Serikali yaitelekeza familia ya Nyerere

Serikali yaitelekeza familia ya Nyerere

Au ulitaka uone wakiwa na vitambi na cheni kifuani,
ni watoto wa mkulima, Nyerere hakuwa mwizi; mali wangezipata wapi?

Hao watoto nao wanatakiwa wasimame kwa miguu yao.
 
Je na mashamba ya baba yake aliyokuwa mzee analima mwenyewe, tena we majina mnafanana ulitakiwa uwe kwanza kumtupia hata pamba na bring bring kabla ya kuanza kutupia lawama watu wengine. Baba alikuwa mchapakazi watoto walikuwa wa kishua sasa miaka yote toka mzee aondoke watoto hampeani tough kweli mpaka mambo yatoke nje ya familia. Serikali kweli ikununulie shati, suruali, boxer na viatu kweli karne hii??

Bi Mkubwa kiinua mgongo chake amnunulie nguo mtoto wa miaka 50 taratibu jamani, aibu yenu hii jamani manake hata nguo za mzee ziligaiwa. Yericko hili sio katika tatizo la nchi liko ngazi ya familia.

Kuna tatizo kubwa la kiitifaki katika nchi kwa sasa, itifaki kwa sasa inabei sio suala la kikatiba tena.

Ndugu yetu Andrew Nyerere hii ndio Tz aliyoipigania na kuifia Baba yako, na hawa ndio watawala aliowasomesha Mzee!
 
Wengi hawajui Andrew ni mtu wa simpo siku mingi, biashara za kujiprop hajazoea.karidhika na non-material side of life.Naamini kaamua kuwa hivyo
Huko sio kuwa "simple." Andrew aliathirika, ni schizo, anashinda ndani tu Butiama virtually maisha yake yote siku hizi. Familia inatunzwa na serikali japo haitakiwi kutunzwa. Kina Miraji na Ridhiwani nao tutawatunza, tutatunza wangapi? Kwa nini vinchi vimasikini ndo havina sense of fiscal responsibility?


ni watoto wa mkulima.
Hata Andrew Chenge na Anna Tibaijuka ni watoto wa mkulima
 
Hivi tukiacha siasa tukajadili ubinadamu tu,kwamfano tuchukue baadhi ya familia kama ya Mandela,Kenyatta,Nanyine ziko kama hii ya muasisi wataifa hili?Uko hapo ulipo ukiayatoa hayo ulionayo kwasababu ya utashi wake,tunajivuna kutokua na ukabira kama nchi nyingine kwasababu ya utashi wake,nikuombe urudie kusoma ulichoandija alafu akae ukitafakari je kwamtu mwenye hekima nisahihi kufanya kamaulivyo fanya?

Haya mawazo mgando, Nyerere alikuwa raisi and was paid for his job. Sasa na mwalimu alimfundisha nyerere naye atunzwe yeye na familia yake, maana ni kwa utashi wake ndo maana alimfundisha nyerere vizuri, The same kwa madereva waliomuendesha, maana wangeamua wangemuua kwa ajali. We appreciate his services, hii nchi imejengwa na watu wengi, manesi, wakulima, walimu nk. hawa wote walishirikiana na viongozi kujenga nchi sasa kila mtu akitunzwa na familia yake itakuwa nchi au kituo cha yatima? Hebu tuache kuona kama nyerere na familia yake ndio wanastahili kutunzwa zaidi kuliko familia zingine, kuna watu baba zao walikufa vitani uganda, kuna wajuu wa mkwawa, chabuluma nk. Hawa nao wakidai kutunzwa itakuwaje? Hii ni nchi ya utawala wa sheria, sio kituo cha yatima.
 
Chuki ilianzia 1995 Mwalimu alipomwambia kuwa asubiri kwanza Urais hadi 2005, na km hiyo 2005 Nyerere angakuwa hai asingekubali JK awe Rais. Tunakukumbuka Mwalimu, taifa linaangamia huku.

Ndiyo maana kuna wale wanaotaka kifo cha Mwalimu kichunguzwe. Tuna kiongozi ambaye angeweza kufanya lolote ili tu afike Ikulu. Bado najiuliza: alikuwa anadhani Ikulu kuna nini hasa? Umaarufu? Utajiri, kusafiri nje?
Kipindi chake kikiisha atasahauliwa kuliko kiongozi yeyote aliyewahi kuongoza Tanzania. Hana legacy yeyote ataacha isipokuwa more misery, umaskini, siasa chafu, eliticism na uongozi viza.
 
Back
Top Bottom