Dah! Huyo Abbas naye ana phd? Kaazi kweli kweli. Anavyoongea lazima utilie mashaka hiyo elimu yake.Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji
watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?
Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.
Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.
Ni kwa uchunguzi upi au kwa kidhibiti kipi unavituhumu vyombo vya ndani?
Wahusika wanaeleweka kivipi? si watajeni basi nao watatoa hoja zao kujitetea?Kaa tulia wahusika wanaeleweka since day 1. Kinachowabeba ni kuwa mmeshika mpini.
Wachunguzi huru? Tukumbushane, wachunguzi hawa hawa wa Bongo ndio walifuatilia kifo cha Chacha Wangwe. Leo Mbowe anawakataa... vipi?
Wahusika wanaeleweka kivipi? si watajeni basi nao watatoa hoja zao kujitetea?
Kwani uchunguzi wa ndani so far umefikia wapi? Sio kwamba umeshindwa? Sasa kwa nini uchunguzi wa nje usiletwe?
Kwa hiyo majambazi na wanyang'anyi wote wanaoua au kujeruhi kwa kutumia silaha ikiwemo hiyo SMG uliyoitaja wanatumwa na serikali au vyombo vya usalama? Halafu nani kakuambia silaha iliyotumika kumshambulia Lissu ni SMG?Chezea washamba, si unajua hata smg kupiga ni shida japo ndio wanazotumia wakishindwa hoja?