazonufaika na mpango huo.
 
Naomba kueleweshwa hapa,hivi hii mikopo ya Helsb Hususan meals and accommodation mahesabu yake yalifanyika kwa kuzingatia gharama za maisha mwaka gani?
Maana inawezekana walifanya mahesabu na kukadiria kiasi ambacho mwanafunzi anapaswa kukitumia miaka ya 2010 huko

Na mahesabu haya yalifanyika kipindi ambacho gharama za maisha zilikuwa chini kulinganisha na hivi sasa.
Nimeona serikali ikiongeza 1500/= kwa siku mwaka 2022 lakini binafsi sidhani kama hizi hela zinatosha kuwakimu wanafunzi na ukizingatia wengine wanategemea hizi hela kukamilisha ada

Naomba serikali ifanye upya calculations za meals and accommodation according to gharama za maisha za sasa
 
Back
Top Bottom