Serikali yagoma kuwepo kwa uchunguzi huru juu ya Tundu Lissu, wadai kwani kibiti walikuja wazungu?

Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji

Dkt%20abbasi.jpg

watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?

Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.

Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.

msemaji%20wa%20serikali....._0.JPG
Wana waza kwa kutumia matako..??
 
Yaani Kibiti ndio reference ya ccm na serikali yake! Ivi wa kibiti waliwajuaje na hawa wasiojulikana wa Lissu imekuwa ngumu kujulikana. Kumbuka wa Kibiti walikuwa wanafanya kazi usiku wa giza hawa wa mchana kweupe bado hawajulikani
Yaani nchi hii mpaka aibu!!

Naanza kuamini maneno ya Zitto kuhusu "Washamba na Malimbukeni".
 
Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji

Dkt%20abbasi.jpg

watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?

Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.

Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.

msemaji%20wa%20serikali....._0.JPG

Kaka kama kumbukumbu za watu zipo sahihi, hvi ajali ya Moto ya Shule ya Shauri Tanga nani alifanya uchunguzi?, hivi Tanzania tulikiwa hatuna vyombo vya uchunguzi?, Kama Chadema hawaiamini Serikali, na Serikali nayo inasema inawezekana Chadema wanahusika kwa nini asitafutwe mtu Neutral aje amalize huu utata?
 
Kibiti ndo Bench Mark yao. Wanazania Lisu ni wa kawaida. Ina maana leo hata Kiongozi mkubwa wa nchi anaweza uwawa wakasema mbona kibiti wameuwawa wengi tu?
Naitaji tupimanee akili watanzania.. nachojua mtuhumiwa hawezi kujichunguza mwenyewe na hawawezi kukubali hao watu waje
 
Nami naungana na Serikali kutokuhitaji wachunguzi kutoka nje. Sababu kubwa ni kuwepo vyombo vyenye uwezo wa kufanya uchunguzi na mazingira ya tukio hilo.

Kama Mbowe na viongozi wa CHADEMA, wana ushahidi wa nani mhusika wautoe wazi. Mbowe, kama mbunge na KUB anaweza kupeleka hoja binafsi bungeni, kuunda Kamati Huru ya Uchunguzi, kama wanavyofanya kila siku.

Hivyo nahitimisha kwamba, Mh Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA, shambulizi la Mh Lissu, kwao wamelifanya mtaji wa kisiasa na kujipatia na mradi wa kutengeneza fedha. Maneno, matendo, na tabia yao ya kurukia matukio inaniacha na maswali kadhaa, km:
1) Ni nini ukweli wa madai ya Mh Lissu kuwa Serikali ina mkono wake katika shambulizi?

2) Ni nini dhamira ya Mh Mbowe kumficha dereva, hivi kweli ni kwa sababu ati anapata matibabu ya trauma) wakati dereva ndiye mwenye ushahidi wa kwanza kwa kilichotokea!

3) Kwa kauli ya huyo huyo dereva, kama inavyoripotiwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kwamba alifuatiliwa toka Dsm, ni kwa nini hakuchukua hatua zozote za kiusalama?

3) Kwamba dereva anawajua waliowashambulia, ni kwa nini pia hakuchukua hatua zinazostahili za usalama wake na wa boss?

Mh Mbowe, usifiche uhalifu nyuma ya pazia ya kisiasa.
 
HUYO NAYE KAJITOA UFAHAMU!
KWA HILI LA LISSU VYOMBO VYA DOLA/USALAMA VYA NDANI NDIO VINASHUKIWA HUWEZI KUJICHUNGUZA MWENYEWE.
WANAPENDA KUTUPA ELIMU YA KULINDA VITUMBUA VISIINGIE MCHANGA.
 
Hata wao wazungu wakisikia tunawaita kwa sababu za kiuchunguzi huo watatudharau japo hawatasema.ni kudhalilisha taifa
 
#G'taxi,

Kuna matukio elfu na maelfu wazungu koko hawaelewi majibu yake nchini mwao.

Ati leo tuwaite waje kutusaidia!? Tutakuwa wajinga kiwango cha lami.
 
Dhana ya uchunguzi huru inamaana haieleweki kwel??

Uchunguzi huru hufanyika pale panapokua na mashaka kwamba vyombo vya usalama vilivyopo ama vinadhaniwa havina uwezo au vinashukiwa kuhusika kwenye mkasa.

Kwan hata ya kibiti nani alikataa usifanyike uchunguzi huru?
You can say that AGAIN!
 
Nani kakwambia ni ngumu??unaweza kutuambia Kibti ilitumia muda gani hadi kuwatia nguvuni wahalifu?
Hivi kweli unalinganisha issue ya kibiti na assassination attempt ya mh TL!kweli huko lumumba mmejaa mazero brain au tuseme mnatetea matumbo yenu!Hata mtu ambaye hajui investigation ataanzia na Nissan patrol na kuhoji wale walinzi wa getini. .kifupi tu ni kuwa mtuhumiwa hawezi kujitia kitanzi yeye mwenyewe!
 
Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji

Dkt%20abbasi.jpg

watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?

Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.

Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.

msemaji%20wa%20serikali....._0.JPG
Sometimes to be quite is better ''Remember this> Any decision you make in Life you are Responsible for it and that Running a way From Problems is a Race you will never win
 
Ni kwa uchunguzi upi au kwa kidhibiti kipi unavituhumu vyombo vya ndani?
Hicho cha kukataa wachunguzi wa nje inaonyesha its obvious...waalifu wanawajua na hata kama hawawajui ila na wao wanajituhumu pia.
Madaraka mabaya sana, yanawapa binadamu viburi na kujichukulia maamuzi ya kijinga kwa kuamini kwamba kwani watafanywa nini.
 
Back
Top Bottom