Serikali yaipinga Big Brother | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaipinga Big Brother

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Chenge, Oct 11, 2011.

 1. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  [h=3]Bhoke Ametuponza: Serikali Yapiga Marufuku Watanzania Kushiriki Big Brother !!!![/h]


  [​IMG]
  Serikali yaipinga Big Brother
  (Vicky Kimaro na Furaha Maugo)
  Friday, 12 August 2011 21:11


  SERIKALI imepinga Tanzania kushiriki shindano la Big Brother Afrika kwa kuwa shindano hilo linapotosha maadili ya kiafrika na kuharibu kizazi cha watoto wa Tanzania.


  Akizungumza bungeni jana, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi alisema shindano hilo ni kero kubwa kwa serikali na taifa kwa ujumla na hawajui linafundisha nini kwa jamii.


  "Hatujui linafundisha nini watoto wetu, linapotosha jamii, ni kero kubwa hatushabikii shindano hili na wanaoenda kushiriki wajue hawana baraka za serikali ndio maana hatujawahi kwenda kuwapokea na bahati yao mawasiliano yao ya kushiriki wanafanya kwa njia ya mtandao,"alisema Nchimbi.


  Alisema shindano hilo limekuwa likichochea uvunjifu wa maadili kwa washiriki na hata kwa wale wanaobaki nchini.


  Kauli ya Nchimbi imekuja baada ya wabunge kuhoji umuhimu wa shindano hilo ambalo limekuwa likichochea vitendo vya ngono kutokana na kuonyeshwa live kila kitu kinachoendelea ndani ya jumba hilo kinyume na maadili ya kiafrika.


  Hivi karibuni mshiriki wa Tanzania, Bhoke Egina alikumbwa na kashfa kubwa ya kujiingiza kwenye uhusiano wa mapenzi na mshiriki toka Uganda Enerst.  [​IMG]


  Washiriki wengine watanzania walioshiriki shindano hilo na hawakukwepa kashfa ya kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi ni Mwisho Mwampamba, Richard Benezueout na Latoya.


  Shindano hilo huandaliwa na M - Net Afrika na kurushwa moja kwa moja na kituo hicho, limekuwa likifanyika nchini Afrika Kusini kwa kushirikisha nchi zaidi ya 20 barani Afrika.


  Wakati huo huo; Wabunge wameendelea kuishutumu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushindwa kukidhi mahitaji ya wasanii, wanamichezo, wanahabari pamoja na kutunza mila destruri na utamaduni wa nchi.


  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati wa kujadili bajeti ya Wizara hiyo wabunge hao walionyesha dhahiri kusikitshwa na baadhi ya vyombo husika vilivyo chini ya Wizara hiyo, vinavyoshughulikia masula ya Michezo na Utamaduni kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha kwa kuzingatia maslahi ya wahitaji ambao wengi wao ni vijana.


  Akichangia hoja Mbunge wa Kinondoni, Iddi Mohamed Azzan alisema Wizara hiyo ina sera na sheria mbovu za zamani zisizokidhi mahitaji ya sasa kwa watu walioamua kujiajiri katika sekta ya sanaa na michezo kutokana na maendeleo sayansi na teknolojia ya sasa, watendaji ni wabovu na vyombo vilivyopewa mamlaka kama BASATA na COSOTA havifanyi kazi ipasavyo.


  "Kutokana na kuwepo kwa watendaji wabovu waliolala usingizi mzito na kutawaliwa na rushwa kamwe hatuwezi kuendelea, la sivyo sera na sheria za zamani zisizokidhi mahitaji ya walioamua kujikita katika masula ya sanaa na michezo zifanyiwe mabadiliko ya hali ya juu,”alisema Azzan.


  Kwa upande wake Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama alisema kiasi kilichotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya Idara ya Maendeleo ya Vijana hakitoshi, kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania ni vijana ambao wengi wao wamejiari katika taaluma ya habari, michezo, muziki na utamaduni.


  Hivyo aliomba bajeti katika Idara hizo iongezwe fedha ili kukidhi mahitaji ya vijana wengi waliopo vijiweni bila ajira na kushauri vijiwe hivyo vitumike kama vikundi vya maendeleo kwa kuvipatia mitaji.
  Source: Mwananchi

   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  ulikuwa wapi ndugu yangu wewe???

  ulikuwa keko au segerea?? naona haupo dunia hii kabisa.
   
 3. M

  Manyema JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  me nilijua kuna jipya...hee huyu wa wapi?
   
 4. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  tatizo la serikali yetu imejaa unafiki tu mamgapi machafu yanatokea imenyamaza tu.upuuzi tu na maamuzi yao ya kijinga
   
 5. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kwani ameandika hiyo ni habari motomoto?
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,570
  Trophy Points: 280
  vilaza wapo wengi tu humu jamvini.
   
 7. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  upupu huu.................huh
   
 8. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  upo pande zipi mkuu maana umeturudisha nyuma au ndiyo nyie mnao subiri magazeti ya miezi mitatu tumia mtandao wako vyema.. siyo kosa lako naona ndiyo umetoka kuvuna matikiti kilimo kwanza..
   
 9. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nchimbi nae wampinge? Maana nae ni mchafu tu! Kila anapoenda lazima awe ame-import! Au gere kwa mganda?
   
 10. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hii Mbona ya Siku nyingi sana..tukienda kwa mtindo huu tutafika kweli???..
  Yaan habari ya miezi mitatu nyuma ndo unaileta leo???...
   
 11. k

  kingmajay Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena mkulu
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Habari kama hii naona mitaani huitwa ndaza has kwenye vilabu vya komoni
   
 13. Barraza

  Barraza JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kupinga peke yake haitoshi, serekali ilipaswa ikataze hata matangazo yake nchini mwetu
   
 14. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kwa serikali Kuanza kusensa Chanel tunazoweza kuangalia itakua uingiliaji wa haki zetu. Ni jukumu lako mwananchi kuchagua kinacho kufaa kuangalia wewe, familia na jamii yako.
   
 15. p

  panjilwa chiwal Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ya kupigwa stop hapa nchini ni mengi tu
   
Loading...