Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,308
- 18,485
Serikali imefuta ndoto ya kuendeleza mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kujiridhisha kuwa itakuwa hasara kuendelea nao.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Juni 26, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mariam Kisangi.
Mradi wa Dege Eco Village ulinzishwa kwa lengo la kuwekeza fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, ambao ulilenga kuwa na faida zaidi kutokana na uwekezaji wake.
Mradi huo ulisimamishwa na Serikali na umekuwa na maswali mengi kutoka kwa wabunge na wananchi ikiwa inakaribia miaka tisa sasa tangu usimamishwe.
Serikali imekuwa ikielekeza kuwa inatafuta mwekezaji wa kuununua mradi huo ambao hadi mwishoni mwa 2023 ulikuwa na thamani ya Dola za Marekani 220 milioni (Sh501 bilioni).