Serikali yagoma kuwepo kwa uchunguzi huru juu ya Tundu Lissu, wadai kwani kibiti walikuja wazungu?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji




Dkt%20abbasi.jpg

watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?

Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.

Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.

msemaji%20wa%20serikali....._0.JPG
 
Dhana ya uchunguzi huru inamaana haieleweki kwel??

Uchunguzi huru hufanyika pale panapokua na mashaka kwamba vyombo vya usalama vilivyopo ama vinadhaniwa havina uwezo au vinashukiwa kuhusika kwenye mkasa.

Kwan hata ya kibiti nani alikataa usifanyike uchunguzi huru?
 
Serikali haiwezi kuthubutu. Wala hili jambo halihitaji uchunguzi. Kauli ya "msaliti kutoku-survive" inaonyesha bila shaka ayekodi hit-men wa Lissu. Uchunguzi wa nini sasa? Hata mimi nakubaliana na serikali katika hili. Kila mtu anajua anayetaka Lissu afe. Hili halihitaji uchunguzi - wa nje ama wa ndani. Tusubiri tu aje Rais mwingine huko mbele ambaye atakuwa tayari kufukuwa makaburi ili huyu bwana naye alipe kwa huu ushetani wake.
 
Wachunguzi huru kutoka nje ya nchi kwa sababu ipi? Je, vyombo vyetu haviwezi au vimeshindwa kufanya kazi hii?
Uchunguzi huru si lazima ufanywe na vyombo toka nje ya nchi. Pia kwa usalama wa nchi wachunguzi kutoka nje ya nchi hawatakiwi maana lazima wataingilia siri za dola.

Hata kama hao wachunguzi kutoka nje wakija, kuna vitu lazima watahitaji ushirikiano toka serikalini, na kama serikali ikikataa kutoa ushirikiono basi kazi yao itakuwa kazi bure.
 
Back
Top Bottom